Msimu wa Chelsea unaelekea ukingoni. Kwanza wanatakiwa kupindua meza dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa.
Mchezo wa mwisho utachezwa Allianz Arena ifikapo Agosti 8 mwaka huu. Uwanja wa Allianz Arena ndio uliompa furaha Frank Lampard. Ni mahali alipotwaa taji la UEFA. Lakini safari hii habari ni tofauti, si mahali pa furaha kwa Lampard akiwa nyuma kwa mabao 3-0 baada ya mchezo wa kwanza.
Lampard bila shaka amepata somo atakalotumia kutumia kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yake. Somo hilo lipo katika maeneo mawili; sokoni katika manunuzi ya wachezaji na mbinu za ufundishaji uwanjani. Lakini anaweza kubadilika kati ya sasa na baadaye.
Kuna mechi 3 ndani ya siku 7 zijazo, na huenda akacheza mechi ya nne pia. Mechi hizo ndizo zitatoa majibu ya msimu wa Chelsea ulivyokuwa. Wanaweza kutwaa Kombe la FA au kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Naye Ole Gunnar Solskjaer anakabiliwa na mtihani huo huo kwenye kikosi chake cha Man United. Kikosi chake kimekutana na Chelsea kwenye nusu fainali ya FA. Kilichotokea kwenye mchezo huo kitamsaidia kutupia jicho kwenye mashindano ya ulaya akiwa na ari mpya ya kazi kuliko ya kubwaga manyanga ya kuinoa timu hiyo.
Kwenye Europa League, mchezo wa kwanza alishinda mabao 5-0 dhidi ya LASK hivyo kuzisubiri Basaksehir au FC Copenhagen ambazo zitachuana katika robo fainali. Mashindano hayo yanampa nafasi ya kuboresha kikosi chake, hukuwa akiwa kocha ambaye anajifunza mengi katika kazi yake.
Lampard na Solskjaer hawajaambiwa ni lazima kutwaa makombe msimu huu. Hakuna aliyesema kuwa Chelsea au Man United zitafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini mazingira yao ya kazi katika klabu kubwa yanataka kuona vikombe vikiwasili msimu huu.
Ukizingatia hicho ni kitu cha kwanza kujadiliwa na kuhukumiwa. Mipango ya Man United ilikuwa angalau kushinda taji la FA au kufuzu Ligi ya Mabingwa iwe kwa njia ya kawaida ya msimamo wa Ligi au kupitia taji la Europa League.
Kwa sababu kama wangetwaa Europa League maana yake wangeshiriki Ligi ya Mabingwa moja kwa moja. Louis van Gaal na Jose Mourinho walishinda mataji wakiwa Man United, ni kama alivyofanya Maurizio Sarri kwa Chelsea. Makocha wote wawili Lampard na Solskjaer, na pamoja na Mikel Arteta wa Arsenal wamepewa timu hizo kwa sababu wameaminiwa katika ubora wao wa mbinu za mchezo vichwani mwao.
Msimu huu wa kwanza kwa Pep Guardiola ulimalizika akiwa mtupu bila taji Manchester City kabla ya kuibuka mbabe wa Ligi England. Naye Jurgen Klopp alimaliza misimu mitatu akiwa Liverpool bila kutwaa taji, kabla ya kuibuka bingwa wa Ulaya mara katika kipindi cha miaka mine na Ligi Kuu England ndani ya miaka mitano.
Lakini Chelsea na Manchester United ni klabu zenye fedha nyingi na uwekezaji mkubwa umefanyika kutokana na matakwa na makocha hao.
Kwa mfano, pale Chelsea chini ya umiliki wa bilionea Roman Abramovich, kumekuwa hakuna uvumilivu kwa fedha za wanazowekeza klabuni. Wamekuwa wakifukuza makocha mara kwa mara.
Pana tofauti ya mbinu za Guardiola na Klopp, vivyo hivyo kwa Lampard na Solskjaer. Inashangaza kuona timu kubwa barani Ulaya kama Chelsea, Man United na Arsenal, zikiwa chini ya makocha wadogo na wenye uzoefu mdogo wa ukocha.
Inawezekana wamiliki wa timu hizo wanavutiwa na mafanikio ya Guardiola alipokabidhiwa Barcelona mwaka 2008.
Lazima tukiri kuwa Guardiola ni kocha mwenye upekee. Hata Zinedine Zidane ambaye amewahi kujiuzulu vipindi viwili, ni mchezaji aliyegeuka kuwa kocha wa Real Madrid.
Kwahiyo, Chelsea na Man United nazo zimeajiri makocha waliowahi kuwa wachezaji klabuni mwao ili kujaribu mtindo uliofanywa na Barcelona na Real Madrid badala ya kuajiri kocha mwenye jina kubwa barani Ulaya.
Sarri alifanikiwa malengo mawili akiwa Chelsea msimu uliopita; kwanza kumaliza katika nafasi nne za juu za Ligi na pili; kutwaa taji la Europa, lakini mabosi wake walikuwa tayari kumpa nafasi ya kuendelea kukinoa kikosi chao kabla ya kuamua kwenda Juventus.
Mashabiki walikuwa na hisia kuwa mafanikio hayo yalikuwa sawa na yale ya Carlo Ancelotti, Roberto Di Matteo, Rafael Benitez, Jose Mourinho, Antonio Conte.
Sasa Chelsea wanaonekana kuachana na kuajiri makocha wenye majina makubwa barani Ulaya, wanatumia mbinu nyingine kutafuta mafanikio.
Kuajiri kocha aliyecheza klabuni hapo hata kama hana uzoefu mkubwa. Pia kutegemea vipaji vinavyoibuliwa katika akademi yao kuliko kumwaga fedha kusajili mastaa wakubwa.
Kikosi cha Chelsea katika mchezo wa fainali ya Europa League msimu uliopita kilikuwa na wastani wa umri wa miaka 28. Wachezaji wenye miaka juu ya 30 walikuwa watatu; Olivier Giroud, David Luiz na Pedro) na mmoja Andreas Christensen alikuwa na miaka 23.
Chini ya Lampard, msisitizo umekuwa kuwaendeleza vipaji vya chipukizi. Msimu uliopita wachezaji waliokulia akademi ya Chelsea walicheza mechi 16 tu; Christensen (6), Ruben Loftus-Cheek(6), Callum Hudson-Odoi (4).
Msimu huu idadi imeongezea; Mason Mount (30), Tammy Abraham(25), Christensen(21), Fikayo Tomori (15), Reece James(14),Hudson-Odoi(7), Billy Gilmour (2), Loftus-Cheek(2) ambao wastani wa umri wao ni miaka 25. Je, ni timu gani imepanga kikosi chipukizi mfululizo katika Ligi Kuu msimu huu? Jibu ni Man United.
Wakati mwingine Chelsea imeonekana ikiwa laini mno. Kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Sheffield United wikiendi iliyopita kilisababisha Lampard akiajipize kuwa hatosahau mechi hiyo.
Uamuzi wa kuwaweka benchi Christensen, James, Mount na Abraham katika ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Norwich City ulizungumza mengi. Lakini sehemu kubwa ya tatizo lao ni nguvu hafifu,kushindwa kukabili presha. Ikiwa bodi ya Chelsea itakosa uvumilivu au uongozi wanaweza kuachana na chipukizi wao.
Conte alikumbana na hali hiyo lakini aliwanyamazisha mabosi wake kwa kutwa taji la Ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza.
Msimu wa pili 2017-18 ukawa majanga, walifungwa mabao 3-0 nyumbani kwa Bournemouth (yite yakifungwa ndani ya dakika 16), kisha wakazabwa mabao 4-1 nyumbani kwa Watford(mabao matatu yalifungwa katika dakika sita za mwisho)
Chini Sarri mwaka mmoja baadaye walifungwa 4-0 kwa Bournemouth (yote yakifungwa kipindi cha pili) na wakazabwa mabao 6-0 nyumbani kwa Manchester City.
Vipigo hivyo vilipotokea viliwapa somo katika vikosi vyao chini ya makocha wenye uzoefu mkubwa wa kandanda ndani ya siku 12 tu. Hapo ndipo Chelsea ikageukia pia kikosi chake cha kwanza kuona namna ya kukikarabati. Eden Hazard akauzwa kwenda Real Madrid msimu uliopita. Chelsea waliamua kufumua kikosi chao na kufanya marekebisho ili kubadili hali ya viwanjani mwao.
Siku ya utambulisho wake Julai mwaka hana, Lampard alijaribu kuongea kwa lugha rahisi kwamba wachezaji wa akademi wanatakiwa kuvuka barabara kujiunga kikosi cha kwanza.
Huo ukawa mwanzo wakuibuka kwa Mount, Abraham, Tomori, James na Gilmour. Ingawa wengi wanadhani kuwapandisha makinda hao kulilazimishwa na Lampard, lakini ukweli mwingine ni adhabu ya FIFA iliathiri mambo mengi ikiwemo kuacha kuwapeleka kwa mkopo vijana hao. Kwahiyo Chelsea walihitaji mbinu hiyo ili kukabiliana na hali halisi kwa vile hawakuruhusiwa kusajili.
Man United nayo ilimhitaji kocha kama Solskjaer kufanya kile anachokifanya sasa kuinua vijana kuwafikisha katika kiwango cha juu kikosi cha kwanza. Mpango huo Ed Woodward anauita “kuinua utamaduni wa Man United”.
Woodward kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akihangaika kutengeneza kile anachokiita „DNA‟ ya Man United, ambapo sasa namna chipukizi walivyojazana na kupewa nafasi kikosini ni wazi anaelekea kuibuka mshindi. Kwamba mpango umelipa vizuri.
Solskjaer anafanya kile ambacho Woodward anakipenda. Mwezi Machi mwkaa jana wengi walidhani ni makosa kwa Man United kumwajiri Solskjaer kwa mkataba wa kudumu baada ya kushinda mechi 14 kati 19 akiwa kaimu kocha mkuu.
Baada ya kupitia vipindi vigumu inaonekana sasa Solskjaer amepata ufumbuzi. Man United imecheza mechi 19 bila kufungwa katika mashindano yote. Ameshinda mechi 8, ametoka sare mechi 4 kati ya 12 za Ligi Kuu.
Wanaonekana sasa kuimarika na kuonesha wao ni Man United kuliko walivyokuwa chini ya Van Gaal au Mourinho. Hata matokeo yao ni mazuri. Wamemwongeza Bruno Fernandes, huku Mason Greenwood akiibuka kuwa gumzo kwa kiwango chake. Antony Martial anaanza kutoa matunda ya kiwango bora mfululizo.
Unaweza kusema haikuwa sawa Man United kumchukua Ole ambaye alikuwa kocha huko Norway. Pia unaweza kusema haikuwa sawa kwa Chelsea kumchukua kocha ambaye alikuwa amekosa nafasiya kupandisha timu yake Ligi Kuu. Sababu kubwa ingekuwa ni sifa za timu hizo kuwa kubwa kuliko makocha.
Ukiachana na sifa zao walipokuwa wachezaji katika klabu za Man United na Chelsea, Solskjaer na Lampard wasingeajiriwa kuzinoa timu hizo kwa vigezo vya mafanikio yao ya katika klabu za Molde na Derby County. Lakini hiyo si hoja tena. Wao wameajiriwa kurejesha umoja katika timu. Lakini wakati jukumu la kwanza la klabu ni kubadili utamaduni, kulinda thamani, hayo yanaeleweka umuhimu wake.
Mshikamano na mashabiki unatakiwa wa manufaa hasa pale safari ya mafanikio inapokuwa ndefu pamoja na maamuzi magumu.
Pengine bila kocha Solskjaer nafasi ya wakongwe wa klabu hiyo ingekuwa ngumu zaidi hasa nyakati za matokeo mabaya kati ya Machi 2019 na January 2020. Imemchukua mwaka kurekebisha mambo baada ya kumalizika jinamizi la Mourinho.
Kumsajili Fernandes kutoka Sporting Lisbon mwezi januari ulikuwa uamuzi mzuri, lakini Solskjaer atangaliwa nafasi aliyopewa na benchi lake la ufundi kuweka mambo sawa nyuma ya pazia.
Solskjaer amefanikiwa kubadili ya Carrington kwa muda mfupi tangu alipochukua mikoba ya Mourinho. Alifanikiwa kuzungumza na wachezaji kwa uwazi,imara na wenye kuona mbali.
“Wachezaji hawa walikuwa wanaanza na mtazamo hasi, lakini sasa wana mitazamo chanya,” alisema siku hivi karibuni na kuongeza, “najisikia mmoja wa wachezaji, hatuna mtu mbaya katika kikosi chetu,”
Katika msimamo wa Ligi Man United wapo nyuma ya Liverpool kwa pointi 31, ambapo wamepata pointi chache sana. Rekodi ya kupata pointi ni 66 msimu uliopita, chini ya Van Gaal mwaka 2016 walipata pointi 66 na chini ya David Moyes walipata pointi 64 katika msimu wa 2013-14
Hadi sasa msimu huu wamepata pointi 62, wameshinda mechi 36. Hakuna atakayejali kama ni 64 au 66 au kupata pointi za kufuzu Ligi ya Mabingwa. Lakini tuwe wakweli, msimu ujao Man United inatakiwa kupigania ubingwa wa Ligi Kuu.
Naye Lampard, akabailiwa na kibarua kigumu kama cha Ole. Huenda anatakiwa kujipanga zaidi kabla ya kazi hiyo hajapewa kocha mwingine. Solskjaer akimaliza nafasi nne za juu itamwongezea ari. Angalau nusu ya pili ya msimu huu tumeona Man United inayojaribu kiufanya mambo makubwa. Lakini anatakiwa kufanya tathmini aina ya wachezaji anaowataka. Jason Sancho wa Borussia Dortmund amekuw awa kwanza kati ya wanaowindwa na Ole.
Pamoja na hali nzuri, lakini wanaweza kushangaa wanatawaliwa na Guardiola na Klopp na kuzishuhudia Manchester City na Liverpool zikichuana zenyewe.
Zipo hisia pia Frank Lampard anapitia mazingira ya Ole, ingawa mmiliki wa Chelsea bado hajaweka imani kwake kwa asilimia 100. Ndani ya viunga vya Satmford Bridge wanaongelea umoja na uthubutu wa timu. Wana hali ya umoja kuliko vipindi vya Mourinho,Conte na Sarri.
Habari kubwa nzuri kwa Chelsea si usajili wa Timo Werner na Hakim Ziyech lakini kusaidia kuboresa mipango ya kuibua vipaji.
Wote wawili wametumia mchezo wa FA kama njia ya kuibua ari na mipango ya kuleta mafanikio katika vikosi vyao. Je nini kitatokea baada ya mechi ya nusu fainali FA? Je, wataweza kuizuia Leicester City wasifuzu Ligi ya Mabingwa katika mechi tatu zijazo?
Comments
Loading…