MFUKO wa Pensheni wa PSPF, “umevuna” mamia ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Shule ya Biashara), ambao wamejiunga ma mpango wa uchangiaji wa hiari PSPF Supplementary Scheme-PSS wakati wa kongamano lililopewa jina, (Women University Platform), na kufanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Sio tu wanafunzi pekee walijiunga na mpango huo, lakini pia watu maarufu kama vile, Mwanamuziki nyota wa muziki wa Bongo Flava, Vanessa Mdee,na mpeperushaji wa vipindi vya runinga vinavyohusu masuala ya wanawake, Joyce Kiria ambao walikuwa ni miongoni mwa wasemaji wakuu kwenye kongamano hilo walijiunga pia.
Kujiunga kwa wanafunzi hao kwenye mpango wa PSS, kulifuatiwa na mfululizo wa elimu ya huduma zitolewazo na Mfuko huo yaliyotolewa na Afisa a Operesheni wa PSPF, Hadji Jamadary, afisa matekelezo, Albert Feruzi, wakiongozwa na Meneja wa mpango huo, yaani PSS, Mwanjaa Sembe, na Balzoi wa PSPF, Mwnaamitindo “nguli” wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata.
Maafisa wa Mfuko huo, Rahma Ngassa, Gasper Lyimo na wengineo, walilazimika kufanya kazi ya ziada, kuwasaidia wanafunzi hao kujaza fomu hizo na kuchukua picha zao tayari kuwatengenezea vitambulisho.
Mambo yaliyowavutia wanafunzi hao na kuamua kujiunga na mpango huo ni zile faida wanazopata wanachama wa PSPF, kama vile Fao la mikopo ya elimu, jipange kimaisha, fao la uzazi, afya, na mikopo ya nyumba na viwanja.
Kongamano hilo lilitanguliwa na kongamano kama hilo lililofanyika Chuo Kikuu Cha Tumaini (tawi la Dar es Salaam, ambapo kazi kama hiyo ilifaywa na Mhamasishaji Anthony Luvanda, kutoka kampuni ya Home of Events, Afisa Masoko Mwandamizi, wa PSPF, Magire Werema, Rahma Ngassa, Delphin Richard, Gasper Lyimo na Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto.
———————————