in , , ,

Ivory Coast watolewa kiutata

*Italia nao wapigwa na Uruguay
*Suarez adaiwa kung’ata tena
*Colombia wawachakaza Japan

Huku kukiwa na taarifa za Luis Suarez kurudia kitendo cha kung’ata wachezaji wa timu pinzani, pamekuwa na matokeo ya kushangaza katika hatua mechi za makundi.

Ugiriki waliwatoa Ivory Coast kwa penati tata ya dakika ya 90 baada ya kuwa sare ya 1-1. Penati ilifungwa na Georgios Samaras baada ya kudaiwa kuchezewa vibaya na Giovanni Sio.

Ugiriki ndio walianza kupata bao kupitia kwa 
Andreas Samaris kutokana na makosa ya kiulinzi ya beki Cheick Tiote.

Hata hivyo, Ivory Coast walirejesha matumaini ya kusonga mbele pale Wilfried Bony aliposawazisha bada ya kupata pasi ya Gervinho.

Penati iliyotolewa ilionekana kama haikustahili kwa sababu Sio hakucheza rafu mbaya na ni kana kwamba Samaras alipiga mpira na Sio kisha akaanguka.

Baada tu ya matokeo hayo, kocha wa Ivory Coast alitangaza kujiuzulu nafasi yake. Ugiriki sasa watakutana na Costa Rica kwenye hatua inayofuata ya mtoano.

URUGUAY WAWATOA ITALIA
20140625-093704-34624946.jpg
Uruguay wamefanikiwa kusonga mbele kwa kuwatoa Italia katika mechi ngumu na iliyokuwa muhimu kwa timu zote mbili.
Hata hivyo, mechi hiyo ilimalizika kwa utata kwamba mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Luis Suarez alimng’ata Giorgio Chielini.

Kitendo hicho kilitokea dakika moja tu kabla ya 
Diego Godin kufunga bao pekee ambapo pia ilishuhudiwa kiungo wa Italia, Claudio Marchisio akipewa kadi nyekundu kwa mchezo wa rafu dhidi ya Egidio Arevalo.

Uruguay watakabiliana na Colombia katika Uwanja wa Maracana Jumamosi hii katika mtoano. Italia walitoka uwanjani kwa hasira, na kocha wao, Cesare Prandelli alisema kabla ulikuwa mchezo muhimu zaidi katika muda wote wa tasnia yake na baada ya kushindwa alitangaza kujiuzulu.

Fifa wametangaza kuendesha uchunguzi kubaini iwapo Suarez kweli alimng’ata Chielini. Suarez alipata kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic na kupewa adhabu kali ya kukosa mechi kadhaa.

ENGLAND WAMALIZA BILA USHINDI

20140616-200911-72551836.jpg
England wanarejea nyumbani pasipo ushindi wowote baada ya kwenda suluhu na Costa Rica katika mechi yao ya tatu na ya mwisho.
England walitolewa baada ya kupoteza mechi ya mwisho na Italia kufungwa na Costa Rica, ikiwa ni mara ya kwanza wamefanya vibaya zaidi katika zaidi ya miongo mitatu.

Kocha Roy Hodgson alishasema kwamba hatajiuzulu na pia chama cha soka nchini mwake kinamuunga mkono aendelee kuandaa kikosi kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.

COLOMBIA WAWACHAKAZA JAPAN20140623-075601-28561939.jpg

Colombia wamemaliza mechi zao tatu za makundi wakiwa nafasi ya kwanza baada ya kuwachakaza Japan 4-1.

Japan walihitaji ushindi ili wawe na nafasi ya kusonga mbele lakini walianza kufungwa mapema kwa penati ya Juan Cuadrado kutokana na Yasuyuki Konno kumchezea vibaya Adrian Ramos.

Shinji Okazaki aliwasawazishia Japan kwa mpira wa kichwa kabla ya Jackson Martinez kupiga bao la pili na la tatu kwa Colombia.
James Rodriguez alipachika bao la nne na kumaliza ubishi wa Japan ambao wamefungasha virago kurudi 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Brazil wavuka

Suarez kikaangoni Fifa