*Arsenal watuma salamu mpya
Wakati Liverpool wametolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), Arsenal wametuma salamu kwa wapinzani wao, kwa kuwafyatua Galatasaray 4-1 na kufungana pointi na Borussia Dortmund.
Wakicheza nyumbani, hali ilikuwa tofauti kabisa na siku nyingine, washabiki hawakuwa wengi na matarajio hayakuwa makubwa, kweli wakaanza kufungwa na Basel mapema dakika ya 25 kupitia kwa Fabian Frei, bao lililodumu hadi dakika tisa kabla ya mechi kumalizika, Steven Gerrrard alipofunga.
Washabiki wa Basel waliwakejeli wale wa Liverpool kwa wimbo wa Reds wa ‘You will never walk alone’ lakini ulikuwa ukweli mchungu kwamba Liver wamatupwa nje ya mashindano hayo, baada ya kushinda mechi moja tu kati ya sita za kundi B.
Hii inamaanisha kwamba vijana wa Brendan Rodgers watarudi kwenye Ligi ya Europa, ambayo ni ndogo na watakuwa na mshikemshike wa msongamano wa mechi. Real Madrid na Basel wanasonga mbele wakati Liver na Ludogorets wametupiwa virago.
Wakati Real Madrid wamemaliza wakiwa na pointi 18 wakishinda mechi zao zote, Basel walipata saba kwa kushinda mechi mbili, Liver wakaambulia tano na wenzao nne tu. Liverpool wangeshinda Jumanne hii.
Kocha Rodgers amekiri kwamba vijana wake hawakufanya vyema uwanjani na nahodha Gerrard ambaye muongo mmoja uliopita aliwaokoa Liverpool kwa kufunga dhidi ya Olympiakos alikaribia kufanya hivyo kwenye mechi hii, baadaye akasema hawakuwa wazuri vya kutosha.
Kwa upande mwingine, Arsenal wakicheza ugenini, walionesha makali tofauti na wanapokuwa kwenye Ligi Kuu ya England ambapo waliwakamua Galatasaray 4-1 kwa mabao ya Lukas Podolski mawili na Aaron Ramsey mawili, likiwamo moja la mguu wa kushoto linalodhaniwa kuwa moja ya bora zaidi kwenye michuano hii.
Walifunga mabao matatu ya mwanzo ndani ya nusu saa, kuanzia dakika ya tatu kupitia kwa Podolski, kisha Ramsey akatupia mawili, la tatu likiwa dakika ya 29 kabla ya Mjerumani kumalizia kushonea la nne dakika ya 90.
Wesley Sneijder alifunga kwa mpira wa adhabu ndogo na kuwa bao la kufutia machozi. Hata wangeshinda mechi hiyo walishatupwa nje, kwa Arsenal na Dortmund kuvuka, Arsenal wakiwa wa pili kutokana na tofauti ya uwiano wa mabao. Wote wawili wana pointi 13 na wamefungwa mara moja tu.
Katika mechi nyingine, Juventus walikwenda suluhu na Atletico Madrid, Olympiakos wakawafunga Malmo 4-2, Real Madrid wakawashushia kipigo cha 4-0 Ludo Razgd, Benfica suluhu na Bayern Leverkusen, Monaco wakawazidi Zenit St P 2-0 na Dortmund wakaenda sare ya 1-1 na Anderlecht.
Mechi za mwisho za makundi ambayo hayakucheza jana zinafanyika Jumatano hii.
Comments
Loading…