in , , ,

Chelsea wabanwa, Leicester hoi

*Man United wa sita kama kawa
*Spurs, Arsenal, City, Liver juu

WAKATI vinara wa Ligi Kuu ya England (EPL), Chelsea wakibanwa na
Burnley kwa sare, mabingwa watetezi, Leicester wameendelea kupokea
vichapo.

Chelsea wakiwa ugenini walitoshana nguvu 1-1 na Burnley, ambapo kwa
mara ya kwanza katika EPL kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois alikubali
mkwaju wa adhabu ndogo kuzama nyavuni moja kwa moja.

Pamoja na sare hiyo, Chelsea wanabaki kwenye uongozi wa ligi kwa
tofauti ya pointi 10. Leicester walikubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa
timu iliyoonesha udhaifu mkubwa hadi karibuni, Swansea.

Kwa mweleka huo, kocha Claudio Ranieri anasema pengine amekuwa mpole
mno kwa nyota wake ambao wamegeuka magarasa na sasa anasema huenda
akafanya mageuzi makubwa.

Lazima achukue hatua kwa sababu wamekuwa pointi moja tu sasa juu ya
eneo la kushuka daraja na mwenendo ukiwa hivi hapana shaka watarudi
ligi ya chini.

“Ni vigumu unapofanikiwa kupata kitu, kisha unataka kuwapa nafasi
moja, mbili, tatu, pengine sasa nimezidisha. Nadhani inabidi nifanye
mageuzi kwa sababu kwa mwenendo huu hatuwezi kuendelea. Nimekuwa
najiuliza; tuanze, tunaweza kufanya jema?” anasema Ranieri.

Leicester wanakuwa timu pekee katika madaraja manne ya juu ya ligi ya
England kutokuwa na bao lolote mwaka huu 2017 na pia mabingwa watetezi
wa kwanza kufungwa mechi ano mfululizo tangu Chelsea walipoadhibiwa
hivyo 1956.

Baadhi ya wachezaji waliochangia sana kupatikana kwa ubingwa msimu
uliopita na sasa wamekuwa magarasa ni mshambuliaji Jamie Vardy
aliyekataa kwenda Arsenal na kiungo Riyad Mahrez. Vardy alifunga mabao
24 msimu uliopita lakini huu anayo matano tu. Mahrez alifunga 17 na
kutoa usaidizi kwa mengine 10 lakini sasa anayo matatu tu.

Leicester wanaweza kuwa mkiani mwa ligi hivi karibuni, kwani
wanakabiliana na Liverpool Jumatatu ya Februari 27.

Arsenal waliotoka kwenye uchovu wa kichapo cha Chelsea 3-1
wamenyanyuka na kuwafunga Hull City 2-0 kwenye mechi ambayo walibanwa
na kupelekeshwa na bao lao moja kati ya mawili ya Alexis Sanchez
likidaiwa kuwa la mkono.

Manchester United wamebaki kwenye nafasi ‘yao’ ya sita baada ya
kuwafunga Watford 2-0, Everton wakabanwa ugenini na kwenda 0-0 na
Middlesbrough.

Stoke walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace, Sunderland
wakakandikwa 4-0 na Southampton, West Ham wakafungana 2-2 na West
Bromwich Albion na Liverpool wakiwa nyumbani wakawapiga Tottenham
Hotspur 2-0.

MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND

Msimamo wa ligi ya epl

Kwa matokeo ya wikiendi hii, Chelsea wanashika usukani wakiwa na
pointi 60 wakifuatiwa na Spurs wenye 50 sawa na Arsenal, Liverpool na
Manchester City wana 49 kila mmoja huku Man United wakiwa nazo 48.
Mkiani wapo Sunderland na pointi zao 19 sawa na Palace, Hull wana 20
na Leicester wananukia kushuka wakiwa nazo 21, Middlesbrough wanazo
22, Swansea 24 na Bournemouth 26. Ni miongoni mwa hawa wanatarajiwa

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

HILI LA PAMBA NA TIMU ZA MWANZA, WASUKUMA MNACHEZA NGOMA GANI?

Tanzania Sports

Man City wapanda