in

Michezo kurejea bado

Maandalizi ya EPL

Waliokuwa wakitarajia msimu wa soka wa 2019/2020 ungerejea mapema wamekosea, kwani serikali imesema bado haijalegeza masharti iliyoweka kusitisha michezo na mikusanyiko mingine kutokana na virusi vya Corona.

Palikuwapo matarajio kwamba wiki hii serikali ingetangaza kulegezwa kwa masharti yaliyosababisha kusitishwa kwa zaidi ya mechi 90 zilizobaki za Ligi Kuu ya England (EPL) na ligi nyingine nchini Uingereza.

EPL imebaki katika sintofahamu, kwani haijulikani hatua gani zitachukuliwa ikiwa Covid-19 itaendelea kutikisa kwa muda mrefu. Wakati Liverpool wamekuwa kwenye nafasi murua ya kutwaa ubingwa, nafasi za kushuka daraja na za kufuzu kwa mashindano ya Ulaya zipo kwa timu nyingi.

Idara ya Dijiti, Utamaduni, Vyombo vya Habari na Michezo pamoja na ile inayohusika na afya zimeonesha kwamba hakuna uwezekano wa kuanza haraka kwa michezo tena nchini, wasemaji wao wakijulisha kwamba hatua yoyote kuchukuliwa kwenye mwelekeo huo inaweza kutangazwa katika muda wa zaidi ya wiki moja toka sasa.

Mipango yoyote ya kulegeza masharti kwa michezo kama ya soka kwenye EPL, mbio za farasi, kriketi na rugby haziwezi kuchukuliwa hadi hapo serikali itakapotangaza mpango wake mpana Mei 7.

Siku hiyo kutakuwapo mkutano wa wadau, ambapo makundi mawili tofauti yaliyokuwa yakifanya utafiti yatawasilisha mapendekezo ya juu ya jinsi gani michezo irejewe, kanuni mpya za kufuata na iwapo itakuwa bila watazamaji au kwamba itasogezwa mbele ili janga limalizike na washabiki waingie uwanjani.

Uingereza imebaki kimya wakati Ligi Kuu ya Ujerumani – Bundesliga ikitarajiwa kuanza Mei 9 baada ya taifa hilo kubwa kiuchumi kuonesha ufanisi wa aina yake katika kukabiliana na virusi hivyo vinavyosababisha homa kali ya mapafu.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa kutoendelea kwa ligi hiyo, baada ya Kansela Angela Merkel kudokeza kwamba masharti makali zaidi yatawekwa kutokana na hisia kwamba kuanza kwa mikusanyiko kunaweza kusababisha kulipuka upya kwa virusi hao waliokwishadhibitiwa. Hata hivyo, baadhi ya magavana wa majimbo walionesha utayari wao wa kurejea tena kwenye Bundesliga, hata kama ni bila watazamaji.

Katika tukio jingine, Mganga Mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Tim Meyer, amesema kwamba upo uwezekano wa wazi kuanza kupanga namna ya kuanza tena kwa msimu wa 2019/2020, licha ya Ligi Kuu ya Ufaransa – Legue 1 kuwa ya pili kufuta msimu baada ya ile ya Uholanzi – Eredivisie.

Akizungumza siku moja baada ya Mganga Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Michel D’Hooghe kuonya kwamba haingewezekana kucheza soka kabla ya amri za kukaa mbalimbali hazijaondolea na kwamba kama kuanza tena soka labda iwe Septemba – Meyer alisema ana matumaini soka itaanza mapema zaidi.

“Vyama vyote vya soka vinavyopanga kuanza tena kwa msimu wa mashindano vitatakiwa kwanza kutoa protokali pana, ili kuhakikisha kwamba afya za wale watakaohusishwa na mechi hizo zinalindwa. Chini ya hali hizi, ni wazi kwamba inawezekana kuanza kuwekwamipango ya kurejea uwanjani ili kumaliza msimu wa 2019/2020,” akasema

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Maandalizi ya mchezo wa soka

Nyambui: Politics and Sport do not mix

Tanzania Sports

EPL viwanja huru