in , , ,

CONGO YAWASILI KUIVAA SERENGETI BOYS

Congo Brazzaville imewasili leo alfajiri (Novemba 15 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Tanzania (Serengeti Boys) itakayochezwa Jumapili.

Timu hiyo imewasili kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 18 ambapo imefikia kwenye hoteli ya Sapphire. Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Serengeti Boys inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa chini ya Kocha wake Jackob Michelsen wakati Congo inafanya mazoezi leo jioni Uwanja wa Karume, na kesho (Novemba 16 mwaka huu) asubuhi na jioni itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo.

Timu hiyo ambayo katika raundi ya pili iliitoa Zimbabwe itafanya mazoezi yake ya mwisho Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Viingilio kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa VIP A, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP C ni sh. 2,000 tu. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni sh. 1,000 tu.

Makocha wa timu zote mbili na manahodha wao watakutana na waandishi wa habari Jumamosi saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzungumzia maandalizi yao kwa ajili ya mechi hiyo kabambe.

 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Tuweke mikakati TOC mpya

The National Sports Council (NSC) has intensified efforts to resolve the long-standing netball quarrel