in , , , ,

BAADA YA WAYNE ROONEY HAWA WATAFUATA

 

 

Wayne Rooney hapo jana alivunja rekodi ya mabao ya Sir Bobby Charlton baada ya kuifungia England kwa mkwaju wa penati dhidi ya Switzerland. Sasa nahodha huyo wa Manchester United na England anakuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa akiwa na mabao 50.

Rooney anaungana na Cristiano Ronaldo, Luis Suarez, Zlatan Ibrahimovic na washambuliaji wengine tishio wa zama hizi ambao ni vinara wa mabao kwenye timu zao za taifa.

Kuna baadhi ya washambuliaji nyota wa sasa bado hawajaweza kuwa vinara wa mabao kwenye timu zao za taifa akiwemo Lionel Messi. Kwenye makala hii tunakuonyesha nyota wengine ambao wana uwezekano mkubwa wa kuvunja rekodi za mabao kwenye timu zao za taifa.

LIONEL MESSI – Jana Lionel Messi aliifungia Argentina bao moja dhidi ya Mexico kwenye mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2.  Bao hilo limemfanya Messi kubakisha idadi ya mabao 8 pekee kuelekea kuwa kinara wa mabao wa muda wote wa Argentina. Ataivunja rekodi inayoshikiliwa Batistuta mwenye mabao 56 hivi punde. Pengine watu wanadhani amechelewa kuivunja rekodi hii ila ikumbukwe kwenye orodha ya wafungaji wa Argentina aliotakiwa kuwapita ili awe kinara wa mabao kulikuwepo na watu kama Hernan Crespo, Maradona na Batistuta.

GARETH BALE – Nyota huyu wa timu ya taifa ya Wales na Real Madrid tayari ameshaifungia Wales mabao 18. Anahitaji kuwavuka nyota watano ambao ni Craig Bellamy, Dean Saunders, Ivor Allchurch, Trevor Ford na Ian Rush ambao wamemzidi kwa idadi ya mabao kwenye chati ya wafungaji wa muda wote wa timu ya taifa ya Wales. Kati ya nyota hao watano hakuna ambaye bado anachezea timu ya taifa kwa sasa. Ian Rush ndiye kinara kwenye chati hiyo akiwa na mabao 28. Haitachukua muda mrefu Gareth Bale kuivunja rekodi ya Rush kutokana na moto alio nao kwa sasa.

KOLBEIN SIGTHORSSON – Mshambuliaji huyu wa FC Nantes ni mmoja kati ya washambuliaji mashuhuri ndani ya taifa la Iceland. Anaifukuza rekodi ya Eidur Gudjohnsen. Gudjohnsen ambaye ni nyota wa zamani wa Chelsea na Barcelona anashikilia rekodi ya mabao ya muda wote ya timu ya taifa ya Iceland akiwa na mabao 25. Sigthorsson mwenye umri wa miaka 25 tayari ameshaifungia Iceland mabao 17 hivyo anayo nafasi kubwa ya kuvunja rekodi ya Gugjohnsen mwenye miaka 37 sasa  hivyo atastahafu hivi karibuni ingawa bado yupo kwenye kikosi cha Iceland.

MAREK HAMSIK – Hamsik tayari ameshaifungia mabao 15 timu ya taifa ya Slovakia. Anainyatia rekodi inayoshikiliwa na Robert Vittek  ambaye ndiye kinara wa mabao wa Slovakia akiwa na jumla ya mabao 23. Vittek bado yumo kwenye kikosi cha sasa cha Slovakia hivyo huenda akaongeza idadi yake ya mabao na kuitia ugumu safari ya Hamsik. Kinachompa matumaini Hamsik ni umri wa Vittek ambaye tayari ana miaka 33 hivyo si muda mrefu hatakuwepo kikosini. Hamsik ana umri wa miaka 28 hivyo bado ana michezo mingi ya kuichezea Slovakia na kuweka rekodi ya mabao mengi zaidi.

NEYMAR JUNIOR – Neymar ana umri wa miaka 23 tu na tayari ameshaifungia Brazil mabao 46 mbaka sasa. Inawezekana atakuwa mfungaji bora wa muda wote wa Brazil miaka ya mbeleni. Hata hivyo mlima anaohitaji kuupanda mshambuliaji huyu ili aifikie rekodi hiyo si mdogo. Anahitaji kuvunja rekodi za mabao ya Zico, Romario na Ronaldo kwanza. Baada ya hapo ndipo atajipanga kumpita Pele mwenye rekodi ya  mabao 77. Neymar ana kipaji cha hali ya juu na bado ana zaidi ya miaka kumi ya kuichezea timu ya taifa ya Brazil hivyo tutarajie atamfunika Pele tu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Kuna wachezaji 176 kutoka England, kati ya wachezaji 528 wa EPL

Tanzania Sports

EPL kuendelea tena J1 hii