in ,

KARIBU TENA JACK WILSHERE

Takribani miaka miwili imepita bila Jack Wilshere kuwa ndani ya jezi ya Arsenal.

Jezi ya timu ambayo ilimkuza, ikamlea na kumwamini kuwa ipo siku moja
atakuwa mfalme wa timu hii.

Kipaji chake kiliwapa imani mashabiki kuwa ipo siku moja Jack Wilshere
ndiye atakuwa Mr. Arsenal.

Arsene Wenger alikuwa mlevi wa kipaji cha Jack Wilshere , kila
alipokuwa anawaza mawazo yake yalimwaminisha kuwa Jack Wilshere
atakuja kuwa mhimili mkubwa sana ndani ya kikosi chake.

Jambo ambalo lilifanya mashabiki wengi kuwa na shauku ya kuona ni lini
Jack Wilshere kipaji chake kitakomaa na kuanza kuonesha matunda ndani
ya timu.

Sekendu zilizidi kwenda, dakika zilichukua nafasi ya sekunde
kukaribisha saa, masaa ambayo yalitupa nafasi ya miezi kutufikia na
kutupa nafasi ya kuona miaka.

Nyakati zilikuwa zinakimbia, kila mtu akisubiri ni lini Jack Wilshere
atakuwa katika kiwango ambacho kila mtu alikuwa anakiwaza katika
ukubwa .

Kiwango ambacho kiliweza kutanabaishwa na aliyekuwa gwiji wa Barcelona
Xavi Hernandez.

Xavi Hernandez aliwahi kusema isingekuwa majeraha , Jack Wilshere
angekuwa mbali sana katika kiwango chake cha mpira.

Hakika Xavi Hernandez hakuwa amekosea maana hicho ndicho kitu ambacho
kilikuwa kinamwangamiza Jack Wilshere kila uchwao.

Amekuwa mhanga wa kupata Majeraha kila msimu, hakuna msimu ambao
umeisha bila yeye kupata majeraha ya muda mrefu au muda mfupi.

Majeraha ya mara kwa mara kwake limekuwa jambo la kawaida katika
maisha yake ya kila siku ya mpira.

Anatumia muda mrefu akiwa wodini kuuguzwa majeraha anayoyapata kitu
ambacho hakimpi nafasi ya kuendeleza kiwango chake.

Utapata wapi muda wa kucheza na kuionesha dunia ubora wa kiwango chako
wakati muda wako mwingi unaumalizia wodini?

Kipi utakifanya ili miguu yako iweze kudhihirisha thamani yake ilihali
huna nafasi ya kuwa uwanjani muda mrefu ?

Ni ngumu kuendeleza kiwango chako ilihali wewe hupati nafasi ya
kuendeleza kiwango chako.

Hiki ndicho kitu ambacho kinamfanya Jack Wilshere mpaka sasa hajawa
mfalme wa Arsenal.

Ndicho kitu ambacho kinachelewesha yeye kuitwa Mr. Arsenal. Na ndicho
hiki hiki kinachomfanya mpaka sasa siyo nahodha wa timu ya Arsenal.

Anaishi kwenye maisha ambayo hakuyachagua, maisha ambayo Arsene Wenger
hatamani kumuona nayo. Maisha ambayo kila shabiki wa Arsenal
anachukizwa nayo.

Jana baada ya kuingia kwenye mechi ya UEFA EUROPA SUPER LEAGUE, uwanja
ulisimama, kila shabiki alishangilia urejeo wake.

Makofi ya mashabiki wa Arsenal yalikuwa yana maana kubwa sana kwa Jack
Wilshere, nyuso za tabasamu za mashabiki wa Arsenal kila Jack Wilshere
alipokuwa anagusa mpira zilikuwa na maana kubwa sana kwa mashabiki wa
Arsenal.

Maana ambayo ilikuwa na tafasri kuwa walikuwa na mapenzi naye na
kikubwa zaidi imani yao juu yake ilikuwa bado iko katika kiwango cha
juu.

Kila shabiki alikuwa na shauku Jack Wilshere aguse mpira kila wakati,
maana hiyo ndiyo ilikuwa faraja kwao kumuona mfalme wao ajaye akigusa
mpira.

Arsenal-Koln

Ulikuwa ukaribisho mzuri sana kwa Jack Wilshere, ukaribisho ambao
ulikuwa na imani kubwa ndani yake.

Imani ambayo anatakiwa aitumie katika kujijenga upya na kupigania
namba tena ili aweze kupata nafasi, kwa sababu muda huu pale Arsenal
kila kitu kimebadirika.

Ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi cha Arsenal hasahasa katika
eneo lake analocheza ndicho kitu ambacho anatakiwa kukifanyia kazi ili
aweze kufikia katika kiwango kikubwa.

Wote tunamuombea majeraha yasiwe karibu yake ili yampe nafasi ya
kucheza mara nyingi kwa sababu hakuna mtu ambaye hapendi kuona kipaji
cha Jack Wilshere kikaishia njiani.

Kuna kitu ambacho Jack Wilshere anatakiwa kukifanya ili afike katika
kiwango ambacho kila mtu alikuwa anakitamani akifikie kipindi ambacho
yeye alikuwa anachipukia pale Arsenal.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NI WAKATI WA TIMU ZA ENGLAND KUTAWALA UEFA?

Tanzania Sports

KANE, JIVUE SHATI LA SHEARER