in , , ,

JE UMEFIKA WAKATI WA ARSENE WENGER KUFUNGA VIRAGO?

Born: October 22, 1949 (age 68), Strasbourg, France Nationality: French Height: 6' 3" (1.91m) Parents: Alphonse Wenger, Louise Wenger Children: LĂ©a Wenger

 

 

Vyombo vya habari Uingereza vimeanza tena kuuliza kwa nguvu mustakabali wa Arsene Wenger baada ya kuzidiwa nguvu na Barcelona, Manchester United na Swansea City ndani ya juma moja. Haijawahi kutokea Arsenal ikashindwa mechi tatu mfululizo toka mwaka 2010. Mmoja wa wazungumzaji wa TV waliotathmini sakata la Man Uinted, Jumapili iliyopita, kocha na mchezaji wa zamani wa Rangers na Liverpool- Graeme Souness aliwararua rarua Arsenal kwa kusema walicheza kama wanafanya utani. Alirejea hoja inayorudiwa kila mwaka kwamba Arsenal huanza ligi yao vizuri, lakini unapofika wakati muhimu kama huu –Februari na Machi “wanatupilia bahati yao shimoni”….

Macho na masikio lakini hayaiangalii wachezaji bali , kocha Arsene Wenger.

Jumatatu hii moja ya magazeti makuu ya Uingereza yalichapisha kura ya maoni kwa wasomaji kuulizia je wangapi wanakubali wakati wake kujiuzulu kabisa umefika?

Mwezi Septemba, Arsene Wenger (66) atatimiza miaka ishirini, akiwa Arsenal. Bw Wenger si kocha wa kwanza kukaa katika klabu muda mrefu. Mwenzake, Alex Ferguson naye alitamba kiti cha ukocha wa Man United toka 1986 hadi 2013. Ingawa wote walichangia sana kubadili klabu hizi mbili, wanatofautiana.

Pale ambapo Arsene Wenger aliiweka Arsenal juu kpindi walivyoitwa “The Invincibles” (1999-2004) walikuwa na wachezaji wakubwa wakubwa kama David Seaman (kipa wa England), walinzi mashuhuri – Tony Adams, Kolo Toure (kaka yake Yaya), Ashley Cole (tunayemjua kama mchezaji wa Chelsea), Martin Keown, Patrick Vieira, nahodha wa timu ya Ufaransa- iliyoshinda kombe la dunia la 1998- washambuliaji Dennis Bergkamp (Uholanzi), Sol Campbell, Robert Pires, Thiery Henry nk….

Arsenal ilitetemesha. Lakini kuanzia 2005 hawajafikia tena kilele hicho.

Mwenzake, Fergusson aliendeleza ujabali wa Machester kwa kipindi kirefu cha 1990 hadi alipostaafu 2013. Kupitia usimamizi wake wachezaji mbalimbali walichezea na kuiweka Manchester United juu : Eric Cantona, Paul Ince, Cristiano Ronaldo, David Beckham, Paul Scholes, Ryan Giggs, Roy Keane, nk. Paul Ince, alikuwa mchezaji wa kwanza mweusi kushika nafasi ya unahodha wa taifa la England (1992-2000).

Ingawa Arsene Wenger hamfikii Fergusson, bado kazi aliyoifanya Arsenal ni zaidi ya vikombe.

Mashabiki wakiwakilisha ujumbe unaomtaka AW atoke...
Mashabiki wakiwakilisha ujumbe unaomtaka AW atoke…

Toka aje Uingereza 1996, Bwana Wenger amesaidia sana kubadili mpira na afya ya wachezaji. Alipoingia alifuta tabia ya wachezaji kulewa ovyo, kulala vibaya na kula bila mpangilio. Kinyume na makocha kama Jose Mourinho- asiyejali sana wachezaji chipukizi- Wenger amejenga wachezaji wachanga kuwa imara kama Thiery Henry na Theo Walcott.

Wenger alisomea masuala ya uchumi Ufaransa –chuo mashuhuri cha Strassbourg- na alipofika Uingereza mwaka 1996 – na baada ya kushinda vikombe kadhaa alianza kuitwa “Profesa”- kutokana na ushindi wa Arsenal. Hata alipoanza kuzidiwa – kipindi cha 2005 hadi 2013- ambapo Arsenal hawakuambulia chochote, washabiki walimremba kwa maneno : “Arsene Knows” yaani Arsene anajua la kufanya. Wamiliki wa klabu, nao, wamekuwa na subira kubwa kwake.

Lakini kila jambo lina mwisho.

Ligi ya 2015 na 2016 iko bado mikononi mwa Arsenal. Manchester United imekuwa na migogoro ya makocha toka Mzee Fergusson alipostaafu. Chelsea wako chini sana, Manchester City hawaeleweki, mara washinde mara washindwe. Timu zinazokuja kasi ni Tottenham Hotspurs na Leicester City. Kwa wahakiki wengi huu ni mwaka wa Arsenal. Na ndiyo maana ashinde au asishinde bwana Arsene Wenger anaombwa ajiuzulu. Na je akiondoka, Arsenal haitadidimia katika matope yaliyowakuta Chelsea na Man United?

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Kilio Arsenal, Spurs, Man City

Tanzania Sports

AZAM, YANGA ZANG’ANG’ANIANA TAIFA