in , ,

MATARAJIO YETU WATANZANIA OLIMPIKI YA RIO 2016

Lack of sports investment in Tanzania

Mashindano ya Olimpiki yanaanza rasmi kesho Ijumaa tarehe 5 Agosti, mjini Rio De Janeiro. Akizungumza na Sky TV- juzi Jumatano mkuu wa Michezo ya Olimpiki Uingereza Bw. Sebastian Coe alimtakia kheri mwenzie wa Brazil, Carlos Nuzman ambaye anapitia kipindi kigumu sana.

Kati ya viunzi watayarishaji wa Brazil walivyopitia ni maradhi ya homa ya Zika, serikali yenye matatizo ya kisiasa na makampuni ya ujenzi ambayo hayakufanya kazi zake vyema kumalizia kambi mbalimbali.

Kwa miezi kadhaa Zika imekuwa habari kuu na wanawake wamekuwa na wasiwasi hasa wale wanaotaka kuzaa. Virusi vya Zika hukaa mwilini bila kuonekana kwa miezi sita. Kwa wanawake husababisha watoto kuzaliwa na vichwa na ubongo mdogo ambao ni kilema.

Kwa Watanzania ingawa Mkuu wetu wa Olimpiki, Bwana Filbert Bayi aliwahakikishia wachezaji wetu kuwa hakuna haja ya wasiwasi , imeulizwa vipi wenzetu wanachanjwa kabla ya kwenda Rio? Timu za wanawake wachezaji tenisi nchi nyingine zimefanyiwa chanja ya kukinga Zika.

Tatizo jingine lililoparamia habari ni matumizi ya dawa za kumwezesha mchezaji kufanya vizuri zaidi. Tatizo hili la “doping” liliwakumba wanamichezo wa Kirusi na mwezi jana ilikuwa karibu wafutwe kabisa katika Olimpiki lakini bahati yao wakapita kutokana na mhusika mkuu kufahamiana na Rais Vladimir Putin.

Kwa Watanzania hakuna tatizo hili, ila wenzetu wa Kenya walikumbwa na msuko suko huu .
Utata wa tatu ni kambi mbalimbali za washiriki kuchelewa ujenzi. Kutokana na kutomalizika kazi hizo wachezaji wengi walilalamika lakini Wabrazili wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha shughuli inamalizika. Hata hivyo mambo mengine yamevuka mpaka. Sehemu ya mashindano ya ngalawa kwa mfano katika ghuba ya Guanabara, jijini Rio ilisemekana kuwa chafu, na maiti ya mtu asiyejulikana ilionekana ikielea.

Kimichezo bara Afrika linaongozwa na Afrika Kusini, Kenya na Ethiopia. Mchezo mpya michuano hii ya 31- ni mpira wa meza ambapo Nigeria na Senegal zimepeleka wachezaji wengi , huku Kenya na Afrika Kusini wakiwa na timu ya Rugby. Kama kawaida Kenya na Ethiopia inao wanariadha wengi.

Kidunia, nchi zinazoongoza kwa wachezaji wengi ni Marekani (550), Brazili, (450) na China (380). Linganisha kiasi hicho na washiriki saba tu kutoka Tanzania.

Akizungumza na Watanzania kabla ya kuondoka , Naibu Waziri wa Michezo, Habari na Utamaduni, Mheshimiwa, Anastazia Wambura aliwasihi waiwakilishe Tanzania kwa kuitangaza kiutalii mbali na kujitahidi kutwaa medali.
Akitoa nasaba hiyo hiyo, Mkurugenzi wa kampuni ya Multichoice iliyo kati ya wadhamini wa timu yetu, Bw Mohammed Chande aliishukuru serikali kwa fursa ya kuthamini michezo.Multi choice inadhamini safari.

Naye Filbert Bayi alionesha matumaini kwa timu ya mwaka huu kwa kusisitiza matayarisho yamekuwa bora na tofauti. Mathalan, mwogeleaje Magdalena Mosha aliyeshiriki Olimpiki ya Biejing (2008) na London (2012), amekuwa akifanya mazoezi Australia juu ya uzoefu huo.

Mosha anaongozana na mwogeleaji mwingine anayekwenda Olimpiki kwa mara ya kwanza, Hilal Hilal. Wengine ni Andrew Tomas Mulugu (Judo), mkimbiaji pekee wa kike wa Marathon, Sara Ramadhan. Na pia wanariadha wa miaka mingi, Fabian Joseph, Said Juma Makula na Alphonce Felix Simbu.
Kama kweli tumejifunza kufanya matayarisho vizuri kinyume na miaka ya nyuma basi tutegemee vimulimuli na medali kama viongozi walivyowataka vijana na mashujaa wetu hawa saba.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Ureno wababe Ulaya

Mashindano ya Olimpiki yanatuumbua watanzania