Machi 2019 Manchester United walikwenda Paris Saint-Germain (PSG) kwa mechi yao ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 kutokana na matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza.
Hadi nusu ya kwanza inaisha Paris, Man U walikuwa wakiongoza kwa 2-1, wakihitaji bao jingine moja tui li kuvuka kwa maana ya faida ya mabao ya ugenini. Kocha wao, Ole Gunar Solskjaer alikuwa makini kuliona la aina hiyo lakini kwa nusu saa hakuna kilichotokea.
PSG walikuwa wakifanya kazi hasa, kwanza wakifanya vyema lakini baadaye wakaonekana kuanza kuchanganyikiwa na Solskjær akatumia hali hiyo kuwasukuma vijana wake kwa kazi, na kweli United wakapata penati baada ya mchezaji wa PSG kuushika mpira ndani ya eneo la hatari, United wakapata.
Akiwa katika kilele cha mafanikio hayo, Garry Neville alianza kuuliza iwapo alitaka wapi iwekwe sanamu yake, japokuwa bado alikuwa katika raha lakini akitaka asigeuke kuwa Jose Mourinho, akashindwa kwa kiasi fulani kuwapanga vyema wachezaji wake kwa mashambulizi, pengine kutokana na hisia.
Wakarudi kwa mtindo wa kupaki basi, na laiti kama PSG wangetia nguvu zaidi, kocha huyo wa Man U angekuwa na maswali mengi juu ya kulikoni alifanya maamuzi yale. Wachezaji walikuwa wakikaa tu na kusonga mbele kwa kasi pale walipoambiwa, tofauti na muda mwingine wote wa awali wa mechi. Hisia zilikuwa zikivuruga hali ya mchezo, na hiyo imekuwa aina ya soka ya England.
Data inathibitisha kuvutia mambo kwa aina fulani kwa kuruhusu kujiongeza na kusonga mbele kwa mashambulizi na kuongeza ufanisi kwa timu kwenye maeneo yote ya uwanja na si kukaa tu eneo moja. Ipo hatari kwamba ule utu wa wachezaji huweza kupotea pia kwa sababu wana hisia, wakati mwingine huwa katika hali yar aha wakiwa juu na wakati mwingine huzuni – na haya mambo yapo, hayaepukiki
Takwimu zaweza kuonesha kwamba mshambuliaji fulani hajawa na ufanano au uendelevu katika kazi yake, ambapo wakati mwingine katika nafasi 10 anapata moja tu ya bao. Je, katika hali hiyo kocha asubiri marejeo kwenye ubora wake au achukue hatua gani?
Solskjær alijihakiki katika kusoma wachezaji na kuangalia mwelekeo wa hisia kwenye mechi. Jambo kubwa ni kujiamini na kutelekeza anachokiamini kwenye soka na hayo ndiyo mapinduzi yake. Data sio kila kitu wala dira katika kazi husika, japokuwa si mbaya kuzisoma na kutazama alama za nyakati kama Solskjær alivyoonesha pale Paris, kwani kila mechi ina mudi ya aina yake.
Tuchukulie kwa mfano, ushindi wa Brighton wa 4-2 dhidi ya Tottenham au Liverpool kupigwa 2-0 na Burnley. Katikia mechi zote mbili, timu zilizosonga mbele na kushinda zilitawala mchezo, zilitakiwa ziwe mbele zaidi. Lakini ukitazama mechi nyingine, Crystal Palace walitoka kuwa wamepigwa mabaio 2-0 na kwenda sare na Manchester City, bao la kusawazisha likitokana na kuchanganyikiwa kwa Phil Foden.
Katika soka hakuna kitu cha uhakika kwa asilimia zote. Falsafa ni muhimu kuwa kama kanuni ongozi au elekezi. Soka si tatizo au changamoto inayosubiri kutatuliwa. Kinachoweza kuwa sahihi katika hali moja kinaweza kisifae kabisa katika nyingine.
Aston Villa wamekuwa wakistawi kwa mtindo wao wa mstari wa kuotea, lakini pale Old Trafford uliwagharimu. Wamekuwa hivyo hivyo tangu kipindi cha pili kwenye mechi ya Arsenal.
Wakiwa na mabao 2-0 dhidi ya Man United, kukiwa na kimbunga cha aina yake, hawakuweza tena kuwazuia wapinzani wao na pasi zao, wakaonekana kuchoka.
“Haihusiani na namna ya ufundishaji wa mwalimu tena,” Jürgen Klopp alisemma kabla ya Liverpool kuwashinda Newcastle 4-2.
“Ni kurudi tu katika hali njema na baadaye kukutana, ndivyo ilivyo.” Labda hiyo inaeleza au kufafanua kuhusu nguvu na kujituma pasi na kuchoka katika kazi, kama tukitazama michezo ya Liverpool, kutoka suuhu na Manchester United na kuendelea.
Kwa namna fulani hiyo ni furaha ya soka ya Krismasi. Kwa sababu ya ukosefu wa muda wa matayarisho, kunakosekana udhibiti, hivyo makosa yanaweza kuwa mengi uwanjani na ukosekanaji wa utulivu unaotakiwa ili kupata matokeo mazuri.
Na hii inaonekana kuwagharimu sana Arsenal walioonekana kuchoka, wakiwa wanawategemea kwa kiasi kikubwa Gabriel Martinelli na zaidi sana Bukayo Saka na ukweli umeonekana. Imekuwa ni kawaida sasasa kwa timu hii iliyo chini ya Mikel Arteta kuwa katika hali hiyo katika kipindi kama hicho cha ama Desemba au Januari.
Arteta amekuwa akijaribu kuiweka timu Pamoja kwa kushikana mikono na kuwa na moyo mmoja. Ni wakati sasa kwa mawili kufanya kazi kwa Pamoja vyema; kwa makocha kuweka sawa mchakato wakiwasiisha akili na saikolojia lakini pia hali ya kimwili ikiwasilishwa na moyo. Klopp, akikiri jinsi ukufunzi nachangia kidogo katika kipindi hicho cha mwaka, kumeonakana wazi kwa vitendo uwanjani.
=-=
Comments
Loading…