in , ,

Kalvin Philips na taswira tata ya Guardiola

Kuondoka kwa Kalvin Philips lilikuwa pigo kwa Leeds United, pengine ni moja ya sababu ya kuyumba kwa timu hiyo…

KILA timu inaposajili mchezaji kuna mambo ya msingi wanayotaka. Baadhi huangalia uwezo wa ndani, wengine huchunguza hadi mambo ya nje ya uwanja ya mchezaji namna anavyoshi na uhusiano wake na wachezaji wengine. Hata hivyo baadhi usajili unaofanywa na makocha au timu unakuwa na utata mwingi kuanzia kiufundi hata amani ya timu.

TANZANIASPORTS hivi karibu ilifanya uchambuzi kuhusu usajili wa klabu ya Yanga waliapoamua kumchukua kiungo mkabaji Jonas Mkude. kiufundi nafasi ya Jonas Mkude inapambana kwanza na kiungo mkabaji mwingine aliyeko benchi, Zawadi Mauya. Yanga wakati wanamsajili Jonas Mkude walikuwa na nyota wengine wanne; Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Zawadi Maua na Yannick Bangala. 

Uongozi wa Yanga uliamua kumuza Yannick Bangala kwenda Azam ili kupisha nafasi ya Jonas Mkude. hadi hivi leo Ligi Kuu imeanza bado kuna mjadala mkubwa juu ya nafasi ya Jonas Mkude kikosini. Pengine kocha anaweza kusema anafanya ‘rotation’ kwa timu ili kuwapa mapumziko wachezaji, lakini hali hiyo haionekani kutokea, labda hapo baadaye.

Wakati ukitafakari Yanga sasa wageukie Manchester City waliopo chini ya kocha Pep Guardiola. Mwaka 2022 Pep Gaurdiola aliingia sokoni kumsajili kiungo wa chuma Kalvin Philips kutoka klabu ya Leeds United. Kalvin Philips mkali wa mtindo wa kucheza ‘murderball’ ya Marcelo Biesla alisajiliwa kikosini hapo huku kukiwa na wachezaji wasiobadilishwa wala kupumzishwa. Kwanza msomaji afahamu kuwa ‘murderball’ ni mtindo wa kucheza mpira muda mrefu bila kupumzika unaotumiwa zaidi na Marcelo Bielsa kwa nia ya kuwajenge pumzika na utimamu wa mwili wachezaji wake. ‘murderball’ inachezwa mazoezini takribani kwa saa tatu hadi nne. 

Tanzania Sports

Naam sasa, mojawapo ya wachezaji wanaocheza nambari 6 ni Rodrigo au jina la maarufu Rodri. Nyota huyu ndiye injini ya timu na ndiye huendesha mipangilio ya timu. Guardiola tangu alipofungwa na Chelsea ya Thomas Tuchel kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa nchini Ureno kwa kosa la kutopanga kiungo mkabaji hakutaka kurudia makosa tena. Siku ya mchezo dhidi ya Chelsea alimpanga Bernando Silva kama kiungo mchezeshaji na kuondoa mchezaji wa kukaba na kuwalinda walinzi. Kuanzia hapo Guardiola aliimaisha safu ya kiungo mkabaji ambapo Rodri ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi za Manchester City kuliko wote. Hata msimu uliopita ulipomalizika wengi walijadili nafasi ya Rodri kuwa anachezeshwa mechi nyingi mno bila kupata mapumziko. Hata hivyo Guardiola katika kikosi chake alikuwa amemsajili Kalvin Philips.

Kuondoka kwa Kalvin Philips lilikuwa pigo kwa Leeds United, pengine ni moja ya sababu ya kuyumba kwa timu hiyo. Maisha ya Kalvin Philips ndani ya Manchester City hayajawa mepesi, kwani Rodri hapumzishwi. Kuanzia mwaka 2022 aliposajiliwa Kalvin Philips hadi leo hii amecheza mechi 12 tu. Msimu mmoja una mechi 38 za Ligi Kuu England. Baada ya hapo kuna mashindano mengine ya FA na Carabao, lakini Kalvi Philips hajapata nafasi ya kutosha. Kwa mfano mechi 38 za EPL ukigawanya kwa mbili maana yake mchezaji anatakiwa kucheza angalau nusu yaani mechi 19.

Kalvin Philips amecheza mechi 12 ikiwa hajafika hata nusu ya mechi za EPL. Hapo hapo kuna mechi za FA au Carabao nako hali ni ngumu. Ukifika hapo swali linaibuka, Pep Guardiola alimsajili nyota huyu ili afanye nini? Kwa sababu Kalvin Philips hajashuka kiwango wala kusema amepotea katika kandanda. Akiwa Leeds United ndiye alikuwa kiungo kiongozi na injini yao. Katika timu ya Taifa, Kalvin Philips na Delcane Rice ndiyo injini ya kikosi cha Gareth Southagate. Hata kwenye Fainali za Kombe la Dunia zilizopita zilianza kuonesha athari mbaya kwa Kalvin Philips kutokana na kuwekwa benchi mara kadhaa kwakuwa hakuwa akicheza mechi nyingi pale Manchester City. 

Katika kuzidisha utata, Pep Guardiola alianza kumtengeneza John Stones kucheza nafasi ya kiungo mkabaji akimsaidia Rodri badala ya mchezaji aliyesajiliwa kwa kazi hiyo, yaani Kalvin Philips. Mara kadhaa Pep Guardiola alipohojiwa na vyombo vya habari alisema nafasi ya Kalvin Philips iko palepale na muda  wake wa kung’ara kikosini ungekuja. Lakini msimu umamalizika na mchezaji kacheza mechi 12, huo ni utata wa aina yake. Si kwamba Kalvin Philips ni mbovu lakini amenyimwa nafasi ya kuwa injini ya timu kwa kuwekwa benchi tu. 

Hapo ndipo unakuja na swali sababu za Pep Guardiola kumsajili Kalvin Philips zilikuwa zipi? Alikuwa na sababu gani kumsajili mchezaji ambaye hakuwa na nia ya kumtumia? Au ni njia ya kuwakomoa makocha wengine, hivyo aliamua kuzuia wasimchukue? Hapo ndipo unarudi hata kwa Yanga juu ya usajili wao wa Jonas Mkude, kasajiliwa ili akae benchi? Sababu kikosi cha Yanga hadi kupenya ni shughuli ngumu.

Lakini kwa Kalvin Philips kikosi cha Manchester City hadi kumbadili John Stones kuwa kiungo maana yake alikuwa na faida ya kukaa kikosini kwa muda mrefu na kuielewa falsafa ya timu. Hata hivyo hakuwa na umahiri kumzidi Kalvin Philips anayejulikana kwa soka la shoka na mchezaji mwenye mapafu ya mbwa kwani huwea kucheza mpira muda mrefu pasipo kuchoka. Ni sababu hiyo ningetamani kumwona Kalvin Philips akiungana na injini mwenzake Declane Rice wakiunda safu kali ya kiungo pale Arsenal. Kama imeandikwa, basi ipo tu. Kalvin Philips ni mwamba kisoka, na hakuna timu ya ‘Top four’ Epla inayoweza kukataa huduma yake. Isipokuwa tu, Pep Guardiola ana utata mwingi sana. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga wameanza walipoishia

Mbappe

Vita kali PSG na Real Madrid