Menu
in , ,

Je Hemed Morocco atavunja rekodi ya Maximo?

Taifa Stars

Wakati Marcio Maximo alipoajiriwa kuwa kocha wa timu ya Taifa Stars nchini Tanzania haikuwahi kushiriki mashindano ya makubwa barani Afrika. Lakini maarifa,ushirikiano aliopewa toka serikalini na shirikisho la soka TFF na mashabiki pamoja na wadau ilimwezesha kuipaisha timu hiyo hadi kufuzu mashindano ya CHAN mwaka 2009. 

Mojawapo ya matukio ya kukumbukwa ni pale Tanzania ilipowahi kuichapa mabao 3-1 Morocco katika moja ya mechi zilizoongozwa na Marcio Maximo, na kwamba nchi kama Sudan, Uganda, Zambia, Burkina Faso zilikuwa za kujipigia tu. Mfano Burkina Faso ilipigwa nyumbani kwao kwa bao la Erasto Nyoni na kuigeza Tanzania kuwa gumzo kwenye mchezo wa soka. Mjadala mkubwa ulikuwa umetawala katika vyombo vya habari kuhusiana na kupanda kwa kasi kwa soka la Tanzania kipindi cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete. 

Hemed Morocco, Kocha mkuu Taifa Stars
Hemed Morocco, Kocha mkuu Taifa Stars

Wengi wa wachambuzi barani Afrika walimtazama Kikwete kama siri ya ushindi wa Tanzania katika mechi mbalimbali. Maximo aliongoza Taifa Stars mwaka 2009 ikiwa na kundi dogo la wachezaji na lenye maarifa ya kawaida. Alichokifanya ni kuhakikisha anahamasisha wadau na mashabiki kuipenda Taifa Stars, kila siku alikuwa anakutana na mashabiki mbalimbali kupiga gumzo na walimfanya kuwa rafiki yao. utawala wa kocha Marcio Maximo ulikuwa na hekaheka nyingi za kuwavutia mashabiki kuipenda na kuichangia Taifa Stars. 

Ni kipindi hicho maelfu ya watanzania walikuwa na imani kuwa timu yetu inaweza kufanya maajabu katika soka. Tangu kufuzu fainali za CHAN za huko Ivory Coasr mwaka 2009 Tanzania imeandika historia nyingi hadi sasa. kwanza imeshiriki AFCON tatu kuliko ilivyotarajiwa. Uelewa wa mchezo wa soka miongoni mwa mashabiki uliongezeka tangu ujio wa Maximo. 

Mwenyeji wa CHAN

Kutoka kuwa mshiriki kwenye mashindano ya AFCON na CHAN katika nchi zingine, hatimaye Tanzania inashuhudia kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kuanzia mwaka 2025. Mataifa mbalimbali yaliyofuzu yanakuja Tanzania kwa ajili ya kushiriki mashindano ya CHAN. 

Sasa Tanzania ni mwenyeji wa mashindano hayo ambayo amefuzu moja kwa moja sambamba na Kenya, na Uganda ambao ni wenyeji wenza. Kuwa mwenyeji pekee kunatona na hatua znuri ya kisoka iliyopo kwa Tanzania. Ni ujumbe kuwa soka linapewa nafasi, pamoja na miundombinu inayoweza kuwapa naafsi ya kuwa mwenyeji pamoja na uwezo wa kulipia ada ya kuwa timu mwenyeji. Katika ngazi ya vilabu Tanzania aimefanya vizuri kuliko wenyeji wenza, Kenya na Uganda, kuwa moja ya kivutio muhimu cha kushuhudia fainali hizi kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Rekodi muhimu

Chini ya Marcio Maximo kwenye mashindano ya CHAN haikuweza kuvuka hatua ya makundi. Halikuwa jambo baya wakati huo kwa sababu ndiyo kwanza ilikuwa inaanza kuonesha makeke yake kwenye ulimwengu wa soka la kimataifa. Lakini fainali za CHAN mwaka huu zinafanyika nyumbani jijini Dar Es Salaam, ambapo kocha mkuu Hemed Suleiman ‘Morocco’ ana kibarua cha kuhakikisha anavunja na kuweka rekodi yake. 

Taifa Stars inatakiwa kupiga hatua kwenda mbele zaidi kwani haitakuwa na sababu nyingine ya kushindwa. Ikiwa inaungwa mkono na mashabiki wa nyumbani, Taifa Stars itakuwa na kila sababu ya kulisaka kombe hilo. Hali ya unyumbani si kwa Dar Es Salaam pekee, hata kama italazimika kucheza fainali nchini Kenya bado itakuwa sehemu nzuri na yenye kupata sapoti ya mashabiki. Kwa maana hiyo ni timu ya Taifa inatakiwa kujiweka katika amzingira mazuri kuelekea fainali za AFCON.

Goli la mama

Hemed Morocco anaingia kwenye mashindano ya CHAN akiwa na vijana wake wakitambua kuhusu ‘goli la mama’. Hili ni goli linalolipiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Rais wa Tanzania amekuwa akilipa mamilioni ya fedha kwa kila goli linalofungwa kwenye mashindano ya Kimataifa. Klabu za Simba na Yanga zimekuwa wanufaika kwa ‘goli la mama’ kwani kila walipofunga na kushinda katika mashindano ya CAF kupitia Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho. 

Fedha hizo zimekuwa na mchango wa kuibua hamasa ili kupata matokeo chanya na kuzisaidia timu hizo kusonga mbele katika mashindano ya CAF. Kwa kuzingatia hilo goli la mama’ limerudi kwenye mashindano ya CHAN. Hivyo bsi vijana wa Hemed Morocco wanatakiwa kuzifuatilia hizi fedha kwa kufunga mabao ya kutosha kwenye mashindano haya na kuivusha Taifa Stars hatua inayofuata. Kadiri wanavyosonga mbele kwenye mashindano haya ndivyo fedha za ‘goli la mama’ zinavyozidi kuongezeka. 

Benchi la ufundi AFCON

Kwa msingi huo kocha Hemed Morocco ana kazi ya kuthibitisha kuwa anastahili kuongoza Taifa Stars kwenye mashindano ya AFCON mwaka 2027. Mafanikio yake kwenye mashindano ya CHAN yanaweza kumbeba hadi kuwa bidhaa adimu kuelekea na wakati wa michuano ya AFCON. Hili litakuwa pamoja na benchi zima la ufundi kupewa sapoti ya hali na mali. Hemed Morocco bila shaka anafahamu kuelekea mashindano ya AFCON anatakiwa kufanya vizuri sasa kwenye fainali za CHAN. Endapo Taifa Stars itapepesuka kwenye mashindano haya basi kutakuwa na kila sababu ya kuondolewa benchini. Lakini pia kibarua chake cha kuvuka hatua ya makundi kinaongozwa na presha kutoka kwa Marcio Maximo, ambaye hakuvuka makundi na hivyo kocha wa sasa anatakiwa kupandisha rekodi kwa kusonga mbele zaidi ya hatua ya makundi.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version