in , ,

KIPI WAKIFANYE MANCHESTER CITY WASHINDE DHIDI YA LIVERPOOL?

Wiki iliyopita ilikuwa wiki ngumu sana kwa Pep Guardiola baada ya
kupoteza michezo miwili kwa magoli sita (6) jumla, kazi kubwa
waliyonayo leo ni wao kuhakikisha wanaifunga Liverpool kuanzia magoli
4-0 ili wafanikiwe kufuzu kwenda hatua ya nusu fainali ya ligi ya
mabingwa barani ulaya.

Manchester City wanaweza kufunga magoli bila kuruhusu goli?

Hiki kitu ni kigumu sana kwao kwa sababu hata ukiangalia katika mechi
mbili zilizopita ameruhusu magoli sita (6) ameruhusu na timu za aina
gani? Hapa ndipo ugumu wa Manchester City kumaliza mchezo bila
kufungwa leo.

Aina ya timu ambazo amekutana nazo katika mechi mbili zilizopita ni
timu ambazo zinakabia kwa juu (zina press high) ndiyo maana
zilifanikiwa kupata goli dhidi ya Manchester City.

Manchester City inaweza ikaonekana kama timu ambayo haijaruhusu magoli
mengi. Lakini kiurahisia Manchester City aina yao ya uchezaji
huwafanya wasiruhusu kushambuliwa sana. Muda mwingi timu hukaa mbele
ya mpira na hii huwafanya wasiruhusu magoli mengi na kuficha udhaifu
wao unaoonekana wakati wanajizuia.

Manchester City hutengeneza uwazi mkubwa sana wanapokuwa wanajiuzia.
Uwazi ambao husababisha timu pinzani kutumia na kufunga. Timu ambazo
zimefanikiwa kupata goli dhidi ya Manchester City zilitumia uwazi
uliokuwa unatengenezwa na mabeki wa Mnachester City huko nyuma.

Pili, Manchester City inapokabiwa juu mabeki wake hulazimishwa kufanya
makosa ambayo huadhibiwa.

Liverpool ina wachezaji wa mbele ambao hukabia juu kwa kasi, mechi
zote mbili ambazo wamechezaji Anfield dhidi ya Manchester City,
waliwalazimisha mabeki wa Manchester City wafanye makosa binafsi
kutokana na wao kukabia juu.

Hiki ni kitu cha pili ambacho kinatia ugumu kwa Manchester City
kumaliza mechi bila kuruhusu goli.

Kitu cha tatu na cha mwisho, ni safu ya ushambuliaji ya Liverpool
ambayo kwa msimu huu wa ligi ya mabingwa barani ulaya ndiyo safu
ambayo imefunga magoli mengi katika michuano hii ya Ulaya kuzidi timu
zote zinazoshiriki Michuano hii.

Magoli ishirini na nane (28) katika michezo tisa (9) ikiwa ni wastani
wa kufunga magoli matatu (3) katika kila mechi kwenye msimu huu wa
ligi ya mabingwa barani ulaya, hii inatoa mwanga kuwa Liverpool hawezi
kumaliza mechi bila kufunga goli.

 Raheem Sterling na Leroy Sané
Raheem Sterling na Leroy Sané

Ubora wa safu ya Ushambuliaji ya Manchester City unatoa tafasri gani
kwenye hii mechi ya leo?

Kuna tafasri moja inayokuja baada ya kutazama safu ya ushambuliaji ya
Manchester City na safu ya ushambuliaji ya Liverpool. Hizi ndizo safu
Imara za ushambuliaji pale kwenye ligi kuu ya England zilizofunga
magoli mengi.

Hii inatosha kuonesha kabisa timu hizi katika mechi ya leo
zitafungana, na idadi kubwa ya magoli yanaweza kupatikana.

Kipi wakifanye Manchester City ili wavuke?

Kitu cha Muhimu ni Pep Guardiola kujidhatiti kwanza katika eneo la
kujilinda. Leo lazima aende kushambulia lakini anatakiwa kumpa heshima
Liverpool kwa kushambulia kwa tahadhari ili wasiruhusu goli.Safu ya
ulinzi inatakiwa kuwa imara zaidi kwa sababu safu ya ushambuliaji ni
bora na ina uwezo wa kufunga magoli.

Kipi wakifanye Liverpool ili wafanikiwe kupita?

Wakubali kuwa underdog(s) kwenye hii mechi, ukikubali kuwa
underdog(s) unakuwa na uwezo wa kumheshimu mpinzani wako na kuna kuwa
na nidhamu ya matumizi ya kila nafasi wanayotumia pia umakini
kuongezeka ndani yao , umakini ambao utawafanya wawe makini sana
wanapojilinda kutokufanya makosa mengi binafsi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

JOSE MOURINHO ALIVAA AKILI ZA SIR ALEX FERGUSON PALE ETIHAD

Tanzania Sports

BUFFON TAZAMA PICHA YA ZIDANE