Menu
in , , ,

Chelsea vs Liverpool 

Ni kasi na vipaji dhidi ya mfumo wa timu

ENZO Maresca ameibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza wa EPL dhidi ya Liverpool. Timu hizo zimekutana katika mchezo huo kwenye mfululizo wa Ligi Kuu England katika dimba la Stamford Bridge jijini London. Katika mchezo huo Enzo Maresca, kocha wa Chelsea alishangilia kwa nguvu ushindi w atimu yake baada ya winga Mbrazil, Estevao kupachika bao la ushindi akimalizia kazi nzuri ya timu kutoka wingi ya kushoto na kuwaacha solemba mabeki wa Liverppool. TANZANIASPORTS inachambua tofauti ya timu hizi mbili ambazo zimeonesha mchezo maridadi wikiendi hii.

Uhaba wa mawinga Liverpool 

Liverpool ni timu nzuri ikiwa katika mfumo ambao kila mchezaji anawajibika kujiunganisha na wenzake. Mfumo wa Liverpool unaifanya timu hiyo iwaweke kando mawinga asilia. Katika kikosi kilichoanza winga wa kulia alikuwa Mohammed Salah, angalau huyu ni winga asilia kuliko Gapko aliyecheza winga wa kushoto. Safu ya ushambuliaji ya Liverpool imekosa wachezaji wenye kasi kutokea pembeni jambo ambalo lilimpa uhuru mwingi Reece James alipotakiwa kucheza kama beki wa kati na hivyo kudhibiti upande wa kushoto wa Liverpool alikokuwa Gapko. Kukosa mawinga asilia mbadala na wa kucheza upande wa kushoto kunainyima Liverpool nafasi ya kutawala mchezo zaidi. Siri kubwa ni injini ya katikati ya dimba kwa McAllister, Szoboslai na Gravenburch. Ni sababu hiyo kocha wa Chelsea alifanya mabaidliko kupindi pili kumwingiza mchezaji mpya wa kwenda kudhibiti injini ya Liverpool katikati ya Dimba. Ukishawashika Liverpool katikati ya dimba wanakosa njia mbadala ya kuibuka na ushindi.

Miguu ya Isak ni kama nta

Tanzania Sports
Slot, kama vile anatafuna limau

Nta ni kitu ambacho kinatumika sana kutengeneza nywele kichwani na kuzifanya ziwe pamoja. Mchezaji aliyekuwa anapendelea kutumia Nta ni Didier Drogba staa wa zamani wa Chelsea. Nyota huyo raia wa Ivory Coast alipendelea kuweka nta kwenye nywele zake na kuzifanya ziwe na mwonekano mzuri na zikiwa zimeshikamana vyema. Kazi ya Nta ni kugandisha nywele na kuwa na mng’aro wa aina yake. Miguu ya mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak inaonekana kuwa na Nta. Jinsi ambavyo alitulia mpira ule, namna alivyomdhibiti beki wa Chelsea kisha akaupiga kidogo kwa kisigino kama vile alikuwa anamwandalia Gapko. Naye Gapko hakufanya masihara alitumia mwanya aliotengenezewa kupiga shuti kali kuelekea langoni mwa Chelsea na kuandika bao la kushawazisha. Isak ni aina ya mshambuliaji ambaye anatakiwa kutunza mali katika boksi la adui. Uwezo wa kutunza mali ili kuipa nafasi timu yake kupata bao ameonesha kiwnago cha juu na miguu yake ni kama in anta.

Kasi ya visheti wa Chelsea

Si haba, Chelsea wana mawinga na viungo wengi visheti; Gittens, Estevao, Neto, Pedro ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kucheza winga wa kulia, kushoto na nyuma ya mshambuliaji. Katika mchezo wao dhidi ya Liverpool, Enzo Maresca alihitaji nguvu ya kuwarudisha nyuma zaidi Liverpool kwani walipoingia kipindi cha pili walifanya mabadiliko zaidi ili kulinda eneo la kiungo mkabaji na ushambuliaji. Kocha wa Liverpool, Arne Slot alimtoa Ibrahim Konate na kumwingiza Jones ambaye alikuwa na kazi ya kulinda eneo la kiungo. Kana kwamba haitoshi Maresca alipoona Liverpool wanapandisha mashambulizi na huku wanamwingiza Endo katika eneo la kiungo maana yake walitaka kulisaka bao lingine. 

Alexander Isak . Ameanza vibaya…

Hata hivyo Enzo Maresca aliwaaingiza viungo wake wawili Gittens na Estevao ambao walisaidia kuipeleka mbele timu yao. mawinga hao walisababisha mabeki wa pembeni wa Liverpool warudi nyuma badala ya kusaidia mashambulizi. Kitendo hicho kilisababisha Liverpool wawe nyuma kulinda bao lao ambalo kuondoka na alama moja. Liverpool walikuwa wanakabiliana na timu ambayo inaonekana kutegemea viungo visheti wengi. Hawa ni aina ya viungo ambao kazi yao ni kuleta nakshi, ubunifu na kasi uwanjani ikiwa kukimbizana sana na mabeki wa timu pinzani. Kasi yao iliwafanya Liverpool waonekane kama vile wamechoka. Kasi ya viungo hawa ndiyo silaha ambayo imesaidia Chelsea kulinda uwanja wake na kuibuka na pointi tatu muhimu.

Mfumo wa nje-ndani

Enzo Maresca alirudia mbinu alizotumia dhidi ya PSG kwenye fainali ya klabu bingwa dunia nchini Marekani. Katika fainali hizo aliwafanya wachezaji wa pembeni wawe muhimu zaidi kuliko wale safu ya ushambuliaji. Kazi yake ilikuwa kuhakikisha mawinga wanatumia vipaji na kasi yao kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa wapinzani. Kwa mtindo huo wa kuwapanga mawinga wa kuongeza kazi maana yake aligundua kuwa njia pekee ya kuwarudisha nyuma mabeki wa Liverpool ni hiyo. Inafahamika kuwa mabeki wa Liverpool hawana kasi na hivyo hawawezi kukimbizana na wachezaji wenye kasi kama Estevao au Gittens. Kwa mfumo huu unaliacha eneo la namba tisa likiwa wazi, huku pembeni ndiko wanakoshughulikiwa wapinzani na mawinga wake wanaingia ndani kwa kasi baada ya kupiga pasi za krosi ama fupi fupi za haraka.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version