in , , , ,

Man U wampata Memphis Depay

*Manchester City wamkimbilia Pogba

*Inter Milan kumchukua Toure bure

 

Manchester United wameanza biashara ya usajili mapema na tayari wamekubaliana na PSV Eindhoven kumchukua mshambuliaji wao, Memphis Depay kwa ada ya kati ya pauni milioni 25 na 30.

 

Depay (21) alicheza chini ya Kocha Louis van Gaal katika Timu ya taifa ya Uholanzi kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka jana.

 

Anatarajiwa kutua Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya na akifuzu atajiunga na Man U pindi dirisha la usajili litajapofunguliwa mwezi ujao.

Depay amecheza mechi 28 na PSV msimu huu na kufunga mabao 21 na hakuna mshambuliaji wa Man U aliyekaribia hata hayo.

 

Washambuliaji wakubwa Old Trafford ni Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao.

 

Kuingia kwa Depay kunatakiwa kuwatia hofu Van Persie na Falcao na Mholanzi huyo amesema kwa njia ya Tweeter kwamba anaingia United kutwaa vikombe kama alivyowasaidia PSV kuwa mabingwa msimu huu.

 

“Daima mie huota, huamini na kufanikiwa. Nilikuwa naota na kuamini kwamba tutakuwa mabingwa wa Eredivisie (Ligi Kuu ya Uholanzi) na PSV na tumefanikiwa,” anasema mchezaji huyu aliyeanzia akademia ya PSV na hajapata kujiunga na timu nyingine yoyote.

 

Man United wamewazidi kete klabu nyingine kama Paris Saint-Germain (PSG), Liverpool waliokuwa na nia ya kumsajili Depay. Inaelezwa kwamba Tottenham Hotspur walipeleka ofa yao ikakataliwa na PSV.

 

Tangu ajiunge na PSV amecheza mechi 104 na kufunga mabao 42. Old Trafford atakutana na Wadachi wenzake, Van Gaal, Van persie (kama atabakishwa) na Daley Blind.

 

TETESI ZA USAJILI LEO

yaya

 

 

Manchester City watawasilisha kwa Juventus ofa ya zaidi ya pauni milioni 50 ili kumsajili kiungo Mfaransa Paul Pogba, 22.

 

Man City watachuana na Chelsea, Barcelona na Real Madrid ambao pia wapo kwenye mbio za kumnasa mchezaji huyo wa zamani wa Man United aliyeachwa na Sir Alex Ferguson kwa madai hakuwa na kiwango.

 

Kuna tetesi kwamba Pogba amekataa ofa na mazungumzo ya awali na PSG. Wakala wa Pogba alionekana kwenye hoteli waliyofikia Real walipokuwa Italia kucheza na Juventus.

 

Inter Milan wameweka wazi nia yao ya kumsajili kiungo wa Manchester City kutoka Ivory Coast, Yaya Toure, 31, bila kulipa ada yoyote ili kuwasaidia City kulipa mshahara wake mkubwa.

 

Awali Toure alitaka kuhama City kwa maelezo kwamba wakubwa wa hapo hawampendi lakini klabu wakasema angebaki.

 

Hata hivyo, wakati ligi kuu ikielekea ukingoni, wakubwa hao walisema walikuwa wakitafuta pa kumuuza maana kiwango chake kimeshuka, naye akasema angebaki hadi mkataba wake uishe.

 

Huenda Inter wakatoa suluhu ili akaungane na kocha wake wa zamani, Roberto Mancini.

 

Newcastle wanafikiria kumchukua Kocha Msaidizi wa Real Madrid, Paul Clement kwa ajili ya kukipiga kama kocha mkuu St James’ Park.

 

Chelsea wanaamini kwamba mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi, 22, atakataa mkataba mpya klabuni hapo ili aingie Stamford Bridge kwa ada ya pauni milioni 22 kiangazi hiki.

 

Inter na Roma watapigishana vikumbo na Arsenal kwa ajili ya kupata saini ya kipa wa Chelsea, Petr Cech, 32, ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu.

 

Winga wa Manchester United, Nani, 28, amesema hataki kuchezea Sporting Lisbon msimu ujao. Nani ni Mreno lakini hataki kuchezea nyumbani kwao.

 

Hatima ya mshambuliaji wa Palermo, Paulo Dybala, 21, anayetakiwa na Chelsea itaamulia ndani ya wiki mbili zijazo, uongozi wa klabu yake umesema.

 

Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero, 26, atakuwa na programu maalumu ya mazoezi kujiandaa na msimu ujao, program inayolenga kumwepusha na kuumia misuli ya paja mwakani.

 

Kocha Msaidizi wa zamani wa Aston Villa, Roy Keane amedai kwamba Kocha wa sasa klabuni hapo, Tim Sherwood alianza ‘kujiandaa’ kuwa kocha klabuni hapo hata kabla Kocha Paul Lambert hajafukuzwa.

 

Keane amesema kwamba alikwenda kutazama mechi ya Villa na Bournemouth katika Kombe la FA na Sherwood alikuwa kaketi nyuma yake na kwamba anaamini alikwenda Villa Park mara mbili au tatu.

 

“Kuna watu ambao huenda mpirani si kwa ajili ya kutazama bali kwa vile wanahisi wanaweza kupata kazi hapo,” akasema nahodha huyo wa zamani wa Manchester United.

 

Keane ambaye sasa ni kocha huyo msaidizi wa Ireland Kaskazini amesema kwamba angekuwa yeye, akijua kocha fulani yu matatani na yeye alikuwa akihusishwa na kazi hiyo, angekwenda kwenda sehemu hiyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Ni Yanga na Azam Afrika

Wahamiaji watikisa kandanda Italia