UNAPOZUNGUMZIA mpira wenye mafanikio katika nchi yoyote, suala la kuchukua kombe ni muhimu. jambo la pili ni nafasi ya timu anayochezea mchezaji mbele ya mashabiki wa soka duniani. Lingine ni namna mipango ya timu inavyoweza kuleta matokeo haraka au kuchora taswira ya kuwa miamba ya soka katika Ligi na barani Ulaya.
Newcastle United haiwezi kumpa mafanikio Alesander Isak hadi walipofikia. Kama mchezjai anahitaji kufanya mabadiliko ni lazima azingatie nafasi ya timu anayotaka kuhamia au inayomtaka. Ikiwa timu inayomtaka inao ushawishi sokoni lakini uwezo wao uwanjani ni mdogo uwezekano wa mchezaji wa kisasa kuitosa ni mkubwa. Unaweza kutazama namna Manchester United ilivyo na sifa nyingi katika uso wa duniani. Kibiashara ni timu inayofanya vizuri lakini ndani ya uwanja bado inakabiliwa na changamoto kubwa.
Msimu uliopita Man United ilinusurika kushuka daraja. Lakini timu hiyo bado ina nguvu katika biashara. timu kama hiyo haiwezi kumvutia tu mchezaji ukiacha suala la mishahara minono na wale wenye ndoto. Ni sababu hiyo Man United imebaki kuwa timu inayovutia wachezaji wa daraja la kati.
Sasa basi kama Man United inavutia wachezaji wa daraja la kati itakuwaje kwa Newcastle United ambayo wachezaji wanaovutiwa nao ni wale wa daraja la chini ya kati. Hii inamaana Newcastle hawawezi kuitisha Man United kibiashara lakini ndani ya ujwanja angalau wameibuka na kombe msimu uliopita.
Hata hivyo kombe walilochukua Newcaste United haliwezi kumbakiza mchezaji mahiri kama Alexander Isak. Msimu uliopita alikuwa nyota wa timu. Alifunga mabao mazuri, aliwasaidia kutwaa kombe la Carabao ambalo hawakunyakua kwa miaka mingi. Newcastle United iliandika rekodi yake mpya baada ya kusotea taji lolote katika soka England.
Kwa mchezaji mwenye malengo ya mbali na alichokifanya msimu uliopita bila shaka yoyote Newcastle United si sehemu sahihi kwake tena. Kama alicheza na kutambulisha uwezo wake kupitia Newcastle United basi ni wakati wa kuona anasoga mbele.
Sababu za nyota huyo kuondoka
Taji la Ligi Kuu England; Newcastle United hawawezi kupigania taji la Ligi Kuu England. Msimu uliopita hawakuwa kwenye mbio za ubingwa. Kama timu haipo kwenye mbio za ubingwa na ina mchezaji kama Alexander Isak, bila shaka yoyote atalazimika kuondoka.
Ushindani uliopo kwenye EPL unamfanya aamini kuwa Newcastle haiwezi kumtimizia mahitaji yake mbali ya kumlipa mshahara mnono. Suala la ubingwa wa Ligi Kuu England ni muhimu na ambalo linatumika kama njia ya kulazimisha kuhama. Newcastle United hawaonekani kuwa katika mbio za kutwaa taji la EPL. Liverpool ambayo inatajwa kumfukuzia nyota huyo, ikiwa chini ya kocha mpya na asiye na uzoefu wa Ligi Kuu England, Arne Slot alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England mbele ya kocha mwenye uzoefu Eddie Howe wa Newcastle United.
Unaweza kumtetea Eddite Howe kuwa hana kikosi imara, lakini huwezi kumtetea kwenye suala la bajeti ya usajili kutoka kwa wamiliki. Suala ambalo linawafanya wasipate wachezaji hata wale wa daraja la kati ni kwa sababu timu yao haina ushawiswhi kwenye soka. Imebaki kuwa timu yaq kukamia wapinzani wa EPL kwa mechi moja moija tu basi. Kama Arne Slot angekuwa na mshambuliaji Alexander Isak basi nyota huyo bila shaka angekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu England. Isivyo bahati anachezea timu ambayo haiwezi hata kumpigia mabao 30 kwa msimu ikiwa uwezo huo anao. Suluhisho ni kuhama.
Ligi ya Mabingwa Ulaya: hili ni ndoto ya kila mchezaji kunyakua taji la Ulaya. Isak kama mchezaji mwenye ubora wa hali ya juu anatakiwa kuangalia malisho mapya na dhahiri Newcastle United hawawezi kufurukuta kwenye mashindano ya Ulaya au walau kujaribu kuchukua ubingwa huo.
Liverpool wanao mwelekeo chini ya Arne Slot. Nafais ya Isak kupangwa kikosi cha kwanza ipo kwa sababu majogoo hao wanahitaji mshambuliaji mwenye uwezo wa kuwapatia mabao angalau 40 kwa msimu. Kiufundi Liverpool na Newcastle ni timu tofauti. Liverpool wanafukuzia ubingwa, wakati Newcastle United wanahangaika kuhakikisha wanajaribu kumaliza nafasi nne za juu. hakuna mchezaji mkubwa ambaye anaweza kuvumilia na kubaki kwenye timu ambayo inafikiria kupigania nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi badala ya kufukuzia makombe.
Nafasi nne za juu; Newcastle united inakuwa kwenye mpambano na Liverpool, Chelsea, Arsenal, Man City kutafuta nafasi nne za juu. Newcastle United haiwezi kuvishinda vilabu hivi kwenye ushindani wa nafasi nne za juu. kwa maana hiyo bingwa wa Ligi Kuu anatoka kati ya timu zilizotajwa hapo juu lakini haiwezi kuwa Newcastle United, kwani haina ubavu wa kufua dafu mbele ya vinara hao. Njia pekee ya Newcastle United kucheza Ligi ya Mabingwa ni kuhakikisha wanakuwa sehemu ya taji la Europa League. Kama hawezi kupata mafanikio hata kwenye Europa League, basi hiyo si timu ya kuwa na mchezaji kama Alexander Isak.
Tuzo; katika suala la kushindana kuwania tuzo, Alexander Isa kana kila sababu ya kutaka kuwahama Newcastle kwa sababu timu hiyo haiwezi kumletea tuzo yoyote. Mchezaji anashiriki kwenye mashiandano ilia pate tuzo kwahiyo njia ya uhakika ni kuhakikisha achezea timu inayoweza kumpa anachotaka na yeye ataipa timu inachotaka. Msimu uliopita Isak aliwapa taji Newcastle United ikiwa na maana amaewapa walichotaka kwake, lakini wao hawawezi kumpa anachotaka. Suluhisho ni kuhama.


Comments
Loading…