in ,

KUNA UWEZEKANO MKUBWA TIMU ZA EPL ZIKACHUKUA UTAWALA WA TIMU ZA LA LIGA MSIMU HUU

Msimu wa mwaka 2011/2012 ndiyo ulikuwa msimu wa mwisho wa timu ya
England kuonekana ikifika katika fainali ya UEFA .

Msimu ambao Chelsea ilichukua kikombe hicho mbele ya Bayern Munich kwa
mikwaju ya penalti.

Hakuna aliyetegemea kama Chelsea ingeweza kuifunga Bayern Munich
iliyokuwa bora kipindi hicho, ubora ambao Chelsea kwa kipindi hicho
hawakuwa wameufikia.

Hata aina ya makocha waliokuwa wamekaa kwenye mabenchi yote mawili
yani la Bayern Munich pamoja na la Chelsea walikuwa wanazidiana kwa
ukubwa sana katika eneo hili la kufundisha na kusoma mbinu za mchezo
husika ili kupata ushindi.

Lakini mwisho wa siku Chelsea ikaibuka bingwa , ubingwa ambao
ulichagizwa na wachezaji kwa kiasi kikubwa kupigana kwa nguvu zao zote
ili wachukue kombe.

Miaka mitano imepita, miaka ambayo imekuwa migumu kwa timu za England
kwenye mashindano haya ya UEFA.

Kwa miaka 7 iliyopita timu za Hispania zimetoa wanafainali kwa 40%
timu za Ujerumani zimetoa wanafainali kwa 35% wakati timu za England
zimetoa wanafainali kwa 15%

Na mara ya mwisho kwa timu ya England kuingia fainali na kuchukua
kombe ni mwaka 2011/2012

Real Madrid wameingia mara tano katika nusu fainali kwa miaka 7
iliyopita, wakati Barcelona na Bayern Munich wameingia mara nne nusu
fainali.

Ukiangalia takwimu hizi zinakuonesha kuwa kwa kipindi kirefu
Wajerumani na Wahispania wametawala soka la ulaya.

Msimu huu ni tofauti na misimu iliyopita.

Ni Barcelona na Real Madrid pekee ambazo mpaka sasa zimeshinda kwa
100%, Sevilla kashinda kwa 60% akiwa na points 4 na Atletico Madrid
ikiwa na point moja tu mpaka sasa

Bayern kashinda kwa 50%, Borrusia Dortmund hajashinda hata mechi
moja.Wakati RB leipzig akiwa na point moja.

Hali hii ni tofauti na timu za England msimu huu, timu nne zina 100%
ya ushindi mpaka sasa.

Chelsea anaongoza kundi lake kwa alama 6 na kafunga goli 8 ,
Manchester United anaongoza kundi lake akiwa na alama 6 na kafunga
goli 7

Manchester city anaongoza kundi lake akiwa na alama 6 na kafunga goli
6, Spurs yuko nafasi ya pili ki alphabetical, Real Madrid anaongoza ki
alphabet na kafunga goli 6 akiwa na alama 6 pia

Liverpool pekee ndio hata hawajui wako wapi. Ingawa kundi lao linawapa
nafasi kubwa ya wao kupita.

Kwa sababu wanapoints 2 wakiwa nafasi ya pili na anayeongoza kundi
lake ana points 4.

Pia msimu huu timu za England zina vikosi imara tena vikubwa tofauti
na misimu michache iliyopita.

Vikosi ambavyo vinatoa nafasi kwao kuwa washindani kwa asilimia kubwa .

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NIMEIKUMBUKA MBEYA CITY KAMA NILIVYOMKUMBUKA DR.SLAA

Tanzania Sports

Jonas Mkude: Pambana na Hali Yako!