in , , ,

Man City, United na vita ya Ramos

Ramos

*Arturo Vidal kwenda Arsenal?

Wakati Manchester United wakijiandaa kuongeza fedha kumpata beki wa kati wa Real Madrid, Sergio Ramos, jirani zao – Manchester City wameingia kwenye vita ya kumnasa Mhispania huyo.

Baada ya kukataliwa ofa yao ya awali ya kati ya pauni milioni 28 na 35, United wameamua kuongeza dau kumnasa mchezaji huyo aliyesema wazi anataka kuondoka Santiago Bernabeu.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, Real wamesema kwamba Ramos (29) anaweza kuuzwa tu iwapo klabu itatoa pauni milioni 64, kiwango kinachoonekana ni kikubwa mno.

Man U walitaka pia kutumia nia ya Real kumsajili kipa wao, David De Gea kama daraja la kumpata kirahisi Ramos, lakini kuibuka kwa City kunawachefua United, ikizingatiwa wana ukwasi mkubwa.

Man U nao wamewageuzia kibao Real Madrid kwa kuongeza bei ya De Gea, wakisema kipa huyo atauzwa kwa rekodi ya dunia, juu ya pauni milioni 35 wakati Real wanataka kutoa pauni milioni 20 tu.

Wiki iliyopita, Pedro Riesco anayefanya kazi na kaka wa Ramos, Rene ambaye pia ni wakala wake, anasema baada ya yote yaliyotokea itakuwa vigumu sana kwa Ramos kubaki Madrid.

United walitumia mwanya huo kutoa dau lao na wakati wakielekea kuwa vizuri kumchukua, City wanaonekana kutia mchanga kwenye kitumbua chao.

City wapo tayari kumwaga kiasi kikubwa cha fedha kiangazi hiki kunasa wachezaji wazuri ili kumpa kocha Manuel Pellegrini nguvu ya kutwaa mataji baada ya kumaliza msimu uliopita mkavu.

Mwenyekiti wa Bodi ya City, Khaldoon Al Mubarak ameahidi kuwasili kwa wachezaji wapya wenye kiwangom cha juu watakaowapeleka mbali City.
Wameshatuma ofa Liverpool na kukataliwa kumchukua mshambuliaji wao, Raheem Sterling na wapo kwenye mkakati wa kumchukua kiungo wa Juventus, Paul Pogba.

Wanataka pia kumsajili winga wa Wolfsburg, Kevin De Bruyne anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30. Kuingia kwao kwenye vita ya kumtaka Ramos sasa ni ishara wazi kwamba wamelenga kujiimarisha vilivyo.

ARTURO VIDAL AKARIBIA ARSENAL

benzema

Zipo habari kwamba kiungo wa kimataifa wa Chile anayekipiga Juventus, Arturo Vidal, 28, anakaribia kujiunga na Arsenal kiangazi hiki.

Licha ya Man United kutaka kumsajili mchezaji huyo tangu kiangazi cha mwaka jana, inaelezwa kwamba Arsenal wanakaribia kuafikiana na Juve kumnunua kwa pauni milioni 21.

Vidal amekaa misimu mitatu Torino, lakini licha ya kuchukuliwa kama mmoja wa wachezaji mahiri, klabu wanatakiwa kuuza kabla ya kununua.
Tayari wamemsajili kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira na inatambulika kwamba fedha itakayopatikana kwa kumuuza Vidal itakuwa kwa ajili ya ofa ya kumpata kiungo wa Bayern Munich, Mehdi Benatia.

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Freddie Ljungberg, ameeleza kufurahishwa na habari za Vidal kuelekea Emirates, akisema ni mchezaji mahiri atakayeungana vyema na Mchile mwenzake, Alexis Sánchez kuwasaidia Arsenal kupigania ubingwa kiukweli.

TETESI NYINGINE ZA USAJILI
PP

Mshambuliaji wa Liverpool, Fabio Borni, 24, anatarajiwa kuuzwa West Ham kwa thamani ya £8m. hata hivyo, kuna tetesi kwamba anaweza kutumika kama chambo kwa Liver kumpata Christian Benteke katika dili linaloweza pia kumhusisha Rickie Lambert.

Liverpool wanaelekea kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa England na Southampton, Nathaniel Clyne, 24, kwa pauni milioni 12.5.

Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri ameeleza tamaa yake ya kumpata kiungo wa Chelsea, Oscar, 23.

Wakati huo huo, Chelsea wanahusishwa na kiungo mshambuliaji wa Atletico Madrid, Arda Turan, 28, huku wakala wake akizungumza na klabu nyingine tatu.

Newcastle wanamtaka winga wa West Ham, Stewart Downing, 30, lakini wanakabili ushindani kutoka kwa Sunderland na Leicester.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

ROBO FAINALI CONCACAF

Petr Cech kamili Arsenal