in

Klabu EPL zinadeka

Wakati mazoezi ya klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) yakianza leo katika makundi madogo madogo, klabu hizo zinaonekana kudeka kwa kujidai kwamba zipo kwenye hali mbaya kifedha.

Klabu hizo zimekuwa zikitengeneza mamilioni ya pauni kupitia mauzo ya tiketi na mapato mengine, lakini changamoto ya virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu ilipokuja, zimekuwa zikidai kwamba zipo kwenye hali mbaya.

Laiti klabu hizo kubwa 20 zingejua hali ilivyo kwa klabu za madaraja ya chini na zile za wanawake, basi hazingethubutu kulalamika, kwani zenyewe ni kana kwamba zimepulizwa tu wakati hizi nyingine zimetikiswa hasa na kuna zilizo katika hofu ya kufilisika.

Klabu hizo zilipiga kura jana Jumatatu juu ya protokali za kurejea kwenye mazoezi, wakati Ujerumani wao wamesharejea kwenye Ligi Kuu – Bundesliga. Klabu hizo zilifanya mkutano wao kwa njia ya video kama kawaida, kama hadhari dhidi ya virusi vya corona.

Kwa sasa zimebaki mechi 92 miongoni mwa klabu hizo 20 za EPL. Klabu hizo, kupitia kwa viongozi wake, kama Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward, zimekuwa zikilalamika kwamba hali ni mbaya kiuchumi.

Woodward anayeongoza moja ya klabu zenye mapato makubwa zaidi katika EPL, amekuwa akisema kwamba wamepigwa sana na janga la corona, hivyo watu wasitarajie usajili wa mamilioni mengi kiangazi cha mwaka huu kwa sababu hakuna fedha.

Lakini ukweli ni kwamba klabu hizo zina fedha, na hata kama mapato yamepungua kwa kiasi fulani nyingi miongoni mwao zinamilikiiwa na mabilionea ambao fedha kwao si kitu cha tatizo na wengine wamekuwa wakiingiza klabuni mamilioni ya pauni pasipo kuchukua fedha za mapato ya klabu.

Nani hajui utajiri wa Roman Abramovich anayeimiliki Chelsea na jinsi tangu aliponunua akawa anapampu fedha ndani pasipo kuchukua chochote miongoni mwa mapato yake? Vipi kuhusu familia ya Glazers wanaoimiliki Manchester United? Tazama Wamarekani – Fenway Sports Group wanaoimiliki Liverpool walivyochafukwa fedha.

Hapo hatujamzungumzia Mike Ashley wa Newcastle ambaye sasa anataka kubadili biashara kwa kuiuza klabu kwa pauni milioni 300 kwa jamaa wa Saudi Arabia, japokuwa pamekuwapo na utata kwenye kukamilisha dili hilo.

Mabilionea wanaomiliki klabu za EPL wana fursa tele za kupata mikopo ndani na nje ya nchi lakini si kwa klabu ndogo zisizo za ligi huko chini au zile za wanawake. Huko ndiko kuna shida kubwa kifedha na wenye nazo ndio wangetakiwa kuonekana wanadeka.

Ni aibu basi, kwa klabu hizi kubwa, kujidai kwamba zipo katika hatari kubwa wakati kwa miaka zimejilimbikizia mamilioni ya pauni, kujiingiza kwa mbwembwe kwenye usajili wa wachezaji kwa mamilioni ya pauni na tulianza pia kuona karibuni wakipaisha bei za magolikipa na mabeki, jambo ambalo halikuwa hivyo miaka ya nyuma.

Ili kuendelea kuwapo wala EPLhaihitaji kustawi sana, tena inatakiwa kupata janga au changamoto ili iamke, tofauti na ilivyo kwa washindani wao wa Ligue 1 – Ligi Kuu ya Ufaransa, Eredivise – Ligi Kuu ya Uholanzi au Championship – Ligi Daraja la Kwanza hapa England.

Klabu za EPL zina mamilioni benki kwao na wamiliki wanaweza pia kuongeza chochote na kama ni usajili wa ghali, hapana wasiwasi kwamba zinaweza kufanya hata kiangazi cha mwaka huu baada ya ligi kumalizika. Lakini hawataki kusema. Wanadeka.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Tyson anarudi ulingoni

Tanzania Sports

Ndemla ana kipaji, kwanini makocha humweka benchi ?