Liverpool wamepoteza mechi ya mkondo wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kwenye uwanja wa ugenini kwao Atletico Madrid na sasa watategemea nguvu ya waandamizi wao kupindua meza watakaporudiana.
Baada ya kichapo cha kwanza katika mechi ya ushindani mkubwa katika kipindi cha miezi mitano, mabingwa hawa wa Ulaya wanaweza kujifariji na historia ya hivi karibuni. Liverpool si wageni kwa matokeo mabaya kwenye viwanja vya ugenini.
Walipoteza mechi zote tatu za hatua ya makundi katika safari yao ya kuja kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu uliopita. Napoli walikuwa miongoni mwa wababe wao enzi hizo na walikuja kuwapiga tena Septemba.
Na, bila shaka, kuna kichapo cha 3-0 kule Camp Nou cha kutafakari. Maana walikuja kuapiga vibaya mnoBarcelona nyumbani – mabao manne kwa nunge, kitu ambachohakikuwa kimefikirika kabisa, kwamba Lionel Messi asingefunga walau bao moja na kuchomoa.
Hayo yanaangaliwa wakati Atletico Madrid wa Diego Simeone ambao msimu huu wapo hovyo, watakapotia mguu Anfield, dimba lenye hali ya hewa tofauti kabisa Liverpool wanapowaaribisha wageni Merseyside.
Liverpool watakuwa mbele ya maelfu ya washabiki wao na fashifashi; ule wekundu angani na nguvu ya wachezaji wa Jurgen Klopp ni hazina kubwa kwao ambapo itabidi wajilinde vyema wasifungwe nyumbani lakini kuhakikisha wanapata zaidi ya bao moja.
Waliporudiana na Barcelona hapo Anfield, kilichoonekana ilikuwa kukamiana, kutishiana kuliko kushindana. Hiyo ilionekana tangu mwanzo, pale Andy Robertson alipomburusha Messi kisogoni, lakini pia mchezaji wa zamani wa Liver, Luis Suarez kuwa katika hamaki na hasira kuliko kujituma taratibu. Huyu alikwatuliwa pia na Fabinho.
Philippe Coutinho aliondoshwa uwanjani na mchezaji mwingine kuingia baada ya saa moja, wakati alikuwa nyota wa Anfield zamani. Hewa ya kitisho ilionekana dhahiri na mara Liver wakafungua kitabu kwa bao la mapema la Sadio Mane, la pili la Javie Mascherano, la tatu la Divock Origin a la dakika a majeruhi la Marko Grujic.
Ilifika mahali mwana wa Messi akamwambia baba yake; “Mimi ni Liverpool, wewe ni Barcelona.” Ni fedheha. Usiku huo ulichangia kwa kiasi kikubwa mwenendo mkali wa Liverpool na kuzidi kuwawashia moto wapinzani wao, wakashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) nyuma ya Manchester City na msimu huu Liver ni kana kwamba wameufikia ubingwa, hadi sasa hawajapoteza mechi EPL.
Hata hivyo, Atletico si wa kubeza; ni hatari sana hasa wanapokuwa tayari na kitu mkononi, nao wana bao moja tayari katika dakika 90 wakisubiri dakika nyingine kama hizo. Kwenye dimba la Wanda Metropolitano mechi ile ya Jumanne Februari 18, 2020 ilikuwa kali na ngumu hasa, Atletico wakifunga mapema kupitia kwa Saul Niguez dakika ya nne.
Atletico wanajua kujipanga hasa kwenye ulinzi kiasi cha kuwachanganya wapinzani wao na hapana shaka kwenye marudiano watafanya hivyo. Vijana wa Klopp walitawala zaidi mchezo lakini hawakulenga goli hata mara moja na Atletico ni wazuri kwenye mashambulizi ya kushitukiza.
Simeone akasema; “kuna usiku kadhaa ambazo hazisahauliki, na huu ni mmoja wa hizo. Timu bora zaidi duniani ilikuja hapa, timu isiyopoteza mechi lakini tumewafunga.” Ni kusubiri kuona dakika hizo nyingine 90 za mechi ya mkondo wa pili.