in , , ,

Huyu ndiyo kiungo mzawa mkabaji anayekosekana pale Yanga

Klabu ya Yanga, kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakihaha kupata kiungo mkabaji bora ambaye mwenye uwezo wa kuilinda timu vizuri pindi wanapo shambuliwa hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Tangu kuondoka kwa Athumani Idd Chuji na Frank Domayo ndani ya Yanga, wameshapita viungo wengi ambao wameshindwa kufikia hata nusu ya ubora wa viungo hao, wachezaji kama Twite, Makapu, Pato Ngonyani, Kelvin Yondani wamejaribu kucheza kwenye eneo hili bila mafanikio yeyote.

Mzambia Justin Zulu naye ameonekana hawezi kutatua tatizo la kiungo mkabaji baada ya kiwango chake kutowavutia wengi hivyo klabu imefikiria kuachana nae mwishoni mwa msimu na kusajili nyota mwingine mwenye uwezo mkubwa kwenye nafasi hiyo
Goal inakuletea aina ya kiungo mzawa mkabaji anayekosekana ndani ya klabu ya Yanga.

HIMID MAO
Ndiye kiungo bora mkabaji kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara, Himid Mao ni mzuri kwenye kulinda safu yake ya ulinzi vizuri pindi inaposhambuliwa, amekuwa akifanya kazi kubwa uwanjani ya kupokonya mipira muda wote wa mchezo bila kuchoka
Akitua ndani ya Jangwani ataleta uwiano mzuri kikosini na kuwafanya kina Kamusoko kuwa huru kushambulia muda wote

JONAS MKUDE
Kiungo huyo wa Simba na timu ya taifa stars anaweza kutatua tatizo la kiungo mkabaji ndani ya Yanga kama wakifanikiwa kuipata saini yake, ni hodari kwenye kuituliza timu na kuziba njia za timu pinzani halikadhalika ni hodari kwa kupiga pasi sahihi fupi na ndefu, Mkude ni aina ya mchezaji anaye itajika Yanga kwa sasa kwa sababu ni kiungo anayetimiza majukumu yake vizuri kwenye eneo la kati.

KENNY ALLY
Hakuna ubishi, Keny Ally ni aina ya kiungo mkabaji ambao klabu kubwa zote zinapenda kuwa naye msimu ujao wa Ligi Kuu. Kwa muda sasa Yanga wamekuwa wakiuliza bei yake kwa Mbeya City.
Uhodari wake wa kutibua mipango ya wapinzani na uwezo mkubwa wa kufunga kwa mashuti ya mbali kumemfanya kuwa mmoja wa viungo watatu bora kwenye eneo la ulinzi.

FRANK DOMAYO
Alifanya kazi nzuri ndani ya Yanga kabla ajatimkia kwa waoka mikate wa Azam, tangu kuondoka kwake Jangwani kumeifanya klabu hiyo kuyumba kwenye eneo hilo, Yanga bado wana nafasi ya kumrudisha Domayo kwani bado uwezo wake haujapote.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Wenger anabaki Arsenal

Tanzania Sports

ANAYEMNG’ATA SIKIO AJIB ASHIKE NA KIBOKO, BAADA YA MACHWEO NI GIZA.