in , , ,

Liverpool bila Mane si kitu?

LIVERPOOL imekuwa na wiki kadhaa mbaya Januari hii, wakishinda mechi
moja tu kati ya saba na kufurushwa kwenye michuano.

Jurgen Klopp anaweza kujitetea kwamba wachezaji wamechoka na
mlundikano wa mechi msimu wa sikukuu, lakini timu nyingine pia
zimecheza.

Moja lililo wazi kwa jinsi wanavyochechemea ni kukosekana kwa mtu wao
muhimu, Sadio Mane aliye kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) nchin Gabon.

Liver waliteleza vibaya kwa kufungwa na vibonde wa mwaka huu, Swansea
na kushangaza wengi, lakini pia wakatandikwa na Southampton
Walianza ligi kwa nguvu wakiwapapatua Arsenal wakaenda vyema na
wakaonekana kuwa washindani wa kweli wa ubingwa wa England, kabla ya
Januari kuanza kuwaendea kombo, wakimkosa Mane aliyenunuliwa kwa pauni
milioni 30.

Takwimu zinaonesha wazi jinsi Liver wanavyoshindwa kufurukuta bila mtu
huyu aliye na Senegal nchini Gabon, akisubiriwa kwa hamu na Liverpool
arudi.

Wangependa sana kumwona akiwa amerudi kabla ya mechi yao dhidi ya
Chelsea, maana ni big match na wangepata ushindi wangefurahi kwani
licha ya kujiweka pazuri wangekata pengo la pointi lililopo baina yao
ambalo ni kubwa.

Walipigwa na kutolewa nje ya Kombe la Ligi na Saints, ambapo ile kasi
waliyokuwa nayo kabla ta Krismasi ilipungua kabisa, wakatoka kwenye
uchaya na kuingia kwenye uhasi.

Liver nadhani hawakuwa wanajua au kupata picha halisi jinsi
wanavyomhitaji Mane. Hizi sasa ni alama za onyo kwao, wajipange na
wacheze kitimu badala ya kutegemea mtu mmoja.

Wananikumbusha enzi zile za Luis Suarez na kuondoka kwake kulivyompa
wakati mgumu kocha Brendan Rodgers, akatumia mamilioni ya pauni
kununua wachezaji wengi kujaribu kuziba pengo hilo lakini akashindwa
kabisa hadi akapoteza kibarua chake.

Mabao yaliyokuwa yakifungwa kwa wingi na The Reds yamekauka kwa kiasi
kikubwa, kama miti inavyokauka kutokana na kukosekana mvua.

Tangu Mane aondoke, Liver wamefunga mabao manne tu na bado Mane ni
mfungaji mwenza bora wa klabu hata kama hajacheza mechi zote hizo.
Liver wameshindwa kabisa kuendeleza ule mchaka mchaka uliokuwa
unawatatiza wachezaji wa timu pinzani na kujikuta wakirudi golini mwao
kuzuia.

Mane akiwapo na Liverpool walifunga wastani wa mabao 55 na wakati
hayupo ni tisa tu. Mechi alizokuwapo ni 21 wakashinda 15 na kwenda
sare moja na kupoteza mchezo mmoja.

Akiwa hayupo alicheza mechi tisa wakashinda tatu, sare mbili na kupoteza nne.
Utaona kwamba wastani wa ushindi ni asilimia 71.43 akiwapo na wastani
wa asilimia 33.33 akiwa hayupo. Utegemezi kwa kwa kiwango kikubwa
sana.

Simba wa Teranga – Senegal, wanacheza dhidi ya Cameroon Jumamosi hii
na ikiwa watavuka basi Liver watazidi kuumia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

SINGANO, MAHUNDI KABEBA ‘JENEZA’ BEGANI MWAKE.

Tanzania Sports

KIPI WAKIFANYE AZAM ILI WASHINDE MECHI DHIDI YA SIMBA?