in , ,

NEYMAR UFALME HAUJENGWI SIKU MOJA

Hapana shaka yeye ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi pale PSG.

Mshahara wake ni mkubwa kiasi kwamba unaweza ukamfanya mtu yoyote awe na kiburi.

Dau lililotumika kumnunulia lilikuwa kubwa tena la kutisha, ambalo
hakuna mchezaji yoyote duniani aliyewahi kununuliwa na dau hilo.

Kitu ambacho kinamfanya awe mchezaji ghali kuzidi mchezaji yoyote duniani.

Ufalme wake ulianzia hapo, akajiona tayari yeye ndiye mmiliki wa jiji la Paris.

Maana kila jicho lilikuwa ƙlinamwangalia yeye, masikio yote yalitamani
kusikia habari zake. Jiji zima la Paris liliamini yeye ndiye yule
mfalme ajaye.

Na hilo likajidhihirisha kwenye mauzo yake ya jezi. Ambapo katika siku
ya kwanza tu jezi 10000 za Neymar zilinunuliwa.

Hii yote ilionesha Neymar alipokelewa kama mfalme hata kabla hajavaa
jezi ya PSG.

Akajiona yeye ndiye mfalme wa PSG hata kabla hajaanza kuitumikia timu yake.

Kamera za vyombo vya habari vilivyokuwa vinamumulika kila wakati
vilizidi kumwaminisha yeye ndiye mfalme pale PSG.

Hakuna alama yoyote ambayo ameiweka pale PSG ndani ya uwanja lakini
tayari alianza kuona bila yeye timu haiendi.

Akasahau kabisa kuwa timu ni zaidi ya mtu mmoja. Ndipo hapo kiburi
kikaanza kujengeka taratibu.

Pamoja na kipaji kikubwa cha Neymar, haimanishi kuwa yeye ndiye anafaa
kumpokonya kila mtu jukumu ambalo alimkuta nalo pale PSG.

Kipaji chake hakimpi nafasi ya yeye kumnyang’anya kitambaa cha
unahodha Thiago Silva.

Kipaji chake hakikuwa na nguvu ya kumtolea jukumu la upigaji penalti
Edson Cavani.

Neymar (right) and Edinson Cavani

Ila uvumilivu wake ndiyo ungemfanya yeye apewe jukumu ambalo analitamani.

Wakati huu ulikuwa mzuri kwa Neymar kuweka ufalme wake na siyo kutaka
ufalme wake PSG.

Mechi 5 pekee alizocheza PSG hazimtoshi yeye kuwa mfalme pale PSG,
anahitaji mechi nyingi tena akicheza katika kiwango kikubwa.

Anahitaji kufunga magoli mengi, kutengeneza nafasi nyingi za magoli na
kutoa pasi nyingi za magoli ili ionekane bila yeye PSG inakuwa inakosa
kitu cha muhimu.

Huu ulikuwa wakati wa yeye kutengeneza mazingira yanayoonesha kuwa
anaibeba PSG ili na yeye PSG imbebe kwa kumpa majukumu muhimu ndani ya
timu.

Kiburi siyo silaha ya yeye kutengeneza ufalme wake pale PSG, bali
kipaji chake ndiyo silaha ya yeye kutengeneza ufalme wake.

Inawezekana bonus ya Euro milioni 1 iliyo kwenye mkataba wake
ikianishwa ataipokea kama atakuwa mfungaji bora wa ligue 1 ,ndiyo
inayompa hamu ya yeye kuchukua jukumu la kupiga penalti ili mwisho wa
msimu aweze kuipata .

Ni wakati kwake kuamini anaweza kufanya kitu bora bila penalti, kipaji
chake ni kikubwa ambacho kinauwezo wa kumpa na kumfikisha popote pale.

Utulivu, uvumilivu, busara na maarifa katika utumiaji wa kipaji chake
ndivyo vitu ambavyo vinaweza kumfanya awe mfamle pale PSG, siyo njia
atakayo yeye kwa maana ufalme imara hujengwa kwa muda mrefu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KANE, JIVUE SHATI LA SHEARER

Tanzania Sports

UWEPO WA OLUNGA GIRONA NI MATUSI KWA KINA AJIB