in , ,

MKUDE , BENCHI LINAMUONDOLEA KILA KITU

Nilikuwa naangalia mechi ya Dodoma Fc dhidi ya Simba jana iliyochezwa
katika uwanja wa Jamhuri.

Mechi hii ilikuwa mechi ya kirafiki katikati ya msimu , ambapo Simba
iliamua kutumia baadhi ya wachezaji wake ambao huwa hawapati nafasi
katika mechi za mashindano.

Kuwatumia hawa wachezaji ilikuwa wazo zuri kwa sababu inawapa nafasi
kwao kucheza tena ili kuongeza kujiamini na kumuonesha kocha kuwa
wanaouwezo wa kufanya vizuri.

Mechi iliwapa nafasi kina Mseja, Mohamedi Ibrahim, Ndemla na wengine
wengi. Lakini moja ya watu ambao walipewa nafasi ile ni aliyewahi kuwa
nahodha wa Simba msimu uliopita Jonas Mkude.

Ilikuwa ndiyo mechi yake ya kwanza msimu huu, hakuwahi kucheza mechi
yoyote ya kimashindano au zile mechi za Pre- season ( mechi za
kujiandaa na msimu mpya).

Hivo ndiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza kuvaa uzi mpya wa Simba
uwanjani tangu msimu huu mpya uanze.

Kwangu mimi sikuwa nategemea kiwango kikubwa kwa Jonas Mkude kwa
sababu ndiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza msimu huu.

Nilichokuwa nategemea ndicho kilichokuja kutokea, hakuonesha kiwango
kikubwa katika mechi ya jana.

Hii ni kwa sababu ya vitu mbalimbali ambavyo Mkude amekuwa akipitia
mara kwa mara tangia msimu huu uanze.

Msimu uliopita Mkude alikuwa nahodha wa timu ya Simba. Yeye ndiye
alikuwa kiongozi wa jahazi hili.

Kabla ya msimu kuanza alipokonywa kitambaa na kupewa mtu mwingine.

Haya ni maamuzi ya kawaida tu kwenye timu lakini inavyoonesha hakuna
maandalizi yoyote yaliyofanywa ili kumtolea kitambaa Mkude na kumpa
mtu mwingine.

Mkude hakuandaliwa kisaikolojia na viongozi wa timu, benchi la ufundi
ili aone hiki ni cha kawaida kwake . Mwisho wa siku kimemfanya
kumuathiri yeye kwenye kiwango chake.

Anacheza anaonekana kama mtu ambaye haiitajiki kwenye timu na hana
thamani yoyote kwenye timu.

Hili limekuja kuchanganywa na yeye kutokupata hata nafasi ndogo ya
kucheza katika timu ya Simba.

Hali hii imekuja kumuua kabisa, mara nyingi amekuwa mtu wa kukalia
mbao na wakati mwingine amekuwa akikaa jukwaani.

Hii imeongeza upweke ndani yake. Hali ambayo inamfanya kukosa
kujiamini ndani yake.

Hali ya kupigania timu pamoja na kupigania kiwango chake haipo tena.

Haoni faida ya yeye kupigana tena kwa sababu kichwani kwake anajiona
hana thamani tena kwenye timu ya Simba.

Hii ni tofauti na kwa wachezaji kama kina Ndemla, Mohamed Ibrahimu
ambao huwa hawapati nafasi mara kwa mara lakini huwa wanajitahidi sana
kupigania nafasi zao.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Jürgen Klopp: KUNA HAJA YA KUZUNGUMZA NA NAFSI

Tanzania Sports

Issues with Tanzanian football: Interview with Paul Mitchell, Siyavuma Sports Group