Ni mambo yanayochangia wachezaji kukubali usajili
TIMU yako inasajili wachezaji wapya kila msimu. Wachezaji wanazihama timu zao na kuamua kwenda mpya au kukataa kuondoka klabuni mwao. Lakini hebu tujiulize ni sababu gani hasa ambazo zinafawanya wachezaji wahame au wabaki katika timu fulani. Labda tuangalie ni sababu zipi angalau tano zinazosababisha wachezaji kuhamia timu mpya? Bila shaka sababu ya kwanza inaweza kutajwa ni pesa.
Ingawaje uchunguzi wa tanzaniasports.com haujawafikia wachezaji 100 wa kulipwa waliofanikiwa. Badala yake wamemudu kuzungumza na vigogo wazito wanaoheshimika katika soka, wakiwemo wachezaji wa sasa, makocha na mawakala, kutafuta sababu za wachezaji wanachagua kujiunga timu walizonazo kwa sasa.
Mazingira, muda wa mchezo,maisha, mfumo wa kucheza, makocha, faida za kibiashara- ndiyo taswira iliyojengwa kocha Arsene Wenger kila alipotaka kumsajili mchezaji. Na zaidi ukubwa wa klabu,pamoja na malengo, vyote hivi vimekuwa na mchango mkubwa linapofika suala la kumsajili mchezaji ambaye aataviangalia vigezo hivyo vyote kama vinaendana na matakwa yake. Kwa mfano kwa sasa Lionel Messi atakuwa anazingatia sababu tajwa hapo juu.
‘F’ TATU ZA USAJILI
Wakala mmoja ameeleza sababu hizo kwa ufupi tu; “ni F kwa lugha ya Kiingereza. Herufi F imewakilisha; Football (Soka), Family (Familia) na Finance (Fedha).”
Anaongeza, “Herufi hizo zinasimama badala ya maneno yanayoeleza sababu za msingi katika uamuzi wa wachezaji katika kazi zao. Kwahiyo kuna sababu zingine pia mbali ya fedha inayojulikana zaidi,”
Kufafanua hoja yake, anatolea mfano mchezaji mmoja aliyeamua kujiunga timu ya Ligi Kuu England mwaka jana katikati ya msimu, licha ya kuwa na malipo ya ziada ya pauni 5000 kwa wiki katika timu kubwa iliyomhitaji lakini hakwenda.
“Unapewa muda wa miezi 18 Ligi Kuu England dhidi ya sifuri ya timu katika ligi hiyo hiyo.” Anasema wakala huyo, na kuingia katika hoja nyingine ya fedha ya wateja wake.
“Mchezaji hawezi kukubali kujiunga na timu fulani kwa sababu ya fedha tu. Mchezaji anaweza kunipa orodha ya timu anazopenda kuchezea kwa miaka mitatu au mine, na atakuwa analipwa pauni 45,000 kwa wiki lakini anaweza kupata pauni 50,000 kwingine. Ukweli ni kwamba, ukiwa wakala wanatakiwa kuhakikisha mchezaji anapata malipo mazuri na timu nzuri. Kama umepata nafasi Newcastle United, halafu wanakuja watu wa Crystal Palace na Burnley inabidi uwadanganye kidogo kwa sababu wakati huo unafikiria timu ya kuchagua kujiunga, ili uhakikishe kuwa wanatoa ofa nzuri ambayo mchezaji hatojutia,” anasema wakala mwingine
FAMILIA KUAMUA PA KWENDA
Baadhi ya dili za usajili mchezaji anaweza kupata ofa za timu nyingi, kila upande lakini wawakilishi wake wanakuwa na kauli ya mwisho kuliko mchezaji mwenyewe linapofika suala la uamuzi wa ofa.
“Upo wakati nawaona wachezaji hawachagui timu, lakini kwenda klabuni kuomba punguzo la malipo ya wakala au namna nyingine ni mambo ya kawaida hivyo sio suala la fedha linalomsukuma mchezaji kujiunga na timu,” anasema kocha mmoja wa timu ya daraja la pili.
Fedha nyingi haziwezi kuwavutia au kuwa na maana kwa wachezaji kuwa matajiri. Lee Johnson, kocha wa zamani wa Bristol City, alizungumza msimu uliopita kuhusu sababu ya malipo ya Kifamilia (kufahamiana/kujuana) yanavyochagia mchezaji kujiunga na timu fulani.
Kiongozi mwandamizi wa Ligi Kuu England ameimbia www.tanzaniasports.com kwamba kumeibuka tatizo katika mchezo wa soka na kwamba imeweka mipaka ambayo inazidi kutibua maendeleo ya mchezaji hasa pale wazazi au ndugu wanapokuwa sehemu ya majadiliano ya fedha ya watoto au ndugu yao.
“Mawakala au wawakilishi wa wachezaji kwa sasa wengi wao wanatoka katika familia zao iwe ndugu au wazazi wao,” anasema kocha mwingine wa timu ya daraja la kwanza England.
“Wakati mwingine anaweza kuwa baba mzazi au kaka, binamu wanaongoza vikao vya majadiliano ya kusajiliwa mchezaji pengine bila mchezaji kufahamu undani na msingi wa makuibaliano,”
Aidha, uwepo wa wazazi matika dili za usajili wakati mwingine sio rasmi. Inafahamika kuwa wazazi wa mchezaji mmoja wa Ligi Kuu England walidai malipo makubwa msimu uliopita kwa msingi kwamba wao ndio wazazi wa mshambuliaji huyo. Pamoja na klabu zingine kumgombania kumsajili, lakini makocha wengi hawakupenda mfumo waliotumia wazazi hao kudai malipo.
MUDA WA KUCHEZA
Kwenye majadiliano ya dili za usajili suala la muda wa kucheza nalo linajadiliwa. Ni jambo muhimu kwa upande wa mchezaji kuliko wawakilishi wake, kwa sababu linakuwa na mchango mkubwa wa maendeleo ya kipaji chake. Lolote linaloendelea uwanjani kwa mchezaji basi chanzo chake ni kwenye majadiliano ya mikataba kuhusu muda wa kucheza..
Wachezaji wanaweza kupoteza hisia ya kucheza kirahisi sana, na kadhani hawatumiki ipasavyo, hasa wale wanaojiunga kwa mkopo. Wakati Renato Sanches alipojiunga na Swansea City kwa mkopo akitokea Bayern Munich mwaka 2017, walilipa kiasi cha pauni milioni 8 kama ada ya mkopo na mshahara wa mchezaji ambaye alifanikiwa kucheza mechi 15 tu.
Ukweli hakuwa na furaha kabisa Swansea City. “Halikuwa chaguo langu kwenda kujiunga Swansea City. Nililazimishwa kwenda huko kuchezea timu hiyo. Sikuwa na mpango nayo kabisa,” alisema Sanches mapema februari.
FEDHA SI KITU BILA MAKOCHA
Ni kweli fedha inaongea katika dili za usajili, lakini makocha nao wanao mchango mkubwa na pengine kuzidi sababu zingine zilizotajwa.
“Wapo makocha wanaowapigia simu wachezaji bila hata kuonana nao katika majadiliano na masharti ya mikataba. Wengine wanatumia mfumo wa video kumweleza mchezaji namna watakavyoboresha kiwango na kipaji chake. Mchezaji ataambiwa namna ya kucheza katika timu anayotaka, mbinu na mipango ya mechi na namna staili yake ya uchezaji inavyoweza kuinufaisha timu. Hivi ni vitu vyenye mchango kwa mchezaji moja kwa moja. Wapo makocha wanaoelezea kwa undani na wengine husema kidogo,” anasema wakala mmoja.
‘Baadhi ya timu zinawakaribisha vizuri. Zina uungwana fulani, wanaweza kukupa kahawa ukanywa vizuri. Mfano kama unaenda kukutana na Karren Brady wa Westham, huwezi kukaribishwa kama uko nyumbani. Lakini Everton unakaribishwa kama uko nyumbani kwako. Na pia, inategemeana na aina ya kocha aliyeko katika timu ili kumshawishi mchezaji kujiunga,”
“Kama unakataa kujiunga na Everton wakati inafundishwa na Sam Allardyce utakuwa mchezaji wa ajabu. Yule ni kocha ambaye anamuuliza mchezaji hali yake ya afya anapoonana nae,, anamkaribisha kama mwanae na kumwagia sifa juu ya juhidi walizofanya kumsajili. Sababu ni moja tu; Big Sam anatumia mtindo wa kizamani, kiungwana na kumfanya mchezaji ajisikie yuko nyumbani hata kama anaingiza mamilioni ya fedha. Kama ulikataa ofa ya Everton wakati inafundishwa na Marco Silva, utakuwa umefanya vizuri, mjinga mno huyo. Alikuwa aina ya watu wakimya au wapole hadi anakera,” anasema Wakala huyo.
Wenger ni miongoni mwa makocha vipenzi katika kandanda. “Alikuwa mcheshi sana. Ndani ya dakika tano tu anaweza kuwapeleka mkahawani kupata chakula kwa gharama zake. kama unahitaji saa mbili tu za kufanya mazungumzo naye anaweza kukuongezea saa moja lingine. Haiba yake inawavutia wengi na alizungumzwa vizuri sana.”
Jina la Wenger linaleta simulizi ya Aaron Ramsey kutoka Cardiff kwenda Arsenal mwaka 2008. Ramsey alipotembelea Manchester United , ambao walikubali ada ya Cardiff, Sir Alex Ferguson hakuwepo ofisini na akamwagiza msaidizi wake Mike Phelan kumpokea kijana huyo klabuni hapo. Kwa upande wao Arsenal walimsafirisha Ramsey na wazazi wake hadi nchini Uswisi kukutana na Arsene Wenger, ambaye alikuwa anafanya kazi kama mchambuzi wa fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya (EURO), na Wenger akimweleza Ramsey kuhusu mipango ya Arsenal kuendeleza kipaji chake. Hapo ndipo Ramsey na wazazi wake walipobadili mawazo ya kujiunga Manchester United badala yake wakageuka na kwenda Asrenal.
Comments
Loading…