Miaka michache iliyopita, mmoja wa watu maarufu katika soka Afrika alinialika nyumbani kwake kwa chakula cha usiku.Wakati mkewe akiandaa Samaki na ndizi tulitazama soka, Sunderland wakiwafunga Arsenal kwenye michuano ya Kombe la FA.
Kadiri muda ulivyokwenda, wachezaji kadhaa wa zamani wakaanza kujitokeza. Walivyokuwa wakizungumza nikaona kwamba walikuwa wakila njama za kupanga mapinduzi dhidi ya rais wa shirikisho la soka la nchi yao.
Moja ya matatizo makubwa, niliambiwa, ni kwamba wizara ya michezo ilikuwa ikilipa mshahara wa kocha wa timu ya taifa lakini mawazo juu ya mpira yalikuwa finyu.
Shirikisho hilo, kama ilivyo kwa mengine mengi, lilishabaini kwamba iwapo lingeteua kocha Mzungu mshahara ungekuwa mkubwa na kwa mshahara kuwa mkubwa ikimaanisha kumegwa zaidi, na hivi ikaanza safari za Wafaransa kwenye soka ya Afrika.
Hii haimaanishi kwamba makocha wa Kizungu walikuwa, au ni wabaya kwa soka ya Afrika, hapana. Baadhi, kama Hervé Renard, Claude Le Roy na Winfried Schäfer – wamekuwa wazuri na wenye faida sana. Mbelgiji Tom Saintfiet alijiuzulu ukocha wa Gambia baada ya kutolewa katioka hatuia ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) wiki hii lakini amefanya kazi kubwa, akiwaongoza mara mbili The Scorpions kwenye fainali hizo ambazo kabla hawakuwa kufika.
Wala haimaanishi kwamba uteuzi wa Mzungu unaofanywa na taifa la Afrika ni lazima iwe imehusishwa rushwa, kuna wakati mashirikisho hayajifikirishi vya kutosha. Lakini, baada ya wiki mbili za aina yake za AFCON zilizoonesha soka nzuri kabisa kwa nyakati hizi, inaelekea kwamba kuna upepo wa mabadiliko unavuma barani.
Katika timu zote 24, ni timu tatu tu zilikuwa na kocha wa Kifaransa kwa asili. Kuiweka hii sawa na kwamba asilimia 27 ya makocha kwenye michuano 10 iliyopita walikuwa Wafaransa. Walikuwapo watatu kwa Cameroon 2021. Mara ya mwisho walipokuwa wachache zaidi ilikuwa kwa Afrika Kusini 1996.
Si lazima kuchukulia kwamba kuvuka makundi moja kwa moja ndiyo mafanikio kwa timu husika, kama ilivyo nadharia ya baadhi, ukiangaia mwenendo wa akina Aimé Jacquet na Didier Deschamps, pale makocha wanapotoa kipaumbele kwenye kushinda kwa ajili ya mataifa husika ili kuepuka kuchafua wasifu zao kwa kushindwa kama ilivyotokea kwa Jean-Louis Gasset aliyefukuzwa na Ivory Coast baada ya vipigo viwili, lakini bad oleo timu husika wapo kwenye robo fainali baada ya kuwapiga Senegal jana usiku.
Tmu zote tatu zilizokuwa na makocha wa Ufaransa zimeingia robo fainali lakini hakuna hata moja iliyoweza kujipamba kwa utukufu. Kocha mwneye umri wa miaka 64 – Hubert Velud, ambaye timu yake, Burkina Faso ilikuwa ya pili nyuma ya Angola ndio aling’aa zaidi walau.
Hii ni kazi yake ya 22 kama kocha na kwa Afrika ni taifa la tatu kufundisha. Akiwa kocha wa Togo, alipigwa risasi mkononi kabla ya mashindano kama haya nchini Angola. Tunaye Sébastien Desabre, ambaye timu yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilitoka sare kwenye mechi zake zote za makundi. Ana umri wa miaka 47, lakini yupo kwenye kazi yake ya 15 na kwa Afrika ni ya pili.
Aliyefanya vibaya zaidi ni huyu mwenye umri wa miaka 70 -Jean-Louis Gasset, kocha msaidizi wa zamani wa Paris Saint-Germain na France. Alifukuzwa baada ya mechi baina ya Ivory Coast na Guinea-Bissau ikifuatiwa na vichapo viwili.
Comments
Loading…