Wenyeji Kenya wamefanikiwa kunyakua ubingwa wa Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Harambee Stars walisherehekea vyema miaka 50 ya uhuru wa Kenya kwa kuwafunga Sudan 2-0 kwenye mechi kali iliyochelewa kuanza kutokana na mvua na uwanja wa Nyayo kujaa maji.
Nahodha wa Kenya, Allan Wanga ndiye alifunga mabao yote mawili na kuwapa ubingwa baada ya kuukosa tangu 2002.
Hili ni kombe la kwanza pia kwa Kocha Adel Amrouche tangu alipokabidhiwa timu hiyo Februari mwaka huu.
Wanga ni mchezaji wa AFC Leopards ambayo pamoja na Gor Mahia zimerejea kwenye kilele cha mafanikio ya soka baada ya kutupwa nje kwa miaka mingi.
Timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars walishindwa kupata nafasi ya tatu baada ya kufungwa na Zambia kwa mikwaju ya penati.
Stars walitangulia kufungwa bao ndani ya muda wa kawaida kabla ya kusawazisha lakini zilipokuja changamoto za penati Chipolopolo wakawapopoa kwa penati 6-5. Kipa wao aliokoa penati tatu.
Comments
Loading…