in , , ,

Leicester ‘shoka’ moja ubingwa

Leicester City wanahitaji ushindi kwenye mechi moja tu ili kutawazwa
mabingwa wapya wa England.

Na ubingwa unaweza kuwa karibu kabisa, ikiwa Jumapili hii watawapiga
Manchester United, mabingwa mara 20 wa Ligi Kuu ya England kwenye
mechi itakayofanyika Old Trafford.

Hali hii mpya imekuja baada ya washindani wao wa karibu, Tottenham
Hotspur kuambulia sare ya 1-1 nyumbani kwa West Bromwich Albion
Jumatatu hii, ikimaanisha sasa Spurs wapo nyuma ya The Foxes kwa
pointi saba nzima, huku mechi zilizosalia zikiwa ni tatu tu.

Vijana wa Claudio Ranieri walianza msimu huu wakiwa wanachukuliwa kuwa
si tu wasindikizaji, bali kwamba wangeshuka daraja. Kati ya watu 5,001
waliotoa maoni yao, ni mmoja tu aliwapa nafasi ya kutwaa taji hilo
lililokwishatemwa na Chelsea.

Msimamo wa EPL, Kwa baadhi ya timu
Msimamo wa EPL, Kwa baadhi ya timu

Wagombea ubingwa ambao wamekuwa wakipewa nafasi kubwa, Arsenal,
Manchester City, Manchester United na Chelsea walishindwa kuwa na
uendelevu katika ufanisi mchezoni, Chelsea wakianza vibaya kuliko
ilivyopata kutokea, hata kufikia kumfukuza kocha wao, Jose Mourinho.

Kocha wa West Brom, Tony Pulis, akizungumza baada ya kuwalazimisha
Spurs sare hiyo, amesema wazi kwamba anataka Leicester watwae ubingwa,
akisema simulizi kuwahusu ni tamu mno, akisema hadhani kwamba inaweza
kutokea sehemu nyingine hapa nchini.

“Wanachoweza kufanya Leicester ni kupigana na kuchimbua matokeo kwa
nguvu na ndicho walichofanya hadi sasa. Kwa kweli inafurahisha, lakini
bado wana kazi kubw aya kufanya,” akasema Pulis baada ya kumkata ngebe
kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino ambaye bado amekuwa akiota kutwaa
ubingwa msimu huu.

Leicester wamebakiza pia mechi dhidi ya Everton nyumbani na Chelsea
ugenini, wakati Spurs watamalizia dhidi ya Chelsea ugenini,
Southampton nyumbani na Newcastle ugenini. Spurs walianza kufunga
kwenye mechi ya Jumatatu katika dakika ya 33 kwa bao la Craig Dawson
la kujifunga mwenyewe akishindwa kuokoa majalo ya Christian Eriksen.

Dawson alirekebisha makosa yake kwa kusawazisha katika dakika ya 73.
Leicester wana pointi 76, Spurs wanazo 69, Man City 64 sawa na Arsenal
wakati Man United wanazo 59 lakini wana mchezo mkononi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Mahrez mwanasoka bora wa mwaka

Tanzania Sports

YANGA YAUA 2-1 CCM KIRUMBA