in , , , ,

Falcao hali ngumu


*Ashindwa kufunga U-21, atolewa nje

Hali ya mshambuliaji wa kati wa Manchester United, Radamel Falcao inazidi kuwa mbaya katika timu hiyo.
Falcao ambaye amekuwa ama akianzia benchi au nje kabisa ya kikosi kwenye mechi nyingi za United, amefikia kuchezeshwa kikosi cha wenye umri wa chini ya miaka 21 na bado anatolewa nje kabla ya mechi kumalizika.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia aliye kwa mkopo United kutoka Monaco, aliwekwa benchi kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Arsenal Jumatatu hii na hakupewa nafasi kucheza.
Falcao Jumanne hii alipewa fursa ya kuchezea kikosi cha U-21 cha Man U dhidi ya Tottenham Hotspur, akashindwa kufurukuta wala kufunga bao kwa dakika 71, ndipo kocha Warren Joyce alipomtoa nje na kumwingiza Joshua Harrop.

Katika mechi iliyomalizika kwa sare ya 1-1 Falcao (29) anayelipwa pauni 260,000 kwa wiki hakucheza vyema na huenda United wasipendelee kumchukua moja kwa moja kwa gharama ya pauni milioni 43.5 mwishoni mwa msimu.

Katika msimu huu, chini ya kocha Louis van Gaal aliyemsajili siku ya mwisho kwa matarajio ya kuwa mpachika mabao kiongozi, Falcao amefunga mabao manne tu katika mechi 20.
Hata hivyo, Van Gaal amemwanzisha mechi mbili tu kati ya tano za United zilizopita, na Jumatatu alisugua benchi hadi mwisho, maana kocha hakuona kama angeweza kwenda kuokoa jahazi.
Van Gaal amepata kudai kwamba Falcao ana uwezo wa kucheza chini ya nusu saa tu kwa mechi kwa sababu hayupo timamu kimwili, lakini mchezaji huyo, mkewe na wakala wake walikerwa.

Wengine wa kikosi cha kwanza waliocheza ni mshambuliaji James Wilson ambaye Van Gaal humpendelea kuliko Flcao, golikipa Victor Valdes na mlinzi Rafael da Silva aliyefunga bao la United kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu kwa U-21.

Kwa kawaida wachezaji waliokuwa wagonjwa, majeruhi au walioshuka viwango huchezeshwa kwenye kikosi cha pili ili kuwapa utimamu kabla ya kuwarejesha kwenye kikosi cha kwanza.
Falcao alikuwa matata akiwa Atletico Madrid, ambapo alifunga mabao 52 katika mechi 68 za La Liga, hivyo kuwavuta Monaco waliomnunua kwa pauni milioni 52.

Rafael (24) amecheza mechi 10 tu kwa kikosi cha kwanza msimu huu, wakati Valdes (33) bado hajacheza chini ya Van Gaal tangu alipomsajili kama mchezaji huru.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ushindi wa Arsenal kwa Man U shida

Chelsea watupwa nje Ulaya