Nahodha wa timu ya taifa ya England ya wanawake, Casey Stoney amebainisha jinsia yake kwa mara ya kwanza, akisema ni msagaji.
Stoney (31) anasema kwamba ameamua kuwa mkweli kwa sababu hakujihisi vyema kwa kuishi uongo muda wote huu.
Mwanamama huyo anasema kwamba amevutwa zaidi kusema ukweli kutokana na mpiga mbizi Tom Daley kutokezea na kusema kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume.
Casey alisema kwamba hakupenda kuficha jinsi yake katika wigo wa soka kwa sababu inaruhusiwa lakini ni vigumu kwa ulimwengu wa nje ya soka.
Huyo pia ni mlinzi katika timu ya wanawake ya Arsenal na alisema alihisi ni muhimu kuweka wazi hali yake kwani kuna watu wengi wapo katika hali ngumu kiasi cha kujiua kwa sababu ya hali zao kimapenzi.
“Je, nawezaje kutarajia watu wengine kuzungumza kuhusu hali zao wakati mie mwenyewe sipendi kujizungumzia?” alihoji mwanamama huyo aliyechezea England mechi 116 na pia alikuwa nahodha wa Uingereza kwenye michezo ya Olimpiki jijini London hivi karibuni.
Casey amewahi pia kuzichezea klabu za Charlton, Chelsea na Lincoln na alishafikiria kustaafu mechi za kimataifa baada ya kushindwa kucheza kwenye Euro 2005 kwa England.
Anasema kwamba kwa miaka 10 ya kwanza alikuwa anaogopa sana juu ya kile ambacho watu walikuwa wakifikiria na jinsi wangemuona lakini sasa ameamua kuwa mkweli hata kama atadhihakiwa kupitia vyombo vya habari.
“Lakini sasa nadhani nipo sehemu ambayo sina wasiwasi, napendwa na kila mtu hivyo naona ni vyema kusema ukweli wangu,” alikiri mwanamama huyo.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameonya kwa muda mrefu dhidi ya wasagaji na mashoga kwenye michezo iliyoandaliwa nchini mwake.
Baada ya kubanwa sana, alisema kwamba watu hao wanaweza kwenda lakini hawaruhusiwi kuwasogelea watoto, akiogopa wasiwatie najisi.
Comments
Loading…