in , , ,

Italia kupima wanasoka

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeshatoa kibali kwa mataifa kujiamulia jinsi ya kumaliza ligi zao

Shirikisho la Soka la Italia linatumaini kuanza kuwapima wanasoka wake wote mwezi ujao kabla ya kuanza tena mechi za msimu wa 2019/2020.

Italia ni moja ya nchi zilizoathirika zaidi kwa maradhi ya homa kali ya mapafu yanayosababishwa na kusambaa kwa virusi vya corona, ikipoteza maelfu ya watu kwa vifo, has wachezaji.

Hali hiyo ilisababisha kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa Ligi Kuu ya Italia – Serie A lakini sasa makali ya ugonjwa yameanza kupungua, hivyo kutoa matumaini kwamba ulimwengu wa soka utaanza tena kufurahia ligi hiyo, ikiwa ni moja ya zile tano maarufu zaidi duniani.

Wakati bado likitafakari iwapo ligi itaanza na washabiki kuhudhuria kuendana na serikali itakavyokuwa imeona, shirikisho hilo linasema kwamba iwe iwavyo, hadi mwezi ujao litaanza kuwapima wachezaji ili kama idadi yao kubwa hawajaathirika, ligi ipangwe kuanza tena.

Viwanja vimekuwa vitupu kama ilivyo kwa mitaa yote na makanisa pia, ambapo Makao Makuu ya Kanisa Katoliki duniani yakiwa Vatican huko Italia, Pasaka imekwenda kwa ukimya, maaskofu na mapadre wakiongoza peke yao na watu kufuatilia mitandaoni.

Ligi hiyo ilisitishwa tangu Machi 9 kwa sababu ya janga hilo. Zimebaki raundi 12 kukamilisha ligi hiyo. Rais wa Shirikisho, Gabriele Gravina, alisema kwamba bado hawajapanga tarehe kamili kwa zoezi hilo, lakini anasema hali inaelekea kuwa nzuri na watajitahidi kuhakikisha kwamba msimu unakamilishwa.

“Hivi karibuni kutakuwapo mkutano. Tutaweka mipango ya kuanza tena ligi, tutawasiliana na wadau wote lakini kabla ya kuannza lazima wachezaji na maofisa wa klabu wanaohusika kuwa benchi wapimwe,’ anasema Gravina.

Anaongeza kwamba baada ya kupima na kukuta wachezaji wapo timamu kiafya, yataanza mazoezi kwa ajili ya kuwaweka sawa kisha ndipo mashindano yatarudia. Kuna uwezekano kwa ligi hiyo kuchezwa hadi wakati wa kiangazi.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeshatoa kibali kwa mataifa kujiamulia jinsi ya kumaliza ligi zao, likisogeza mbele muda wa msimu na pia muda wa kuanza kwa msimu ujao wa 2020/2021.

Vivyo hivyo muda wa usajili utasogezwa mbele kama ambavyo limeshasema mikataba ya wachezaji iliyokuwa ikimalizika mwishoni mwa Juni kwa maana ya haki zao katika malipo, imesogezwa mbele pia.

Juventus ndio wanaoongoza kwenye msimamo wa Serie A, lakini ikiwa ni alama moja tu juu ya Lazio na alama nane juu ya Inter Milan. Rais wa Brescia, Massimo Cellino, ambaye klabu yake wapo chini kabisa kwenye msimamo wa ligi, anasema yupo tayari kuachana na mechi zilizobaki za klabu hiyo msimu utakapoanza.

Wiki iliyopita, timu za Ujerumani zilikuwa za kwanza katika ligi kubwa zaidi duniani kurejea kwenye mazoezi. Ujerumani hawakupigwa sana na virusi hivyo. England bado hawajapanga tarehe ya kuanza, kwa sasa wakiwa kwenye mipango ya fedha zaidi ili kuwafidia wafanyakazi wasiokuwa wachezaji.

Hispania, Ufaransa bado wametulia kusubiri makali ya virusi kumalizika. Hispania nao walikuwa katika hali mbaya, ambapo Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alimpoteza mama yake kwa homa hiyo kali ya mapafu, Covid-19

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Umwamba EPL, BT na Sky

Tanzania Sports

Mabosi Arsenal wajitolea