Kwa Watanzania wengi huenda wasijue thamani ya wataalamu wanaohusika na viungo vya mwanadamu hasa kwa wana michezo wataalamu hao wanaitwa ‘Physiotherapists’.
Huwezi kuwatengansiha baina ya watu wawili, wanamichezo na wataalamu hao ambao wamejikita zaidi katika kuangalia viungo vya mwanadamu wakati vikiwa katika majeraha watu hao wanafahamika kama ‘Physiotherapists’ kama nilivyoanza kueleza hapo juu.
Mara nyingi watalamu hawa wanajiriwa kabisa katika timu mbalimbali wakiwa na lengo moja tu la kuangalia mifupa na viungo vya mwanadamu kwa sehemu ambayo ameajirwa majeraha mengi kwa wachezaji ‘Injury’ huwa inafahamika misuli, magoti, nyama ya paja, kuvunjika mfupa,mabega,kidole kiazi cha mguu, kisigino na vingine ambavyo tukiendelea haviishi kuvitaja.
Barani Afrika ni timu chache sana zinazokuwa na wataalamu kama hawa ambao wanaokoa maisha ya wanakabumbu ktika maendeleo na maisha ya mpira.
Kumekuwa na kukatishwa ndoto za wasakata kabumbu hapa nchini kutokana na kutokuwa na wataalamu wa viungo vya mwanadamu hii ni moja ya njia ya kurudisha nyuma maendeleo ya mchezo wenyewe.
Mifano mingi ipo hapa nchini Tanzania Victor Costa alikuwa anacheza Simba aliumia mguu ila kwakuwa hakukuwa na watu ambao wangeweza kumsaidia hasa wataalamu wa viungo ‘Physiotherapists’ alifeli na kuendelea na soka.
Ali Mayai mchambuzi wa mpira wa miguu naye ana majeruhi hadi hii leo ya goti la mguu wake wa kulia tatizo likiwa ni hilo hilo.
Hivi ni kweli vilabu vingapi vina hawa wataalamu ? hata hao Simba na Yanga kweli wapo hawa watu, ukiangalia utakuwa mtihani mkubwa sana.
Ikiwa kama hao madaktari wa timu wengine hawa taaluma hiyo itawezekana vipi kuwepo mtalaamu wa viungo vya mwanadamu bado mtihani sana soka letu kukua na kufika pale ambapo tunahitaji.
Tovuti hii imemtauta mtaalamu wa viungo na aliwahi kuhudumu timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa taalauma hiyo Gilbert Elias Kingadie.
Kingadie amesema kuwa ‘Physiotherapists’ sio tu muhimu kwa wachezaji bali hata kwa jamii nzima, akisisitiza kuwa hapo zamani wengi hawakuweza kuwatambua kwakuwa mpira haukuwa katika biashara kubwa kama ilivyo hivi sasa.
Hii ndio tatizo kubwa kwa Tanzania kutokuwekeza katika kuwatafuta wataalamu hawa wa viungo vya wanadamu, ila kwa sasa amekiri kuwa wapo na wanaanza kuelewa umuhimu wao.
Amesisita kuwa wanatibia kwa njia ya kawaida bila ya kutumia madawa japo pia hutumika pale inapohitajika.
“Tunatumia mikono yetu kuwatibu watu kabla ya kutumia dawa, hii inaweza ikawa tofauti kubwa kwa sisi na madaktari wa kawaida,”alisema.
“Mara nyingi huwa tunawaeleza wachezaji wanapoumia wanatakiwa watu wa kwanza wawafuate wataalamu hao kabla ya kwenda hospitali,”aliongeza.
Sisi ‘Physiotherapists’ tunaondoa chanzo cha maumivu ila dawa unazuia tu ule ugonjwa hivyo unaweza kuona utofauti,”aliongeza.
Kingadie amewashauri kuwa kila timu inatakiwa wawe na ‘Physiotherapists’ kwani wataweza kupunguza majeruhi wengi pindi wanapoumia wanakuwa wa kwanza kuwaelekeza sehemu sahihi ya kupata tiba.
“Nawashauri viongozi wa timu wawe na wataalamu wa viungo kwani wanakuwa wa kwanza kuwaelezea matatizo yao kama ikiwa waende hospitali au wanaweza kutibiwa kupitia hao wataalamu bila kutumia dawa,”alisema.
Kingadie moja ya wataalamu ambao bado wanatumika sana na wachezaji wa timu nyingi hapa Tanzania ambao wakiumia wanaenda kupata huduma katika kituo chake kilichopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere.
Wakati naenda kumfanyia mahojiano haya niliwaona wachezaji wengi wa timu kubwa wakisubiri huduma yake.
Mtaalamu huyo amesema kuwa tatizo ambalo amekumbana nalo kwa wachezaji wengi wakianza kupata nafuu hawamalizii dozi hivyo bado wanasababisha usugu wanapoumia tena.
Aliwahi kuwashauri viongozi wa Simba kumpeleka India aliyekuwa mhezaji wao wakati huo Haruna Niyonzima juu ya majeraha aliyokuwa nayo, hii kuonesha kuwa kama tatizo linahitaji matibabu zaidi huwa wanatoa ushauri.
Aliwahi pia kumtibia Donald Ngoma na akapata nafuu kabisa pia alimshauri kutoanza mapema mazoezi na aliweza kupona majeraha hayo.
Hiyo ni mifano ila bado wachezaji wengi wa timu mbalimbali hukimbilia kwakwe kwa ajiri ya kupata huduma. Kama ndio hivyo kwanini timu zishindwe kumuajiri mtaalamu wa aina hiyo ili awe karibu na wachezaji wakati wote.
Amewashauri wachezaji kuwa kucheza bila majeraha kunaweza kukuza kipaji chako kukua zaidi ila kama unacheza kwa kujilazimisha wakati unaumwa utarudi nyuma na hutoonesha kiwango chako kamili.
Katika kuwahimiza vijana wanaopenda kujiunga na utaalamu huo waongezeke kwa wingi hakuna taaluma isiyokuwa na kazi hivyo kama kweli unapenda unaweza kufanya na kutimiza ndoto zako.
Nchi nyingi zilizoendelea katika benchi la ufundi kuna watu zaidi ya 25 wakiwa katika taaluma mbalimbali, kuna watu wa saikolojia,wataalumu wa viungo, wa ufundi na mwengine mengi hivyo ni bora timu zetu zifuate yaliyo mazuri ili kupata weldi na maendeleo sahihi ya michezo iende mbele.
Comments
Loading…