in

Eti Uingereza imeleta gundu Afrika

The Cranes

Wakati mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN yakiendelea sasa nchini Cameron upo utani ambao unaumiza akili za mashabiki wa wengi. 

Baadhi ya mashabiki wanachukulia kama utani wa mpira wa miguu lakini umekuwa ukweli unaoziamndamana nchi zinazohisishwa na kihistoria na Uingereza. 

Wanasema nchi zote zilizotawaliwa na Uingereza hazijawahi kutoboa kwenye kandanda duniani, ama zilizowahi ni chache na hazijawahi kufika matawi ya juu.

Historia inaonesha kuwa Bara la Afrika limetawaliwa na wakoloni wa Uingereza, Ufaransa, Ureno, Hispania, Ujerumani na Ubelgiji. Mataifa hayo ndiyo yaligawana makoloni na kuyakalia, kaskazini mwa Afrika, kusini mwa Afrika, nchi za Maziwa Makuu na Afrika mashariki na Afrika magharibi. 

Mara baada ya timu ya taifa ya Tanzania kuchapwa mabao 2-0 na Zambia utani huo uliibuka tena mitandaoni kuwa kwa vile Tanzania ilikuwa koloni la Uingereza hivyo imeathiriwa na mwenendo ambao hata Uingereza wenyewe hawana mafanikio kisoka.

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia lililofungwa na winga Farid Mussa Shah waliopata Taifa Stars uliendeleza utani uleule. Kwamba Namibia nayo imepitia mikononi mwa ukoloni wa Uingereza hivyo haieezi kuwa na mafanikio kisoka hapa duniani. 

Takwimu zinaonesha ni mataifa mawili pekee ambayo yamepata mafanikio makubwa kisoka na ambayo yaliwahi kutawaliwa na wakoloni wa Uingereza, ambayo ni Ghana na Nigeria. 

Hata Uingereza wenyewe kwenye mashindano ya Ulaya na Kombe la Dunia wamekuwa ‘wakitapika damu’ kwa kushindwa kufurukuta. 

Ingawa jambo hilo linaonekana kama utani w asoka lakini linao ukweli wake kwenye mashindano mbalimbali  ambayo yanafanyika iwe yanayoandaliwa na FIFA au CAF habari imekuwa ni ileile moja. 

KOMBE LA DUNIA

Mataifa mawili yaliyotawaliwa na Uingereza ya Nigeria na Ghana yamewatoa kimasomaso kati ya mengi. Kwenye mashindano ya Kombe la Dunia, Ghana imewahi kufika hatua ya robo fainali mwaka 2010 nchini Afrika kusini kabla ya kutolewa na Uruguay.

Nigeria ni taifa lenye historia maridhawa barani Afrika na miongoni mwa vigogo vinavyoogopewa kwenye Fainali za Kombe la Dunia kila inaposhiriki. 

Kwa mara ya kwanza Nigeria ilishiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani, ambako iliwashangaza wengi kutinga raundi ya pili kwenye mashindano hayo. 

Tukirudi nyuma kidogo tunaona Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1990 zilikuwa za Cameron ambayo ilifanikiwa kutinga robo fainali. Cameron imetawaliwa na mkoloni wa Kifaransa. 

Cameron imeshiriki fainali 7 za Kombe la Dunia 7 katika miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014. Hii ndiyo nchi yabkwanza barani Afrika kushiriki Fainali za Kombe la Dunia mara nyingi zaidi. 

Nigeria imeshiriki Fainali 6 za Kombe la Dunia katika miaka ya 1994,1998, 2002,2010,2014 na 2018. Hii ni nchi ya pili barani Afrika kushiriki mara nyingi zaidi kwenye mashindano hayo. Pia ni nchi ya kwanza kati ya zile zilizotawaliwa na Uingereza kufanikiwa kuweka rekodi hiyo.

Morocco imeshiriki Fainali 5 za Kombe la Dunia mnamo mwaka 1970, 1986, 1994, 1998 na 2018. Hii ni nchi ya pili kimafanikio ya soka kati ya mataifa yaliyotawaliwa na mkoloni wa Kifaransa. 

Tunisia imeshiriki Fainali 5 za Kombe la Dunia 1978,1998,2002,2006 na 2018. Hii inakuwa nchi ya tatu kati ya zile zilizotawaliwa na Ufaransa kushiriki mara nyingi kwenye mashindano ya FIFA.

Algeria imeshiriki Fainali 4 za Kombe la Dunia, 1982,1986,2010, na 2014. Nayo ni nchi inayotoka kwenye upande wa mkoloni wa Ufaransa ikiwa imeshiriki mara nyingi mashindano ya FIFA. 

Ghana imeshiriki Fainali 3 za Kombe la Dunia 2006, 2010 na 2014. Hii inakuwa nchi ya pili baada ya Nigeria kutoka zile zilizotawaliwa na mkoloni wa Kiingereza.

Ivory Coast imeshiriki Fainali 3 za Kombe la Dunia 2006,2010 na 2014. Ni nchi inayotoka  katika kambi ya mkoloni wa Kifaransa ikiwa imetoa mastaa wengi duniani na kushiriki mashindano hayo.

Misri imeshiriki fainali 3 za kombe la dunia, 1934,1990 na 2018. Misri ni miongoni mwa mataifa yaliyotawaliwa na Ufaransa, likiwa limeshiriki mashindano ya FIFA mwanzoni kwa kabisa tangu kuanzishwa kwake.

Afrika kusini imeshiriki fainali 3 za kombe la dunia 1998,2002 na 2010. Makaburu kutoka Uholanzi waliungwa mkono na Uingereza na Marekani ndiyo walitawala taifa hilo. 

Senegal imeshiriki Fainali mbili za Kombe la Dunia 2002, 2018. Kizazi cha Senegal cha mwala 2002 ndicho kilifanya makubwa kwenye soka, kabla ya baadaye kufuatiwa na vijana waliovuna matunda ya kazi za kaka zao. Senegal ilitawaliwa na Ufaransa.

DR Congo imeshiriki Fainali  moja ya Kombe la dunia 1974. Ni taifa la kwanza kutoka Nchi za Maziwa Makuu kushiriki Finali za Kombe la Dunia.  Kihistoria ilitawaliwa na Ufaransa na Ubelgiji kwa nyakati tofauti.

Togo imeshiriki Fainali moja ya Kombe la Dunia 2006. Hii nayo imtawaliwa na Ufaransa, hivyo kwao kufuzu fainali za Kombe la Dunia yalikuwa mafanikio makubwa. 

Angola imeshiriki Fainali moja ya Kombe la Dunia 2006. Hili ni taifa lililotawaliwa na mkoloni wa Ureno. Likiwa taifa la kwanza kutawaliwa na Ureno kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, na la pili kutoka kusini mwa Afrika kushiriki mashindano hayo baada ya Afrika Kusini.

UBINGWA WA AFCON

Nchi za Afrika magharibi zinaongoza kwa kushiriki mashindano ya kombe la dunia na Afrika. Hebu tuangalie takwimu za mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kuona uhalisi. 

Tukichukua takwimu za AFCON kuanzia mwaka 2000 hadi sasa utaona mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza hayana mafanikio yoyote kisoka. Fainalinza mwaka 2000 bingwa ni Cameron. Fainali za mwaka 2002 bingwa ni Cameron.

Fainali za mwaka 2004 bingwa ni Tunisia. Fainali za mwaka 2006 bingwa ni Misri. Fainali za mwaka 2008 bingwa ni Misri. Fainali za mwaka 2010 bingwa ni Misri.

Fainali za mwaka 2012 bingwa ni Nigeria. Fainali za mwaka 2013 bingwa ni Zambia. Fainali za mwaka 2015 bingwa ni Ivory Coast. Fainali za mwaka 2017 bingwa ni Cameron. Fainali za mwaka 2019 bingwa ni Algeria.

Takwimu zinaonesha Misri imetwaa AFCON mara 7, Cameron (5), Ghana (4),Nigeria (3), Ivory Coast (2), Algeria (2), DR Congo (2), Zambia(1),Tunisia (1),Sudan (1),Ethiopia(1)Morocco(1),Afrika kusini (1) na Congo (1)

Kwa nchi za kusini mwa Afrika ni Zambia na Afrika kusini pekee ndizo zimetwaa AFCON. Zambia imecheza mechi 3 za fainali kuliko zingine za kusini mwa Afrika.

MATAJI YA KLABU

Klabu za Esperance, Etoile Du Sahel na Club African za Tunisia zimekuwa zikicheza kwa mafanikio kwenye mashindano ya ngazi za klabu barani Afrika.

Klabu za Waydad Casablanca na Raja Casablanca ni klabu  za Morocco ambazo zimekuwa miongoni mwa vigogo wa soka kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Asec Mimosas (Ivory Coast), Hearts of Oak, Asante Kotoko (Ghana), JS Kablie (Algeria), FC Horoya, Enyimba, Al Ahly, Ismailia, Zamalek, Coton Sports na nyinginezo zimekuwa miamba ya soka Afrika ngazi ya klabu. 

Nyingi ya klabu hizo zinatoka Afrika magharibi. Lakini nyingi zaidi zinatoka katika mataifa ambayo yalitawaliwa na mkoloni wa Kifaransa. 

Mara chache utaona klabu zilitoka nchi zilizotawaliwa na Mwingereza zikicheza kwa mafaniko. Kwahiyo zile cnhi za Francophone zote zimekuwa tishio kwenye soka Afrika kama zilivyo timu zao za taifa. 

Kwa upande wa kusini mwa Afrika klabu za Kaizer Chiefs, Orlando Pirates, Petro Atletico zimekuwa zikicheza kwa mafanikio kwenye mashindano mbalimbali Afrika. Zote hazikuwa mkoloni wa kiingereza.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Didier Gomes Da Rosa

SIMBA ni WCB ya mpira wa miguu ?

Taifa Stars

Tulikosea mechi ya Zambia