in , , ,

Ni Norwich au Middlesbrough EPL

Norwich wamejipatia nafasi ya kucheza na Middlesbrough katika fainali ya mtoano wa Ligi Daraja la Pili (Championships) dimbani Wembley Mei 25 ili kupata timu ya kuingia Ligi Kuu ya England (EPL).

Norwich walivuka baada ya kuwafunga Ipswich Town 3-1 na kubaki hatua moja kuingia EPL walikoshuka hivi karibuni.

Klabu mbili ambazo zilipanda moja kwa moja kutokana na msimamo wa Championships ni Bournemouth na Watford.

Mechi hii ya mkondo wa pili ilikuja timu zote zikiwa nguvu sawa kwani mechi ya awali zilitoka 1-1 kwenye dimba la Ipswich.

Wenyeji Norwich walifungua njia Jumamosi hii kupitia kwa Wes Hoolahan kwa penati, iliyotolewa baada ya Christophe Berra kumchezea vibaya Nathan Redmond na kutolewa nje.

Wageni walisawazisha bao hilo kupitia kwa Tommy Smith lakini Redmond akawanyanyua tena washabiki wa Norwichkwa mkwaju mkali.

Cameron Jerome alifunga bao la tatu na kukata tiketi ya safari ya mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Wembley wakitoka na ushindi wa jumla ya mabao 4-2.

Matokeo hayo yanawaacha Ipswich wakibaki kujiandaa na msimu wa 14 mfululizo katika Championships na pia wamebaki bila kupata ushindi Carrow Road tangu 2006.

Middlesbrough wamefika fainali baada ya kuwafunga Brentford jumla ya mabao 5-1 katika mechi za mikondo miwili.

Norwich, au kama wanavyojulikana, The Canaries, walio kaskazini mwa London wakifundishwa na Alex Neil (33) wamekuwa wazuri msimu huu, wakishinda mechi 16 kati ya 14 tangu Neil achukue nafasi ya Neil Adams.

Ipswich sasa wamepoteza katika hatua ya nusu fainali ya mtoano mara saba kati ya nane zilizopita.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

La Liga ruksa kuendelea

Hali tete Ligi Kuu England