*Arsenal wapigwa, lakini wavuka
Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) imehitimishwa katika hatua za makundi kwa Chelsea kupata ushindi na kukaa kileleni kwa kundi lao la E.
Demba Ba aliyetumiwa jana aliwafungia Chelsea katika dakika ya 10 tu dhidi ya Steaua Bucharest katika dimba la Stamford Bridge.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal alifunga kutokana na mpira wa Oscar. Ba na Eden Hazard walikosa nafasi nyingine za wazi ambazo zingeweza kuwapatia ushindi mkubwa zaidi.
Chelsea wanaweza kukwaana na Bayer Leverkusen, Galatasaray, Olympiakos, Zenit St Petersburg au AC Milan katika hatua ya mtoano kwenye 16 bora.
Ratiba yake tapangwa jijini Nyon, Uswisi Jumatatu hii.
ARSENAL WACHAPWA NA KUVUKA
Arsenal nao walifanikiwa kuvuka hatua ya makundi licha ya kuchezea kichapo cha 2-0 nyumbani kwa Napoli.
Licha ya ushindi huo, Napoli wametolewa kwenye mashndano na Arsenal wakashika nafasi ya pili nyuma ya Borussia Dortmund.
Huu ni msimu wa 14 mfululizo Washika Bunduki wa London wanafika hatua hiyo. Mchezaji aliyewaniwa na Arsenal, Gonzalo Higuain ndiye aliyetangulia kuwaliza kabla ya Mikel Arteta wa Arsenal kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Jose Callejon alifunga bao la pili katika dakika za majeruhi lakini ushindi wa Borussia Dortmund wa 2-1 dhidi ya Marseille ulitosha kuwatupa nje vijana hao wa Rafa Benitez.
Kwa kushika nafasi ya pili, Arsenal sasa watakabiliana na moja ya timu za Bayern Munich,
Barcelona, Real Madrid, Paris St-Germain au Atletico Madrid.
MATOKEO MENGINE UCL
Katike mechi iliyorudiwa baada ya kuchezwa dakika chache Jumanne, Galatasaray waliwafunga Juventus 1-0, Schalke wakawafunga Basel 2-0 na Atletico Madrid wakashinda 2-0 dhidi ya Porto. FK Austria Vienna wakashinda 4-1 dhidi ya Zenit St Petersburg, Barcelona wakawakandika Celtic 6-1 na Milan wakaenda suluhu na Ajax.
Timu zilizofuzu kwa 16 bora ni Manchester United, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Galatasaray, Paris Saint Germain, Olympiakos, Bayern Munich, Manchester City na Chelsea.
Nyingine ni FC Schalke, Borussia Dortund, Arsenal, Atletico Madrid, Zenit St Petersburg, Barcelona na Milan.
Comments
Loading…