in , ,

MCHUJO MWANASOKA BORA:

 

Ni Ronaldo Messi au Neymar

Wachezaji watatu wanaokipiga soka ya Hispania, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Lionel Messi na Neymar wa Barcelona wamevuka mchujo wa kutafuta mwanasoka bora wa dunia.

Ni mmoja kati yao atakayepata tuzo ya Ballon d’Or – ambapo mshindi atatangazwa jijini Zurich, yaliko makao makuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Januari 11 mwaka huu.

Tuzo hiyo kwa miaka miwili iliyopita imekuwa inashikiliwa na Ronaldo, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno. Messi ni wa Argentina wakati Neymar ni wa kimataifa wa Brazil. Watatu hao wamechaguliwa huku wengine 20 wakitupwa nje akiwamo mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale.

Makocha wanaowania tuzo bora ya ukocha ni Luis Enrique wa Barcelona, Pep Guardiola wa Bayern Munich na Jorge Sampaoli anayefundisha timu ya taifa ya Chile iliyotwaa ubingwa wa Copa America mwaka huu.

Orodha kamili ya wachezaji, nchi na timu wanazochezea na walizokuwa msimu uliopita waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Sergio Aguero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale (Wales/Real Madrid), Karim Benzema (Ufaransa/Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid) na Kevin De Bruyne (Ubelgiji/VfL Wolfsburg/Manchester City).

Wengine ni Eden Hazard (Ubelgiji/Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain), Andres Iniesta (Hispania/ Barcelona), Toni Kroos (Ujerumaniy/Real Madrid), Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich) na Javier Mascherano (Argentina/ Barcelona).

Walikuwamo pia Lionel Messi (Argentina/ Barcelona), Thomas Muller (Ujerumani/ Bayern Munich), Manuel Neuer (Ujerumani/ Bayern Munich), Neymar (Brazil/ Barcelona), Paul Pogba (Ufaransa/Juventus) na Ivan Rakitic (Croatia/ Barcelona).

Mkongwe Arjen Robben (Uholanzi/Bayern Munich) amerudi na pia walikuwamo James Rodriguez (Colombia/Real Madrid), Alexis Sanchez (Chile/Arsenal), Luis Suarez (Uruguay/ Barcelona), Yaya Toure (Côte d’Ivoire/Manchester City) na Arturo Vidal (Chile/Juventus/ Bayern Munich).

Orodha kamili, uraia na timu wanazofundisha ni Massimiliano Allegri (Italia/Juventus), Carlo Ancelotti (Italia/Real Madrid), Laurent Blanc (Ufaransa/Paris Saint-Germain), Unai Emery (Hispania/Sevilla), Pep Guardiola (Hispania/FC Bayern Munich), Luis Enrique (Hispania/FC Barcelona), Jose Mourinho (Ureno/Chelsea), Jorge Sampaoli (Argentina/Timu ya Taifa ya Chile), Diego Simeone (Argentina/Atletico Madrid), Arsene Wenger (Ufaransa/Arsenal).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsenal wanasota

Tanzania Sports

Garry Neville kocha Valencia