in , , ,

Guardiola: Nakuja England

Pep Guardiola

Kocha wa Bayern Munich, Josep ‘Pep’ Guardiola sasa ametamka bayana
kwamba anakuja kufanya kazi ya ukocha nchini England.

Pep (44)ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona anayemaliza mkataba
wake Allianz Arena mwishoni mwa msimu huu, amesema alikuwa na tama ya
kubadili jiji tena ndiyo maana akaamua kutoingia mkataba mpya.

Hakusema anahamia klabu gani, lakini inajulikana kwamba amekuwa
akihusishwa na Manchester City na Manchester United ambao makocha wao
hawaonekani kwenda na kasi wanayotaka wamiliki; Chelsea waliomtimua
Jose Mourinho na kumweka Guus Hiddink kocha wa mpito lakini pia
Arsenal, baadhi wakidhani huenda Arsene Wenger anaweza kuamua
kustaafu.

“Nataka kupata uzoefu wa jiji jipya na nataka kufanya kazi England.
Nina ofa kadhaa England lakini sijasaini chochote bado. Ninayo fursa
ya kufanya kazi England. Nadhani nipo katika umri sahihi na nahisi
kwamba ni muda mwafaka kwangu kuja huko. Hiyo ndiyo sababu nimechukua
uamuzi huu,” akasema Mhispania huyo.

Mtendaji Mkuu wa Munich, Karl-Heinz Rummenigge, hata hivyo, anaamini
kwamba tayari Guardiola ameshaamua klabu ya kwenda na Mjerumani huyo
alisema alijua tangu awali kwamba Guardiola hangesaini mkataba mpya.

Guardiola alizaliwa Januari 18 huko Katalunya, akaanzia soka ya utoto
Barcelona akiwa kiungo mkabaji, hadi alipopanda kikosi cha wakubwa
1990 kisha akaenda Bresica, Roma, Al-Ahli na Dorados kati ya 2001 na
2006 alipostaafu. Alichezea pia Timu ya Taifa ya Hispania tangu 1991
kwa wadogo hadi 2001 na ya Katalunya kati ya 1995 na 2005.

Kazi ya ukocha alianzia Barcelona ‘B’ 2007 kabla ya kupandishwa hadi
Barcelona 2008 akakaa kwa mafanikio makubwa hadi 2012 alipoamua
kupumzika kwa mwaka mmoja ajinoe upya na aliporejea 2013 akawa na
Bayern Munich.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

TETESI ZA USAJILI JANUARI 2016

Tanzania Sports

NI Mbwana Samatta