in , , ,

Machozi ya Nabi ni mzigo mpya wa klabu za Tanzania

Ligi kuu Tanzania imeshuhudia makipa wazuri sana. Makipa kama Steven Nemes, Mohammed Mwameja,Ali Bushiri,Juma Kaseja, Ivo Mapunda na wengineo, lakini kati yao hakuna aliyewahi kuchukua tuzo ya golikipa bora wa mashindano yanayoandaliwa na CAF. Golikipa wa Yanga Djigui Diara. Ni mzigo mwingine kwa makipa wa Ligi ya Tanzania. 

MABINGWA wa soka nchini Tanzania klabu ya Yanga wameshindwa kutwaa taji la Kombe la Shirikisho licha ya kushinda bao 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji USM Alger kwenye dimba la Julai 5 jijini Algiers, na kumshuhusia kocha wao mkuu maarufu kama Profesa, Nasreddine Nabi akimwaga machozi mara baada ya kupulizwa filimbi ya  kuashiria mchzo kufika tamati. 

Hofu na mashaka zilizowakumba wenyeji USM Alger zilionekana mara baada ya kuanza kulalamika mitandaoni na kueleza kufanyiwa fitina katika uwanja wa Benjamin Mkapa licha ya kushinda mabao 2-1. Ilikuwa dhahiri wenyeji wenza wa fainali hiyo walikuwa wanaiogopa Yanga ambayo machozi ya kocha wao yameleta mzigo mpya kwa klabu za soka nchini Tanzania. Mashaka ya wenyeji yalidhihirika katika mchezo huo ambao Yanga waliwatandika bao moja licha ya kushindwa kuongeza la pili ambalo lingewapa taji.

Mabeki watano Yanga

Katika mchezo huo kocha Nasreddine Nabi alifanya mabadiliko makubwa ya kiufundi kwa kuanza na mabeki watano kuimarisha safu ya ulinzi. Mfumo huo ulikuwa na mabeki wa aina mbili ambao wale waliokuwa na jukumu la kushambulia na wengine kulinda. 

Lomalisa Mutambala na Djuma Shaban walirudi katika kikosi cha kwanza cha Yanga wakiwa na lengo ya kushambulia toka mwanzo wa mchezo. Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca walikuwa na jukumu la ulinzi. Matunda ya mbinu yalijitokea ndani ya dakika tano za mchezo baada ya Yanga kupata penati kufuatia Fiston Mayele kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari. Djuma Shaban bila ajizi akatumbukiza mpira kimyani.

Nabi aliwashtua mashabiki

Kama kuna jambo ambalo kocha huyo aliwafanyia jambo la kushtukiza ni uamuzi wa kumweka benchi kiungo wake ngangari na kiraka Yannick Bangala, na badala yake akacheza kamari kwa Salum Abubakar na Mudathir Yahya waliokuwa kwenye eneo la kiungo. Yanga walicheza bila kiungo wake mkuu Khalid Aucho ambaye alikosa fainali hiyo kutokana na sheria kumbana baada ya kupata kadi mbili za njano. Uamuzi wa kuwapa nafasi kwenye kiungo Mudathir na Salum Abubakar uliwaacha na mshangao wengi lakini Nabi amedhihirisha kuwa yeye ni Profesa kama wanavyoitwa na mashabiki wake.

Mzigo wa machozi ya Nabi

Tanzania Sports

Katika soka la Tanzania mafanikio makubwa yaliyofikiwa yalikuwa ya klabu kongwe ya Simba ikiwa na mastaa kama Ramadhani Lenny, Damian Kimti, Thomas Kipese,Mohammed Mwameja, George Masatu,Edward Chumila ‘Ball Jangler” ambayo ilitinga fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 dhidi ya Stella Abdijan. 

Simba walipoteza katika mchezo wa marudiano jijini Dar Es Salaam baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0. Machozi ya Nasreddine Nabi yana maana kuwa viwango vipya vya mafanikio ya soka vimewekwa rasmi katika kizazi cha sasa. Kwamba timu za Tanzania kuishia hatua ya robo fainali iwe kwenye Ligi ya Mabingwa, Kombe la Shirikisho ama jingine lolote sio habari tena, badala yake mafanikio makubwa yanayotakiwa kufanyika sasa ni kuipiku rekodi iliyowekwa kwa machozi ya Nabi. 

Mzigo wa tuzo ya Mayele

Katika mchezo wa kwanza jijini Dar Es Salaam Fiston Mayele alipachika bao maridadi katika mazingira magumu na kudhihirisha kuwa yeye ni moto wa kuotea mbali. Mshambuliaji huyo wa Yanga amemaliza mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa kupachika mabao 7.

Emmanuel Okwi alikuwa miongoni mwa wafungaji bora kwenye mashindano ya AFCON miaka kadhaa iliyopita akitookea klabu ya Simba, lakini ngazi ya klabu hakuna mchezaji wa Tanzania aliyefikia rekodi ya Fiston Mayele kwa miaka ya karibuni. Kwa maana hiyo washambuliaji wa klabu za Tanzania wanakabiliwa na mlima wa kutafuta mafanikio kwa kuvunja rekodi hii. 

Mvuto wa Ligi Kuu Tanzania

Kwa namna nyingine machozi ya Nabi yameonesha kuwa Ligi Kuu Tanzania inavutia wachezaji wengi ambao wangelitamani kucheza hapa nchini. Si Yanga pekee, hata klabu ya Simba jinsi ilivyopambana katika misimu mitano mfululizo kuchuana na vigogo wa soka Afrika inaonesha kuwa Ligi ya inakua kwa kasi. Simba walitolewa kwa paneti mara mbili kwenye Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates na Ligi ya mabingwa dhidi ya Wydad Casablanca. 

Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Karim Boimanda amesema, “Miaka michache nyuma haikuwa rahisi kwa klabu za Tanzania kuonesha kiwango bora na kunyamazisha mashabiki wa wapinzani tukiwa ugenini. Sasa inatokea mara kwa mara, tumeanza kuzoea nah ii ni hatua muhimu katika kuendelea kuwasogelea hao wanaoitwa vigogo wa soka Afrika. Ushirikiano na hamasa kutoka serikalini, usimamizi bora wa Ligi, umoja katika klabu, hamasa ya amshabiki,ubunifu katika uongozi wa klabu,usajili wa wachezaji bora,kuajiri maafisa bora wa ufundi, fedha za wadhamini na mchango wa vyombo vya habari katika kutangaza habari za timu zetu, ndiyo msingi wa mafanikio ya Ligi yetu,”

Mzigo wa rekodi ya Djigui

Tanzania Sports

Ligi kuu Tanzania iemshuhudia makipa wazuri sana. Makipa kama Steven Nemes, Mohammed Mwameja,Ali Bushiri,Juma Kaseja, Ivo Mapunda na wengineo, lakini kati yao hakuna aliyewahi kuchukua tuzo ya golikipa bora wa mashindano yanayoandaliwa na CAF. Golikipa wa Yanga Djigui Diara. Ni mzigo mwingine kwa makipa wa Ligi ya Tanzania. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Manchester City

Manchester City: waleteni hao Inter Milan sasa

Man u

Mapengo matano Manchester United