in , , ,

Man U waoga kichapo

 

 

Manchester United wamekuwa kama washuka ngazi, ambapo baada ya kuanza ligi kuu kwa ushindi mwembamba mara mbili, walikwenda suluhu na wikiendi hii kuoga kichapo.

 

Vijana wa Louis van Gaal walianza vyema baada ya Juan Mata kuwafungia bao la kuongoza katika dakika ya 48 akiunganisha majalo ya Luke Shaw. Hata hivyo Swansea wanaofundishwa na Garry Monk walipambana na kusawazisha dakika ya 61.

 

Mchezaji bora wa mechi hiyo, ambaye pia ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew alisawazisha baada ya dakika 13 na dakika tano baadaye akamtilia Bafetimbi Gome pasi maridadi iliyozaa bao la ushindi, huku kipa Sergio Romero wa United akiwa hana la kufanya.

 

Huu ni mchezo wa tatu mfululizo katika ligi Swansea wanashinda, kwani msimu uliopita waliwafunga United kwenye mechi zote mbili na wanakuwa timu ya sita tu kwenye ligi hii kuzoa pointi zote katika michezo mitatu ya ligi kuu.

'muuaji' wa Man U....
‘muuaji’ wa Man U….

 

United walionekana kuwa wazito kwenye kiungo na pia inaonekana kwamba katika ushambuliaji bado Wayne Rooney anaonekana kutokuwa na kiwango kizuri bado wakati kwa mtazamo mwingine ni kwamba hunda anahitaji mshirika mwingine kwenye ushambuliaji.

 

Upande wa ushambuliaji wa Man U pia ulionekana kuwa mbovu kwenye mechi hii, baada ya kuzuia washindano wao kupata bao katika mechi tatu za awali. Pamoja na kutawala mchezo kwa asilimia 64, bado United walipoteza pointi zote, na safari yao Liberty Stadium ikamalizika kwa huzuni kubwa.

 

Daley Blind ambaye ni kiungo alichezeshwa katika beki ya kati lakini alionekana kuzidiwa na washambuliaji, akiwamo Gomis aliyefunga bao la ushindi. Monk alionekana kuwa mjanja, japo alishangaza wengi, ambapo wakiwa nyuma kwa bao moja, alimtoa winga Wayne Routledge na kumwingiza kiungo Ki Sung-yueng.

 

Ni hapo ilianza kuchezwa kiungo mfumo wa ‘diamond’ na dakika tatu tu baadaye Ashley Williams aliwazidi nguvu Man U, akampata Gylfi Sigurdsson, ambaye majalo yake nzuri ilimkuta Ayew akasawazisha kabla ya Gomis kutia la pili.

 

Wakiwa wametoka kwenye ushindi mnono dhidi ya Club Brugge na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Van Gaal Jumapili hii aliwaita wachezaji wake wawili aliowasajili kiangazi hiki, Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin waliopumzika walipocheza na Brugge, lakini hawakumsaidia.

 

Kiungo Ander Herrera alisogezwa mbele kucheza nyuma ya Rooney, lakini United walionekana kutokuwa wachangamfu. Moja zuri kwa United ilikuwa uchezaji mzuri wa Mata japokuwa alichezeshwa eneo ambalo hajazoea

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Farah, Bolt usipime

Tanzania Sports

Kenya kidedea