Walipigiana pasi murua na uhakika katika dakika za muda wa ziada kwenye mchezo wa nusu fainali ya EURO 2020 mbele ya wagumu Denmark. England walijiamini,wakatuliza akili na mpira,walipambana na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ili kufuzu hatua ya fainali.
Wakishangiliwa na mashabiki wao ndani ya dimba la Wembley, England wanaonekana kupania, licha ya mashabka kadhaa katika hatua za awali za mashindano hayo, lakini sasa wameamini kuwa ‘it’s coming home’.
Hatimaye harakati zao zikazaa matunda na sasa wanakabiliwa na jaribio la pili la kutwaa kombe hilo katika ardhi ya nyumbani kwao. Ni jaribio la pili pia kwa Gareth Southgate na ambaye amebeba roho na imani za mashabiki wa soka nchini mwake.
Mwaka 1996 England walikuwa wenyeji wa mashindano ya EURO. Imani ya mashabiki ilikuwa kubwa na waliamini watatwaa taji hilo kubwa ngazi ya kimataifa katika ardhi yao. hata hivyo haikutokea baada ya aliyekuwa kiungo wao mahiri Gareth Southgate kushindwa kupachika mkwaju wake na kuiondoa mashindanoni England katika hatua ya nusu fainali.
Kiubinadamu tangu hapo Gareth Southgate ni kama alikuwa na deni kwa wananchi wenzake. Pengine alijiuliza angewezaje kulilipa deni hilo ambalo lilicha vilio na majonzi mwaka 1996! Sasa anayo fursa nyingine, amewaleta kwenye furaha tangu alipochukua timu hiyo amekuwa akifanya jitihada za kuimarisha na kuwaaminisha kuwa anaweza kutwaa kikombe chochote.
Fainali ya Euro 2020 ndilo jaribio lake la pili, alifeli jaribio la kwanza na vipi hili akiwa kocha nalo ashindwe? Hakika ni mtihani. Ni jaribio la pili kwa England wenyewe baada ya kushindwa kwenye ardhi yao mwaka 1996, sasa wanacheza fainali katika ardhi yao, baa zao,vitongoji vyao,pub zao na kila mtaa unaguswa moja kwa moja.
Je watakubali kushindwa kwa mara ya pili katika ardhi yao? hilo nalo linahitaji kujibiwa na wao wenyewe huku wakimtazama Southgate kama mwokozi wao ambaye amewahi kuwaliza.
Tangu kuanza mashindano Juni 11 England haikuruhusu nyavu zake kutikiswa hadi kwenye mchezo wa nusu fainali ambapo walishuhudia Denmark wakitishia nafasi yao ya kulitwaa kombe hilo. Lakini mabao ya Harry Kane na lile la kujifunga wenyewe la Denmark liliwapa nafasi ya kutinga fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 safi.
Wajukuu wa Malkia Elizabeth yaani England walianza mbio za kuwania ubingwa huo Juni 13 kwa kuchuana na Croatia kwenye dimba la Wembley. Na safari yao ikaendelea hatua kwa hatua hadi kufika fainali ambayo watacheza dhidi ya vigogo wengine wa soka barani Uropa, Italia.
Je ni siri gani ya imewapa mafanikio England?
Asilimia 99 ya kikosi cha England kina wachezaji chipukizi zaidi kuliko wakati wowote ambao timu imeshiriki mashindano iwe Fainali za Kombe la Dunia au Euro ya miaka ya nyuma. Southgate anaonekana kutengeneza kikosi cha chipukizi ambacho kimetokana na vijana wengi waliounda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20.
MAKIPA:Dean Handerson (Manchester United), Sam Johnstone (West Brom) na Jordan Pickford(Everton).
MABEKI; Ben White (Brighton), Ben Chilwell(Chelsea), Conor Coady(Wolves, Reece James (Chelsea),Harry Maguire(Manchester United), Tyrone Mings(Aston Villa), Luke Shaw(Manchester United),John Stones(Manchester City), Kieran Trippier (Atletico Madrid), Kyle Walker (Manchester United).
VIUNGO; Jude Bellingham (Borussia Dortmund),Jordan Henderson(Liverpool),Mason Mount(Chelsea),Kalvin Philips(Leeds United), Declan Rice(West Ham).
WASHAMBULIAJI;Dominic Calvert-Lewinbg(Everton),Phil Foden (Manchester City), Jack Grealish (Aston Villa),Harry Kane(Tottenham Hotspurs), Marcus Rashford (Manchester United), Bukayo Saka(Arsnela), Jadon Sancho(Borussia Dortmund) na Raheem Sterling(Manchester City).
Ni wachezaji gani muhimu zaidi?
Kwa siku ya fainali England wanatakiwa kuomba sala zote kuhakikisha Kalvin Philips anakuwa na afya njema. Nyota huyo kutoka Leeds United amekuwa injini ya timu tangu Juni 13 dhidi ya Croatia hadi nusu fainali. Ni mchezaji ambaye ameonekana wazi kubeba roho ya timu katika ulinzi na mashambulizi. Baada ya Philips wamuombee sana Delcan Rice aongeze kasi wakati wa kujilinda na kushambulia.
Mwingine ni Raheem Sterling naye anatashili sifa zake. washabiki wa England wanatakiwa kuomba sala zote kuhakikisha nyota wao huyu anaamka akiwa na afya njema na kucheza kwa kiwango cha juu pamoja na kuonesha uzoefu wa aina yake katika kusaidia timu hiyo.
Ameng’arisha nyota yake
Luke Shaw ni beki wa kushoto ambaye ameonesha mabadiliko makubw amno. Ametulia, anashambulia,analinda lango na uwezo wake wa kucheza umeimarika kwa kiasi kikubwa. ni mchezaji ambaye England wanatakiwa kuomba sala zote aamke akiwa na nyota njema.
Ukuta mgumu
Harry Maguire,John Stones na Jordan Pickford wameunda safu imara ya ulinzi na ndiyo maana wamefanikiwa kuruhusu bao moja pekee katika mashindano hayo.
Licha ya makosa madogo madogo yakiwemo kukosa utulivu na umakini lakini Jordan Pickford ni golikipa mzuri na ambaye anajua kuamrisha na kupanga namna ya kucheza. Kwenye mchezo wa nusu fainali alipiga mipira mara tatu hadi nne hovyo na ikawafikia wapinzani. Lakini ni kipa maridadi kwenye mashindano haya.
Wazee wa timu Kapteni Harry na Walker
Kapteni Harry Kane amekuwa akionekana kuwatuliza wenzake mara kwa mara, lakini naye ana siri moja kubwa anaye mchezaji mwenye uwezo wa kuongoza timu uwanjani ingawa si kapteni kama yeye. ni Kyle Walker, ametulia na anaelekeza mara nyingi namna timu inavyokwenda kushambulia na amefuta makosa mengi ya mabeki wake wa namba tano na nne.
Aliyeshangaza
Mchezaji aliyeshangaza zaidi ni Harry Maguire, huyu amekuwa beki kisiki na anaonesha kile alichokifanya akiwa Leicester City na kilichowafanya Manchester United kumwaga fedha kumnunua. Amecheza vizuri na kwa utulivu, anaelekeza na kuamrisha.
Comments
Loading…