in , , ,

Manchester United haina njia MBADALA!

Wakati natazama mechi kati ya Manchester United na Liverpool, kuna picha moja ilikuja katika akili yangu. Picha ya mechi kati ya Manchester United na PSG.

Mechi ambayo ilichezwa pale Old Trafford, mechi ambayo ilichezwa kipindi ambacho Manchester United ilikuwa kwenye kiwango bora.

Mechi kumi na moja mfululizo walikuwa wameenda bila kufungwa kwenye michuano yote ambayo Manchester United ilikuwa inashiriki.

Kwa hiyo watu wengi walikuwa wanaipa nafasi kubwa sana ya Manchester United kufanya vizuri kutokana na sababu mbalimbali kwa wakati huo.

Ukiachana na kuwa Manchester United ilikuwa imeenda mechi 11 bila kufungwa, PSG iliingia uwanjani ikiwa na wachezaji wao nyota wawili.

Edson Cavanni pamoja Neymar. Kutokuwepo kwa hawa wachezaji wawili lilikuwa pigo kubwa sana kwa PSG kwenye mechi hii.

Na hii ni kwa sababu hawa wachezaji wawili kwa asilimia kubwa huwa ni ufunguo wa ushindi kwa PSG kwa mismu kadhaa.

PSG hii ambayo ilikuwa inaenda uwanja wa nyumbani wa Manchester United uwanja ambao ulianza kuonekana machinjioni.

Asilimia kubwa ya mechi hii ilitazamika kwa Manchester United kushinda mechi hii. Lakini matokeo yalikuwa tofauti kabisa na matazamio ya wengi.

Manchester United alipoteza mechi hii, na mwanzo wa kupoteza mechi hii ulianza baada ya Antony Martial kuumia pamoja na Jesse Lingard.

Walipoumia wachezaji ambao walitakiwa kuja kuziba nafasi zao hawakuweza kufanya kitu ambacho kingekuwa na msaada mkubwa.

PSG waliingia bila na Cavanni pamoja na Neymar lakini wachezaji waliokuwa wamepewa nafasi kwenye mechi ile waliisaidia PSG.

Pamoja na kwamba hawakucheza katika kiwango kikubwa cha kina Neymar na Cavanni lakini walikuwa na msaada mkubwa wa kuipa matokeo chanya PSG.

Hii yote unaweza ukaijumuisha na kuiweka katika sentensi moja tu, PSG walikuwa na mbadala sahihi kwenye timu kwa hawa wachezaji wawili.

Hiki ndicho kitu pekee na kikubwa ambacho unaweza ukakisema. Hata mahali pa Rabiot hapakuonekana kama kuna shida , kwa sababu tu walipata mbadala.

Wakati mechi inaendelea Martial na Lingard wakaumia, waliosimama kutoka benchini kuja uwanjani hawakuweza kuwa mbadala mzuri.

Mwisho wa siku Manchester United akapoteza ile mechi tena nyumbani na kuweka mazingira magumu katika mechi ya mkondo wa pili itakayochezwa PARIS.

Tuachane na hayo , turudi sasa kwenye mechi kati ya Manchester United na Liverpool. Hii ilichezwa pale pale ambapo PSG alifanikiwa kupata matokeo chanya.

Na katika mechi ile kulitokea kitu kile kile ambacho kilitokea kwenye mechi dhidi ya PSG, lakini safari hii kikitokea kwa wengine.

Hakuwa Martial na Lingard walioumia kwenye ile mechi, safari hii ilikuwa zamu ya kina Rashford kuumia. Na walipoumia ukawa mwanzo wa Manchester United kutokuwa na uwiano mzuri.

Kwa sababu watu ambao walikuja kuziba pengo la hao wachezaji walioumia hawakuweza kuwa na msaada mkubwa sana wa kubadilisha matokeo kwa kiasi kikubwa cha hali ya juu.

Hawakuwa mbadala sahihi wa wachezaji waliokuwa wameumia kwa kwenye mechi ile. Hii ni picha tosha kuwa kuna kitu kinakosekana.

Pamoja na kwamba Manchester United tangu aondoke Jose Mourinho imekuwa na matokeo chanya, lakini imekuwa inakoasa vitu vichache sana.

Moja ya vitu hivo ni timu kukosa mbadala sahihi katika nyakati ngumu. Hiki kitu kinaweza kutengenezwa na kocha kwa kuleta watu ambao wanaweza wakawa mbadala sahihi katika maeneo muhimu ndani ya timu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Kepa katuonesha SARRI hana SAUTI NZITO !

Tanzania Sports

Ronaldo ameondoka na mvuto wa El Clásico