in , , ,

Man U wawang’ang’ania Bayern

*Barcelona wabanwa na Atletico

Robo fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya za usiku wa Jumanne zilitawaliwa na sare za bao 1-1 jijini Manchester na Barcelona, ambapo Manchester United walicheza vyema tofauti na walivyotarajiwa dhidi ya Bayern Munich.

Kocha wao, David Moyes anasema anaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kuwang’oa Bayern kwenye mzunguko wa pili wiki ijayo nchini Ujerumani licha ya vijana hao wa Pep Guardiola kuwa na faida ya bao la ugenini.

Shujaa wa United alikuwa Nahodha Nemanja Vidic anayehama mwisho wa msimu huu kwani ndiye alifunga bao kwa kichwa dakika ya 58, lakini pia aliongoza vyema ngome yao na kufanikiwa kuwazuia Bayern wasiwaaibishe nyumbani.

Hata hivyo, Bayern waliosawazisha bao hilo dakika ya 66 kupitia kwa Basten Schweinsteiger walitawala mchezo kila idara kwa asilimia 74 wakiwaachia United 26, lakini Man U walipata nafasi zaidi za kufunga mbazo zilikoswa, mojawapo ikiwa ya Danny Wellbeck.

Schweinsteiger alikuja kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na rafu ambayo haikuwa na sababu dhidi ya Wayne Rooney aliyekuwa akianza kukokota mpira kutoka eneo la nyuma la United. Mjerumani huyo muhimu atakosa mechi ijayo, hivyo United wanaweza kuwekeza hapo.

Wenyeji walishangiliwa mfululizo na washabiki waliojazana kwenye Uwanja wa Old Trafford na imani ikaonekana kurudi, hata kama itakuwa kwa muda mfupi, kwa Kocha Moyes ambaye kwenye ligi kuu anafanya vibaya, timu yake ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi inayoelekea ukingoni.

BARCELONA WABANWA NYUMBANI

Neymar

Katika mechi nyingine kwenye Uwanja wa Camp Nou, wenyeji Barelona walielekea kulala baada ya kupigwa bao moja lililofungwa na wajina wa Diego Coasta, Diego katika dakika ya 56, lakini Neymar wa Barcelona akaja kusawazisha dakika ya 71.

Nyota wa Atletico anayewaniwa na timu za Ligi Kuu ya Uingereza, Costa aliumia na kutolewa nje kipindi cha kwanza, na kuwatia wasiwasi wageni kwamba wangelala mbele ya miamba hao wa dunia, lakini siku haikuwa ya Barca.

Bao la Diego lilikuwa zuri, ambalo alifunga akiwa umbali wa yadi 30 na lilirudishwa kwa jitihada za kiungo mzoefu, Andes Iniesta aliyempa pande Neymar.

Jumatano hii Chelsea watakuwa wageni wa Paris Saint Germain nchini Ufaransa wakati Real Madrid wanawakaribisha Borussia Dortmud kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Mourinho: Nahitaji mshambuliaji wa kweli

Barcelona wazuiwa kusajili