Baada ya kukaa miaka 22 katika klabu ya Arsenal, kocha Arsene Wenger
leo kupitia ntandao wa klabu ya Arsenal katangaza rasmi kuwa mwishoni
mwa msimu huu hatokuwa kocha wa Arsenal tena.
Arsene Wenger alichaguliwa kuwa kocha wa Arsenal tarehe 1 October
mwaka 1996, ndiye kocha aliyedumu muda mrefu katika ligi kuu ya
England kwa sasa.
Akiwa ameiongoza Arsenal katika michezo 823 akishinda michezo 473 huku
akichukua kombe la ligi kuu ya England mara tatu na kombe la FA mara
7.
Msimu wa mwaka 2003/2004 aliiongoza Arsenal kuchukua ubingwa wa ligi
kuu bila kupoteza hata mchezo mmoja ni mwaka wa “Invincible” kwa
Arsenal na alifanikiwa kwenda michezo 49 bila kufungwa.
Msimu wa mwaka 2005/2006 alifanikiwa kuifikisha Arsenal katika fainali
ya kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo alipoteza dhidi ya
Barcelona kwa magoli 2-1.
Baada ya hapo walihama uwanja wa Highbury na kwenda katika uwanja wa
Emirates, ndipo hapo maisha ya mateso yalipoanza.
Tangu mwaka 2006 kombe pekee ambalo Arsenal wamechukua ni kombe la FA
Cup ambalo ndilo kombe ambalo Arsene Wenger kalichukua mara nyingi
kuzidi kocha yoyote.
Vipigo vya aibu vilikuwa vinamuandama baada ya hapo, kufungwa 8-2 na
Manchester United kutolewa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya
kwa jumla ya magoli 10-2 na Bayern Munich.
Michuano ambayo tangu aje Arsenal kashindwa kufuzu mara moja tu, baada
ya msimu jana kumaliza nafasi ya tano (5) , nafasi ambayo ilimpa
nafasi ya kushiriki kombe la UEFA EUROPA League ambapo mpaka sasa yupo
katika hatua ya nusu fainali na atakutana na Atletico Madrid.
Stan Kroenke amekiri kuwa uamuzi aliouchukua Arsene Wenger ni uamuzi
mgumu sana na anapitia kipindi kigumu zaidi.
Kuna majina kadhaa yanatajwa kuja kuchukua nafasi ya Arsene Wenger,
majina hayo ni Leorndo Jardim kocha wa Monaco wa sasa, Maximilliano
Allegri kocha wa Juventus lakini kuna habari za ndani zinadai Arsene
Wenger kampendekeza aliyewahi kuwa nahodha wake Patrick Viera kuchukua
nafasi yake KANG’OKA ARSENAL.