Msimu wa mwaka 2023/2024 umeisha kwa klabu ya soka ya Yanga kutawazwa kuwa ni mabingwa wa ligi kuu ya soka ya nchini Tanzania. Ubingwa huo umezidi kuitangaza klabu hiyo ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Kwa sasa klabu ya Yanga ina mashabiki mpaka Afrika Kusini na hiyo ni baada ya kuonyesha mechi ya ushindani sana dhidi ya wababe wa soka wa taifa hilo klabu ya Mamelodi Sundowns katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa ya afrika. Msimu uliotangulia halikadhalika klabu ya Yanga ilifika katika hatua ya fainali ya mashindano ya shirikisho la soka la barani Afrika.
Yanga ya msimu ulioisha ilikuwa ni klabu iliyojaa wachezaji wa hadhi ya kimataifa yaani wachezaji ambao walikuwa wanacheza katika timu za taifa na pia walishiriki katika mashindano ya AFCON kwa kuwakilisha mataifa yao. Wachezaji kama Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki, Bakari Mwamnyeto na wengineo. Uwepo wa wachezji hao ulikifanya kikosi kiwe ni kikosi imara sana.
Inafahamika wazi kwamba katika klabu ya Real Madrid ilipochukuliwa uraisi wa klabu na Florentino Perez aliamua kuleta kauli mbiu mpya ambayo aliita ‘Galacticos’ ambayo katika kauli hiyo aliamua kuanza kusajili wachezaji wenye majina makubwa ambao walikuwa ndio nembo ya soka katika mataifa mbalimbali duniani. Aliwasajili wachezaji kama vile Zinedine Yazid Zidane kutoka Ufaransa, Michael Owen kutoka England, Ronaldo luiz Nazario kutoka Brazil, David Beckham kutoka England na wengineo. Hatua hii ilifanya klabu ya Real Madrid izidi kuongeza mashabiki katika mataifa mengi na kuifanya ijenge ufalme wake katika soka la Uhispania na dunia kwa ujumla. Nembo ya klabu ilikuwa sana na pia mapato ya klabu yaliongezeka sana kwani bidhaa za klabu zilinunuliwa kwa wingi sana.
Raisi wa sasa wa klabu ya Yanga alipochukua madaraka naye halikadhalika alianza kwa kutengeneza Yanga ya kimataifa kwani alianza kuleta wachezaji wa daraja kubwa sana katika bara la Afrika. Alipomleta Stephane Aziz Ki aliushitua ulimwengu wa soka barani Afrika kwani mashabiki wengi hawakuamini kama mchezaji huyo mkubwa kutoka Burkina Faso anaweza kuamua kuja kucheza nchi ya Tanzania kwani wengi waliona kama klabu ya Yanga haina uwezo wa kifedha wa kumsajili mchezaji huyo. Uraisi wa Hersi umepata mafanikio makubwa sana katika klabu ndani ya mda mfupi kwani katika kipindi hicho ndipo klabu imeingia katika hatua ya fainali ya mashindano ya shirikisho la soka barani Africa na pia ikaingia katika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa katika msimu uliofuatia.
Mashabiki wa klabu ya Yanga walishaonjeshwa ladha ya GALACTICOS wa kiafrika na wameletewa wachezaji mbalimbali kama vile lazarous Kambole, Gael Bigirimana na wengineo ambao walikuwa ni wachezaji wa daraja la juu. Licha ya kwamba baadhi ya Galacticos hawakufanya vizuri lakini baadhi yao wamefanya vizuri sana na kuonyesha kwa mashabiki kwamba uongozi wa klabu hiyo haukufanya maakosa pindi ilipoamua kuwasajili tena kwa thamani kubwa sana.
Msimu umeisha na katika nyakati ambazo mashabiki wanasubiria kuanza kwamsimu mpya kumeanza tetesi za kuhitajiwa mastaa mbalimbali katika klabu hiyo. Tetesi hizo zimekuwa zinatengenezwa na waandishi wa habari za michezo nchini Tanzania. Washabiki hawana wasiwasi tena kwamba usajili utakaofanywa utakuwa mkubwa sana na wataletwa wachezaji wa kimataifa ila shauku yao ni kujua ni nani na nani ambao watakaoletwa klabuni hapo.
Wakati mashabiki hawajakaa sawa zilianza tetesi kwamba klabu ya Yanga ina mpango wa kumsajili mchezaji mahiri wa klabu ya Simba Clatous Chota Chama ambaye anatokea taia jirani la Zambia. Chama ni mchezaji ambaye ameichezea klabu ya Simba kwa mafanikio makubwa sana. Huku watu wakiwa hawana majibu zikazuka tetesi nyingine kwamba klabu ya Yanga imeshamalizana na mchambuliaji hatari wa kutokea taifa la Zimbabwe ambaye ni Prince Dube. Dube kwa sasa bado ana mkataba na klabu ya Azam. Dube kwa misimu ambayo alicheza ligi kuu ya Tanzania ameonyesha kwamba ni mojawapo ya washambuliaji hatari sana na tena ambao wana uwezo wa hali ya juu sana katika kufunga magoli.
Mpaka naingia mtamboni kurusha Makala hii Clatous Chama ameshasajiliwa kunako klabu ya Yanga. Kama hao wachezaji wengine wanaotajwa kutakiwa Jangawani wakifika Jangwani basi mashabiki wa Jangwani wana hamu kubwa sana ya kuona muunganiko wa uwanjani katika Aziz Ki, Chama na Dube na kama muunganiko huo utawezekana basi itakuwa ni Galacticos mpya katika ukanda huu wa Afrika mashariki. Ni wazi kama usajili huo utawezekana basi suala la ufungaji magoli katika klabu hiyo hautakuwa tena wa Aziz Ki peke yake bali utakuwa unabebwa tena na wachezaji hao wapya ambao nao kama watasajiliwa basi ukame wa mabao utaondoka kabisa.
Kiujumla kila wachezaji wapya wanaposajiliwa basi kuna wachezaji lazima ima watauzwa ama kuondoka wenyewe.hilo nalo latarajiwa kutokea katika viunga vya mtaa wa Jangwani na tayari minong’ono imeanza tayari kwamba wachezaji kama Denis Nkane, Kenedy Musonda na wengineo wana uwezekano wa kuondoka
Comments
Loading…