in , , ,

EPL kuendelea tena J1 hii

Baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa Ligi Kuu ya England itaendelea tena kutimua vumbi hapo Jumamosi. Tunaangalia michezo ya wiki hii ya timu nne za EPL zenye mashabiki wengi zaidi huko nyumbani.

EPL LOGO

Timu hizo ni Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester United.  Kati ya timu hizo hakuna yoyote iliyo ndani ya nafasi nne za juu mbaka sasa kwenye msimamo wa EPL. Nafikiri kila moja inatazamia kuanza ligi rasmi hapo Jumamosi.

*Je Van Gaal ataanza ligi rasmi Jumamosi kwa kuwashushia kipigo Liverpool?

*Je Everton wataendeleza mwanzo mbaya wa Chelsea msimu huu?

*Je Arsenal wataitumia vizuri nafasi ya kuwaacha nyuma Manchester United au/na Liverpool?

Maswali hayo matatu hapo juu yatapata majibu kamili hapo Jumamosi wiki hii. Majibu ya maswali hayo yatapatikana kupitia matokeo ya michezo mitatu inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki. Kwenye makala hii tunaangalia michezo hiyo mitatu.

 

Manchester United v Liverpool

deee

 

Timu hizi mbili zitakutana Jumamosi hii kila moja ikiwa na jumla ya alama 7 kwenye msimamo wa EPL. Luis Van Gaal ameshinda mechi zote mbili alizokutana na Liverpool tangu alipojiunga na Manchester United mwaka jana. Ni wazi kuwa ana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi.

Brendan Rodgers pia atahitaji ushindi kwa kuwa akipoteza mchezo huu ataachwa nyuma na Manchester United kwa alama tatu na pia Arsenal huenda wakamuacha kwa alama hizo hizo. Mchezo huu utakuwa wa kushambualiana zaidi. Timu itakayotumia vizuri nafasi zake za kufunga ndio itakayoshinda.

United pengine watamtumia mshambuliaji wao mpya Anthony Martial. Atashirikiana na Wayne Rooney na Memphis Depay kwenye safu ya ushambuliaji. Liverpool itamkosa Philippe Coutinho anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu. Hata hivyo uwepo wa Christian Benteke na Roberto Firmino unatosha kabisa kupeleka kilio Old Trafford.

 

Everton v Chelsea

ctt

Chelsea wameshinda mchezo mmoja tu mbaka sasa kati ya michezo minne waliyocheza. Pia mabingwa hao watetezi wameruhusu mabao 9 mbaka sasa ambayo ni mengi kuliko timu yoyote ukiwatoa Sunderland wanaoburuza mkia kwenye msimamo wa EPL.

Kocha Jose Mourinho yupo kwenye presha ya hali ya juu kwa sasa kwa kuwa timu yake imekuwa na mwanzo mbaya msimu huu. Msimu uliopita akiwa na timu hii alishinda mechi zake zote nne za mwanzo ukiwemo mchezo dhidi ya Everton anaokutana nao hapo Jumamosi.

Pengine matokeo mabovu ya Chelsea kwenye michezo ya nyuma yanampa matumaini mwalimu wa Everton Roberto Martinez hivyo huenda atakiongoza kikosi chake kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kuendeleza mwanzo mbaya wa Chelsea msimu huu.

 

Arsenal v Stoke City

awe

Arsenal wanacheza nyumbani kwenye dimba la Emirates siku ya Jumamosi wakiwa bado hawajapata ushindi kwenye dimba hilo msimu huu. Kwenye mchezo wao wa kwanza wa nyumbani walipoteza dhidi ya West Ham kwa 2-0 na mchezo wao wa pili wa nyumbani uliisha kwa sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool.

Arsene Wenger ataingiza kikosi chake uwanjani kutafuta ushindi ili waiache nyuma Liverpool au/na Manchester United ambazo kila moja ina alama 7 sawa na Arsenal. Timu hizo zinakutana zenyewe hapo Jumamosi hivyo ni wazi kuwa moja kati yao itapoteza alama ama zitatoka sare na kugawana alama moja moja.

Stoke City bado haijapata ushindi wowote msimu huu na Jumamosi itapambana na Arsenal bila nyota wao wawili muhimu walioonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya West Bromwich. Hao ni Ibrahim Affellay na Charlie Adam. Huenda Arsenal watapata ushindi mkubwa hapo Jumamosi.

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

BAADA YA WAYNE ROONEY HAWA WATAFUATA

Tanzania Sports

NANI ATAKUWA MENEJA WA KWANZA KUTIMULIWA EPL MSIMU HUU?