Nyota ya soka iliyozima
Aliiteka dunia kwa soka yake baada ya kuonesha kipaji cha aina yake tangu utoto wake.
Diego Armando Maradona amepumzika usingizi wa milele siku chache baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
Maradona alikuwa kama uwakilishi wa sura tofauti za mwanadamu mwenye uwezo mkubwa kwa mambo magumu, mwenye utata pia na wakati mwingine akiupelekesha ulimwengu wa soka kiasi cha baadhi kuamini hadi leo kwamba ndiye mwanasoka mahiri zaidi katika historia.
Pamoja na umahiri wake uwanjani na nje, Maradona amekuwa pia na utata, hasa alipokaribia na kisha kustaafu, kwa habari ya matumizi ya dawa za kulevya zisizoruhusiwa na mambo mengine ya jinai.
Lakini kwa habari ya dimbani, Maradona atabaki kwenye kumbukumbu kwa bao lake la mkono dhidi ya Timu ya Taifa ya England Juni ya 1986, kwenye fainali za Kombe la Dunia hatua ya robo fainali ambapo Argentina waliishia kushinda 2-1.
Hata baada ya England kusawazisha, alikuwa Maradona tena aliyefunga lililoitwa ‘Bao la Karne’ akiisha kuchukua mpira kwenye nusu yao, akawalamba chenga wachezaji wa England, akakimbia hadi kwenye lango la wapinzani wao, akamlamba chenga golikipa Peter Shilton na kuandika bao.
Lile la kwanza la mkono, mwenyewe aliliita baadaye kuwa ni ‘Bao la Mkono wa Mungu’. Argentina walisonga mbele na kuwafunga Ubelgiji kwenye nusu fainali kisha Maradona akawaongoza kutwaa ubingwa wa dunia kwa kuwapiga Ujerumani Magharibi.
Ni huyu anayekumbukwa kwa kuvunja rekodi ya usajili mara mbili duniani; akisajiliwa kwanza na Barcelona, Hispania kutoka Bocka Juniors ya kwao Argentina kisha kwenda Napoli, Italia kwa bei kubwa kuliko zote za wakati huo. Napoli alipokewa na washabiki 80,000 alipowasili kwa helikopta uwanjani.
“Mwanamume mwenye kipaji cha pekee havumiliki isipokuwa kama ana vitu viwili zaidi; shukurani na usafi,” anasema Friedrich Nietzsche, juu ya upendo, uvumilivu na kusonga mbele, ng’ambo ya jema dhidi v uovu.
Maradona mwenyewe alipata kusema kwamba ukiisha kufika mwezini na kurudi duniani, mambo ni tofauti. “Unakuwa na mzio na mwezi na si wakati wote kwamba kuna uwezekano wa kurudi chini,” akasema.
Maradona alifikisha umri wa miaka 60 Oktoba 30 na salamu zilizomiminika kutoka kila kona ya dunia ilikuwa kama vile kusherehekea maisha ambayo yalionekana kukaribia mwisho. Alikuwa tayari anaumwa, kutokana na matatizo ya moyo na hatimaye alifanyiwa upasuaji ulioelezwa kwamba ulikuwa wa kawaida.
Alitokea kwa muda mfupi kwenye hafla ya siku ya kuzaliwa kwake kwenye klabu ya Gimnasia y Esgrima de La Plata, sura ikionekana kuwa ya kusikitisha, kwani alionekana wazi kwamba uwazi wake ulikuwa umepitiliza, akitembea taratibu akijitaidi bila kusaidiwa, kuzungumza nako hakukuwa kwema sana.
Alishindwa pia kupokea na kushika zawadi aliyokuwa amepewa, ikionekana wazi kwamba ile nguvu aliyokuwa nayo awali ilikuwa ikimtoka.
Yupo aliyesema kwamba ni afadhali amepumzika, kwa maana ilikuwa inaumiza sana kumwona alivyokuwa akishuka kihali. Alizaliwa na kukuzwa Villa Fiorito, nje kiodoho ya Buenos Aires, na uwezo wake kwa mpira uligundulika wazi mapema sana katika umri mdogo, ikawa kawaida kuanza kuchukuliwa picha za video na vituo vya televisheni.
Aliondoshwa kwenye kikosi cha fainali za Kombe la Dunia 1978 baada ya kucheza mechi kadhaa za kufuzu, na Maradona anasema ndipo alianza kuchanganyikiwa lakini ilikuwa muhimu, kwani ndiko kulikomwezesha kujenga maisha yake kwa kutia jitihada.
Mwaka uliofuata alifanikiwa kutwaa Kombe la Dunia la Vijana na kadiri muda ulivyokwenda akatokea kuwa nembo ya Argentina, akaja kuwa nyota mkubwa. Umaarufu wake, na wakati mwingine utata, ulisababisha hafla za siku zake za kuzaliwa kurushwa na vyombo vya habari; ugomvi wake na wenza wake kuchukuliwa picha pia kwa sim una kisha kuvujishwa mitandaoni.
Mijadala ilikuwa pia mikubwa baada ya kubainika Watoto waliozaliwa nje ya ndoa walikuwa wake, ilimradi tu kila jambo lake halikupita bila kujadiliwa. Ni kana kwamba alikuwa akikabiliana namapepo hadharani, akizungumza wazi juu ya mzio aliopata kwenye madawa ya kulevya huku akienda kila mahali na dawa alizopewa.
Katika maisha yake kuna vitu alikuwa akizidisha sana kula na kunywa pia – pizza na champagne. Uzito uliongezeka hadi zaidi ya kilogramu 128 na alifanyiwa upasuaji ili kumsaidia kwa changamoto hiyo.
Watu wamekuwa wakijadili hali zake – kipaji na umahiri wa miguu yake, vitu alivyokosa kwa akili yake, lakini ukweli ni kwamba pia akili ilifanya kazi ndiyo maana aliweza kuwa na mafanikio kwenye soka kiasi hiki. Alikaa sana mazoezini kuliko wengine, akijaribu kile alichoona alikuwa na udhaifu; akafanya hivyo tena na tena hadi alipofanikiwa.
Ni ukweli pia kwamba alikuwa akilala nyakati ziziso za kawaida, pengine akitarajia pia ulimwengu kwenda na kasi yake. Labda sasa, mwishowe tunaweza kusema kwamba anaweza kupumzika – tulia sasa. Usingizi wa Diego.
Comments
Loading…