in , ,

Changamoto ya kufundisha timu ya Taifa Morocco

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Morocco ni mchanganyiko wa utamaduni ambao unawapa wakati mgumu makocha wengi waliowahi kupewa jukumu hilo. Hilo limelezwa na kocha mkuu wa nchi hiyo Walid Regragui wakati akizungumzia mashindano yajayo ya AFCON yanayotarajiw akufanyika nchini humo. Kocha huyo mkuu wa Morocco aliviambia vyombo vya habari kuwa amekutana na changamoto kubwa katika kuongoza timu ya taifa ya nchi hiyo. Kwenye mahojiano na jarida la French Sports amekiri kikosi chake kina utamaduni mchanganyiko na tofauti kubwa baina ya wachezaji wake. amaesema kufundisha kikosi chenye wachezaji wenye majina makubwa duniani si jambo rahisi, lakini amesisitiza kuwa mchanganyiko wa utamaduni ni suala muhimu linaloleta tofauti kikosini mwake na kukifanya kuwa kitu cha kipekee.

“Morocco tuna kikosi cha aina yake. Watu wanaweza kuongea lolote na wakatukosoa kwa kitu chochote, lakini ukweli ni kwamba timu ya taifa ya Morocco ni ngumu kuiongoza hapa duniani.” Alisema kocha Walid Regragui.

Regragui amefichua kuwa anazungumza lugha ya Darija ya Morocco na wachezaji wake, ingawaje si hodari wa lugha hiyo. Walid anaamini kuwa lugha ya Darija inamsaidia kutengeneza imani na mshikamano miongoni mwa wachezaji. Pia amesema lugha ya Darija huwa ya kwanza kwake ingawaje huwa anatumia mkalimani au njia nyingine ili kuhakikisha ujumbe wake unawafikia wachezaji wote. 

Kwa mujibu wa kocha huyo, “kwenye timu yetu tuna wachezaji wa Morocco kutoka sehemu mbalimbali. Kuna wachezaji wenye utamaduni kutoka Ligi ya Hispania, wengine wanacheza Ligi Kuu za Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi, Ujerumani na Italia, na sasa tunaona wengine wanacheza Ligi Kuu England. Tunao wachezaji hata kutoka Sahrawi wanaocheza Ligi Kuu Norway. Ni hali ya kufurahisha na kipekee sana, inatupatia nguvu, lakini pia inamaanisha kila mmoja anatoka kwenye utamaduni wake,”

Mbali ya changamoto hiyo, amesema kwamba kwa mchezaji kuichezea timu ya Taifa ya Morocco maarufu kama Simba wa Milima ya Atlas ni suala muhimu na la kujivunia. “Kimsingi Morocco, ndicho kitu muhimu katika kikosi chetu. Lakini wachezaji hao wote ni raia wa Morocco waliozaliwa na kukulia sehemu tofauti. Malezi na makuzi ya mchezaji anayeishi Hispania, hayafanani na yule aliyekulia Ufaransa, saw ana kusema haifanani na Uholanzi. Lakini kazi yangu ni kuwafanya wachezaji hawa wawe wamoja, wafanye kazi pamoja, lengo liwe moja kuifanya Morocco kuwa kitu cha kwanza katika maisha yao. ni wachezaji ambao wanakuwa kwenye kikosi chetu kwa malengo ya kuipigania timu ya taifa ya Morocco.”

Aidha, kocha huyu amesema kuwa njia anayotumia kuhakikisha wachezaji wanasimamia lengo moja la kuitumikia Morocco ni pamoja na kuangalia mahali anakotokea sasa. Kama mcehzaji anacheza Ligi Kuu Ufaransa atakuwa na mbinu tofauti za kuwasiliana naye ili amfikishie ujumbe unaoeleweka kwa maslahi ya Morocco. Hali kadhalika amesema mchezaji anayecheza Ligi Kuu Ujerumani au Hispania na ambaye ni raia wa Morocco (wana uraia pacha) anatumia mbinu nyingine zisizofanana kwa vile anaelewa tofauti za kiutamaduni kwa nchi hizo. 

“Kwa namna unavyozungumza na mtu unaweza kupata matokeo mawili; mabaya na mazuri iwe kwako au kwake. Mtu anaweza asielewe kile unachotaka kumwelewesha kwa sababu ya makuzi tofauti ya kiutamaduni. Unavyozungumza na mchezaji anaycheza Ufaransa ni tofauti na unavyoongea na mchezaji wa Morocco aliyezaliwa Ujerumani (German-Moroccan). Lakini kinachotuunganisha, na kwa pamoja ni mapenzi yetu kwa Timu ya Taifa ya Morocco, familia zao na asili yao ambayo ni Morocco. Wote wanathamini asili yao na wanapenda kuvaa jezi za timu ya taifa ya Morocco.”

Katika muktadha huo kocha huyo anakumbusha kuwa vipaji vingine vinakosa nafasi ya kurudi kwenye asili yao kwa sababu nchi hizo hazijaruhusu uraia pacha. Kwamba nchi ya Morocco imepokea changamoto ya tofauti za kiutamaduni na kugeuza kuwa njia ya mafanikio. Katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zilizofanyika huko nchini Qatar, timu ya taifa ya Morocco iliweka rekodi ya aina yake kuwa Taifa la kwanza kutoka barani Afrika kutinga hatua ya nusu fainali. Ingawaje haikufikia malengo ya kutinga fainali ya Kombe hilo, lakini tofauti zao za kiutamaduni ahzikuwa kikwazo kupata mafanikio.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Bila roho ngumu hamna mafanikio Man United

Tanzania Sports

Siku ya burudani na malalamiko imewadia