in , , ,

Man City wamtaka Messi

 
Katika hali isiyotarajiwa, Manchester City wanatafakari kumsajili nyota wa Barcelona, Lionel Messi.

City wanaomilikiwa na matajiri wa mafuta wa Mashariki ya Kati, wapo tayari ‘kuvunja benki’ kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 28.

Taarifa zinasema kwamba tayari mawakala wa Messi wameanza majadiliano ya awali juu ya dili hilo ambapo City wanataka kumvutia Messi na kumpatia mshahara mnono wa pauni 800,000 kwa wiki, na itakuwa ni rekodi mpya kwenye soka hapa England.

Messi (28) amekuwa Barcelona tangu 2001 akichezea kikosi cha vijana baada ya kutoka Newell’s Old Boys, kisha akapanda Barcelona C, B kabla ya 2004 kuanza kukipiga wkenye kikosi cha kwanza na timu ya taifa ya nchi yake.

Inaelezwa kwamba Messi yupo tayari kuondoka Camp Nou baada ya miaka yote hiyo na kuijaribu soka ya England yenye mvuto zaidi duniani na kwamba dili likikubali inavyofikiriwa, atatengeneza pauni milioni 40 kwa mwaka, pauni milioni 32 kati ya hizo zikiwa ni mshahara na kiasi kilichobaki ni malipo kwa kutangaza bidhaa pamoja na bonasi.

Kwa sasa Messi anapata pauni 500,000 kwa wiki na mkataba wake huko unamalizika 2018, lakini unaweza kusitishwa kwa kuwalipa fidia Barcelona, na hilo si jambo gumu kwa Sheikh Mansour. Katika mkataba wake, kumewekwa kipengele kwamba anayetaka kumnunua ni pauni milioni 250 lakini haidhaniwi kwamba ni uhalisia.

Inasemekana kwamba huenda Barcelona wakakubali ofa ya pauni milioni 120 kwa mchezaji huyo aliyepata kutwaa tuzo ya mwanasoka bora – Ballon D’Or mara nne. Barcelona wanaonekana kukazania zaidi kuhuisha mkataba wa Neymar kuliko Messi, na nyota huyo anaona kana kwamba anadharauliwa.

Neymar na Luis Suarez wamekuwa wakitamba sana kwenye mechi za Barca karibuni huku Messi akiwa anauguza majeraha. Pia ameandamwa na mashitaka ya kukwepa kodi pamoja na baba yake, hivyo anadhaniwa kufikiria upya hatima yake nchini Hispania. Messi ametwaa ubingwa wa Ulaya akiwa na Barcelona mara nne.

Pamoja na Messi, pamekuwapo tetesi kwamba Barca wanataka pia kumchukua kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola aliyekuwa na Messi Barcelona. Ofisa Mtendaji wa City, Ferran Soriano na mkurugenzi, Txiki Begiristain, wana uhusiano mzuri na Messi na baba yake, ambaye pia ndiye wakala wake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsenal, Chelsea safi

Tanzania Sports

Man City warudi kileleni